bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Takwimu mpya zinashtua na kuumiza kichwa kwa pamoja: Utajiri wa Dola Trilioni 1 ($1,000,000,000,000) wa Elon Musk unaweza kuendesha bajeti zote za Tanzania, Kenya, na Uganda kwa miaka 14 mfululizo!
Yaani mtu mmoja ana hela ya kulisha, kuhudumia, na kuendesha nchi tatu nzima za Afrika Mashariki hadi mwaka 2040, huku sisi huku mtaani tukipiga hesabu kali za kupata elfu mbili ya chipsi mayai!
Hapa kuna mambo 4 ya kuchekesha na kusikitisha kuhusu utajiri huu wa ajabu:
1. Kalkulator Inaomba Po! Ukijaribu kubadili $1 Trillion kwenda Shilingi za Kitanzania au za Kenya, kalkulator ya simu yako inajifunga yenyewe na kukuandikia SMS: "Ndugu mtumiaji, tafadhali pambana na umaskini wako, hapa umenizidi uwezo!" Zile sifuri pekee zikipangwa kwenye mstari, zinaanzia Dar es Salaam hadi Nairobi!
2. Elon Akiamua Kuwa Rais wa Kanda: Hela ya Musk inaweza kulipa madeni yote ya Afrika Mashariki, ikatujengea treni za SGR hadi milimani vijijini, ikalipa umeme na maji bure kwa miaka 10, na bado akabakiwa na chenji ya kununulia Ligi Kuu ya Uingereza!
3. Majuto ya Mshahara wa Mwezi: Wakati sisi mtaani tukisuguana na mwenye nyumba tarehe za mwisho wa mwezi kuhusu kodi ya chumba kimoja, Elon Musk anaweza kudondosha Dola Milioni 10 kwenye mfuko wa suruali aliyofua jana na asigundue kabisa kama kuna hela imepungua!
4. Mkataba wa Kustaafu: Hii ina maana Elon Musk akijisikia vibaya kesho, anaweza kuja East Africa na kusema: "Ninyi maraisi pumzikeni, nimeshawalipia bajeti ya miaka 14 ijayo. Kila raia akae nyumbani ale na alale!"
Usiseme wote hatuwezi kuwa matajiri wote na nanii? Jisemee wewe mwenyewe😁😁