Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alichovumbua ndio biashara yake.Steve Jobs hao ni wavumbuzi. Sisi wa Africa utajiri wetu unakuja kwenye kukwepa kodi, kukwapua na kuwalalia wengine.
Unasema kwamba kampuni yake inakiuka taratibu za ajira?. Ni vizuri waajiriwa wake wakachukua jitihada za kudai haki zao. Huo ni uonevuMo watanzania tunampenda sana ila hapa hajaenda haki kusema ukweli wa viwanda vyake ku take off moja kubwa ni kuchukua viwanda kwa bei ya kutupwa ya mr Mkapa ila Pili muhimu sana ni very cheap labour . Ukiangalia Kwa mfano watu wanaofanya kwenye viwanda kama vya kuzalisha chuo a za plastic pale vingunguti unaweza kulia maana wafanya kazi wa kawaida wanashindwa hata kulipa koddi ya chumba uswahilini wakati wanalala na kukesha kwenye nashine zake za moto. Na mbaya zaidi wengine wanaumia kukatika vidole then mwisho wao hawalipwi . So labour imechamgia kwa kiwango kikubwa kwa utajiri wake ila pia management wanaendeleana sana hao kanji against waafrika . Ni shida
Amekutan
Siku zote ukizoea kula nawewe kubali kuliwa.
Makosa ni chamay Tawala kungangania madaraka name kudanganya eti wanaleta sera ya viwanda.Na tusiwateke watu kwa misingi ya wivu. Makosa ni ya Serikali ya Tanzania. Yeye alichangamkia fursa. Saizi ndo tunapata akili baada ya mali nyingi kumilikiwa na familia moja. Kazi sana nchi hii
Ninyi ndo watekaji wenyewe.Mnamo mwezi wa 06 mwaka 2018, Mohammed Dewji alifanya Mahojiano na mwandishi mashuhuri wa maswala ya biashara ndugu MFONOBONG NSEHE (http://www.campdenfb.com/author/mfonobong-nsehe). Mahojiano hayo yalichapishwa tarehe 19/06/2018 katika tovuti ya CampdenFB.com (http://www.campdenfb.com/article/tanzania-s-titan-mohammed-mo-dewji). Lengo kuu la mahojiano hayo ni kuonesha mafanikio na changamoto za kibiashara za Kampuni ya MeTL.
Hizi ni baadhi ya dondoo za mahojiano hayo:
Mohammed Dewji (MO); Nilianza kujifunza biashara nikiwa na umri wa miaka 11. Nilikuwa nikiuza duka pamoja na Baba yangu pale SINGIDA. Wakati wa likizo Baba alikuwa akiniambia, "Mohammedi, hii ni biashara ya familia hivyo unatakiwa kujua mbinu".
MO; Nilisoma maswala ya biashara nchini Marekani na baadae nilipata kazi ambayo nilikuwa nalipwa kama dola 60,000 kwa mwaka. Ilikuwa pesa nyingi kwa Maisha ya Tanzania, lakini haikuwa kitu kwa Maisha ya Marekani hususani gharama za Maisha pale New York nilipokuwa naishi. Mambo yangu hayakuwa vizuri. Hivyo, nilimwomba Mzee awe akinitumia pesa kidogo ya kujikumu wakati naendelea kupambana na Maisha lakini Mzee alikataa kata kata. Alisema, kwanini nahangaika kutafuta vijisenti na kukuza uchumi wa Marekani badala ya kurudi Tanzania na kuendeleza biashara za familia na kukuza uchumi wa Tanzania. Baada ya Maneno hayo, mwaka 1998 niliamua kupaki mizigo na kurudi Tanzania. Nilifanya kazi kwenye Kampuni ya MeTL kama Chief Financial Controller.
MO; Nilikuja na wazo la kuanzisha biashara ya viwanda ili kuzalisha baadhi ya bidhaa muhimu. Nilishangaa kwanini nchi yangu ilikuwa ikinunua hadi sabuni na mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati kulikuwa na fursa ya kuzalisha bidhaa hizo nchini. Hivyo, nilimshauri Mzee tuanzishe viwanda lakini alikataa. Mojwapo ya sababu ilikuwa ni swala zima la mtaji pamoja na uzoefu katika biashara hiyo.
MO; Ndoto yangu ya viwanda ilitimia Mwaka 2003. Wakati huo, Serikali ya awamu ya tatu ilichukua uamuzi wa kuuza viwanda vyote vilivyokuwa vikipata hasara na kuelekea kufilisika kutokana na uongozi mbovu, rushwa n.k. Mali hizi ziliuzwa kwa bei poa. Tulinunua viwanda, mashamba, magodown n.k. Kadri biashara ilivyozidi kupanuka ndivyo tuliendelea kununua mali zingine kutoka kwa makampuni na watu binafsi. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa sura mpya ya Kampuni ya MeTL.
MO; Makampuni makubwa ya Kilimo ya Kimataifa yamekuwa yakinijia kutaka kuwekeza katika kilimo lakini bado sijafikia uamuzi huo
MO; China haiwezi kushindana na mimi katika uzalishaji wa nguo. Kwa mwaka tunazalisha vitambaa vya nguo vyenye urefu unaoweza kuizunguka dunia zaidi ya mara 2,500.
Soma zaidi makala hiyo ili ujifunze mbinu za ujasiriamali pamoja na mchango wa Kampuni ya MeTL katika uchumi wa nchi ya Tanzania.
View attachment 906161View attachment 906162
Sharing is Caring
Hapo ndio unapoelewa maana ya msemo dunia duara. Unafurukuta weee, unawadhalilisha raia lakini baadae laana ya wananchi lazima ikupate tu. Hayo ndiyo maisha.Huwezi kuta Apple,Microsoft,etc zinasubiri kusaidiwa na serikali au wanasiasa!
Yote yanayosaidiwa mwisho wa siku ni aibu...
Ujinga kama Boeing ya USA ,BAE Systems ya UK,etc yameisha kupata aibu za mwaka....
Dewji nae ndio anavuna aliyopanda.....na bado....
Hiyo siyo tamthilia. Ni mahojiano ya moja kwa moja na mhusika mwenyewe. Kwahiyo kilichoandikwa hapo ni mia mia. Ukitaka kusoma makala yote bonyeza link hiyo ya pili. Ukweli ni kwamba serikali ya awamu ya 3 ndiyo imempa huyu jamaa utajiri, over"And he produces a highly popular energy drink called BOMBA,considered a redbull competitor".
Ukiwa mtu wa kusoma na kuamini kila unachosoma bila kuchuja utalishwa sana matango pori dunia hii.
Hakunyonya MTU,viwanda alivyouziwa,vilikuwa vimeishakufa,na vifo vyake vilisababishwa na majitu meusi kama sisi,yalivifisadi,yakavimalizaBasi aliwanyonya sn ndugu zetu wenye rangi nyeusi kwenye hayo maviwanda yao, ndio c wanajulikana walivyo wakax kwa wabongo