Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 08.

Baada ya siku mbili,yule jamaa aliyekuwa mpangaji mwenzangu aliyeitwa Steve alinifuata akawa ameniambia Team leader amekubali.

Steve "Kaka jiandae kesho nikupeleke maana nilizungumza na team leader akaniambia twende"

Mimi "Sawa kaka"

Kweli,tuliondoka na Steve hadi Buguruni kulikokuwa na ofisi ya Tigo,nilipofika hapo nilikuta kuna vijana wengi wakiwa mchanganyiko(KE & ME) na kiukweli kulikuwa na mabinti wazuri sana,Steve aliniambia nifuatane nae hadi ndani na tulipofika ndani alimuita huyo aliyekuwa Team leader akaja nilipokuwa nimesimama.

Steve "Kiongozi huyu mshikaji ndiye nilikwambia ile juzi anahitaji Code"

Team leader " Aahh ok!"

Aliendelea "Hebu nisubirini kidogo nina mazungumzo nakuja!"

Team leader aliondoka akawa ametuacha pale na Steve,Steve nae akawa yuko bize kupiga stori na washikaji zake wengine ambao pia walikuwa wakifanya kazi ya usajili wa line.Baada ya dakika 20 yule Team leader akawa amerudi.

Team leader "Unaitwa nani ndugu?"
Mimi "Naitwa Umughaka"

Team leader "Kanda ya ziwa nini!"

Mimi "Yeah"

Team leader "Ok,sasa nitakupa line ya Code kwa ajili ya kusajilia,na process zote inabidi ukamilishe muda huu ili uondoke na Steven akakuonyeshe kazi inavyofanyika"

Aliendelea "The more u register customers,the more u get more money"

Team leader "Kwa kanuni za sasa kwenye kampuni ni kwamba,kila freelancer atakuwa anapokea Revenue shares every month within six months"

Aliendelea "Mambo mengine yote Steven atakuelekeza"

Team leader "Steve hakikisha jamaa anakuwa poa"

Steve "Hakuna tatizo kiongozi"

Baada ya ufafanuzi mdogo ambao sikuelewa chochote,Team leader aliingia ndani akawa ametoka na tisheti mbili za Tigo zikiwa mpya zenye maandishi yaliyosomeka "Sajili line yako Tigo hapa",pia aliniletea Kofia, na kizibao,hivi vyote vilikuwa na maandishi yaliyohusu kampuni ya mawasiliano ya Tigo.

Team leader "Ukishaelewa tunavyofanya kazi,wiki ijayo nitakupatia Mwamvuli na meza ili uwe na chimbo lako,au unataka kupiga door to door?"

Mimi "Door to door ndo kitu gani?"

Team leader "Naamanisha uwe unasajili laini kwa kutembea tembea?"

Mimi "Nadhani nipe muda nitakujuza njia ipi kwangu itakuwa bora zaidi!"

Team leader "Ok,hakikisha kila siku asubuhi hukosi hapa ofisini kuanzia saa 1 : 30 uwe hapa maana kila siku kuna kuwa na vikao vya maelekezo"

Mimi "sawa,hakuna tatizo"

Baada ya maelekezo hayo,Team leader alimpatia Steve boksi mpya la laini za simu ambazo hazijasajiliwa na kumtaka anielekeze namna ya kusajili wateja.Tuliondoka na Steve kuelekea Tandika ambako yeye alikuwa akifanyia Shughuli zake huko za kusajili line,sasa tulipofika hapo Tandika jamaa alikuwa na tenti lake kubwa (Gazebo) ambalo lilikuwa la kampuni ya Tigo,tulipofika hapo kuna demu tulimkuta ambaye alikuwa na wateja,yule demu alikuwa akishirikiana na Steve kwenye lile tenti kusajili line.

Wateja walivyokuwa wakija nilikuwa nikielekezwa namna ya kusajili line za simu na kiukweli nilielewa ile kazi kwa muda mfupi sana na nikawa nafanya vizuri sana kuwashinda hata niliowakuta mwanzo.Nifahamu hadi kurudisha line za simu zilipotea na nilifahamu mambo mengi sana na nikawa mnyama sana kwenye ile kazi ya usajili wa line.

Baada ya mwezi kuisha na kupokea malipo,Steve alinishauri niongee na Team leader anipatie Meza na mwamvuli niweke kambi sehemu yenye watu wengi niendelee kupiga kazi.

Steve "Kaka kwakuwa umeshakuwa mzoefu,mwambie Kiongozi akupe mwamvuli na meza upige kazi"

Aliendelea "Au unataka kuparasa?"

Mimi "Kuparasa ndo kufanyaje?"

Steve"Kuparasa ni kupiga door to door,kuna wana wanaita kuparasa"

Mimi "Ni bora nitulie sehemu kaka,hili jua na ishu ya kutembea siyo poa"

Steve "Basi mwambie kiongozi akupe meza na mwamvuli au akupe Gazebo kabisa ila utakuwa unakatwa hela"

Niliona alichokuwa ananiambia Steve ni jambo jema kwasababu nisingeendelea tena kukaa pale kwenye Gazebo lao tukiendelea kugawana wateja.Siku iliyofuata baada ya kufika ofisini pale Buguruni,nilimwambia Team leader anipatie Mwamvuli na meza kama vipi niangalie chimbo ambalo litanifaa kupiga kazi.

Team leader "Sasa umepata chimbo la kuweka meza?"

Mimi "Nitatafuta kulekule Tandika kiongozi"

Team leader "Tandika watu wangu wamejaa sana,kwanini usiende kariakoo maana kule kuna watu wengi pia hii itakuongezea revenue maana kule watu wanahela za kuweka vocha"

Mimi "Ok sawa kiongozi ngoja niingie Kariakoo"

Baada ya kunipatia vitendea kazi(Mwamvuli na Meza) nilipanda gari pale Buguruni kuelekea Kariakoo kwa ajili ya kutafuta chimbo la kufanya kazi.Nilitafuta sana sehemu nitakayoweka meza ili nipige kazi,sasa niliingia mtaa wa Lindi lakini nikakuta kuna jamaa wengi tu wwameweka meza zao za usajili hapo na hivyo nikawa nimekosa eneo.

Nilitembea kuelekea mbele hadi nikawa nimeikamata barabara ya Kamata/Msimbazi road.Sasa kuna duka moja lilikuwa la vyombo vya electronic ambapo pembeni yake kulikuwa na duka dogo la simu,duka hilo ni miongoni mwa maduka ambayo leo yanakitazama kituo cha mwendokasi pale Gerezani,sasa pembeni yake nikaenda kuweka meza,kabla ya kuweka meza nikasogea mpaka kwenye lile duka nikakuta kuna mwanamke wa kiarabu aliyekuwa amejifunika vazi la Nikabu.

Mwanamke "Karibu"

Mimi "Ahsante"

Mimi "Aunt samahani,mimi nafanya kazi ya kusajili line kutoka Tigo,naomba niweke meza hapa pembeni"

Mwanamke "Mmmh hebu tuone"

Yule mwanamke alitoka dukani akawa amekuja nje kuchungulia kuangalia ni eneo lipi ambalo nilikuwa nahitaji kuweka meza na mwamvuli.

Mwanamke "Sawa,utasogeza kidogo pembeni ili usiwakinge wateja"

Mimi "Nashukuru sana Aunt"

Mwanamke "Usijali "

Nilifungua ile meza kutoka kwenye boksi pamoja na ule mwamvuli kisha nikawa nimesimama nasubuiri wateja,changamoto siku hiyo ilikuwa ni kiti,nilipanga kesho yake ningenunua kiti cha kukalia kwasababu pesa nilikuwa nimeacha nyumbani.Japo ilikuwa siku ya kwanza hapo Kariakoo lakini kazi ilifanyika sana na kumbuka nilisajili line 55 kwa siku hiyo moja!.

Maisha yalisonga na nikawa nishakuwa mzoefu sana wa ile kazi,sasa hapo jirani yangu kwenye lile duka la yule dada kulikuwa na huduma za miamala ya kifedha(TIGO,VODA,AIRTEL) ambapo nilipokuwa nikisajili line mteja akihitaji nimuweke pesa kwenye akaunti yake ya Tigo pesa,nilikuwa naingia tu kwenye lile duka!.Ile ilifanya nikazoeleka na taratibu nikawa najulikana.Kuna siku nyingine asipokuwepo yule dada basi utamkuta mumewe,hivyo wote kwa pamoja wakawa wamenizoea.

Niliifanya kazi ya kusajili line za simu kwa uaminifu mkubwa na kwa roho moja kana kwamba ile kampuni ilikuwa ya familia yangu,nilihakikisha naweka na kuhifadhi pesa ili nije nifanye mambo makubwa nilikuwa ninayawaza,nilikuwa nina uchungu sana baada ya Kileri kutafuna pesa yangu ya mtaji niliyokuwa nimempatia.

Sasa kuna siku nikiwa nimetoka kwenye mihangaiko yangu hiyo ya kusajili line nikiwa nimefika pale nyumbani nilikuta kuna zogo la Steve na demu wake.Niliingia zangu ndani kisha nikaingia bafuni kuoga ili nipike nile kisha nilale.Malumbano ya jamaa na demu wake yalikuwa makubwa mno kiasi kwamba jamaa akaja kunigongea mlango huku akilia.

Steve "Kaka njoo unisaidie kunibemebelezea shemeji yako kaka"

Nilimshangaa Steve namna alivyokuwa akitiririsha machozi kana kwamba amefiwa.

Mimi "Kuna nini?"

Steve "We njoo kaka"

Hicho kidemu cha jamaa kilikuwa ni kidemu fulani kilichokuwa kinambabaisha sana jamaa na sikuwahi kuelewa uenda jamaa atakuwa alirogwa kwasababu alikuwaga haambiliki kabisa kwa kile kidemu,nisiseme uongo,kidemu kilikuwa kizuri na kilikuwa na shepu isiyokuwa ya kawaida,sasa labda uenda Steve alichanganyikiwa na kile kishepu,kile kidemu kilikuwa kijitu cha Mtwara kwa mujibu wa Steve na walikutana kwenye pilika zetu hizo za usajili wa line.

Jina la huyo demu alikuwa akiitwa Zubeda ila Steve alikuwa akimuita Zuu.

Niliondoka na jamaa kuelekea hadi ndani kwake ambako kilikuwa chumba kimoja,nilipoingia ndani nilikuta kidemu kimelala kimeweka matako juu huku kinaendelea kuchezea kiswanswadu chake huku hakina habari kabisa na mtu!.

Mimi "Shem mambo vipi"

Zubeda "poa"

Sasa kilikuwa kinajibu huku kinaendelea kuchezea simu.

Mimi "Kuna nini shemeji yangu maana naona jamaa analia tu kama kichaa"

Zubeda "Ndo umwambie akueleze kinachomliza ni kitu gani!"

Muda huo wote naongea nae bado alikuwa bize akicheza na simu yake na akiwa hana habari kabisa.

Mimi "Shem muhurumie mwenzio yawezakana umemkosea"

Zubeda "Nimemkosea kitu gani bwana eeeh na wewe usitake kunichosha"

Aliendelea "Huyo kinachomliza ni wivu tu wakijinga"

Zubeda "Sikia,kuna mwanaume niliwahi kuwa nae kwenye uhusiano na alikuwa akinidai hela yake aliwahi kunipatia mtaji sasa tulipoachana akataka nimrudishie hela yake,ndiyo nikawa nimemuelekeza aje achukue hela yake"

Steve "Mtu mmeachana na bado mnawasiliana nae kila siku usiku anakupigia simu"

Zubeda "Sasa kwani kunipigia simu ndiyo kurudiana nae?"

Steve "Ungeenda sasa kumpatia huko siyo kumwambia aje hapa nyumbani kwangu"

Kwa maelezo ya Steve ni kwamba,huyo jamaa yake na hako kademu kake alikwenda hapo nyumbani kwa Steve wakati jamaa akiwa kazini kwake huko Tandika,ni nilikuka kufahamu ya kwamba kilichokuwa kinamliza Steve ni kuamini huyo demu wake atakuwa ametombewa ndani kwenye gheto lake kwasababu tabia za demu wake alizifahamu kabisa alikuwa hajatulia.

Yule demu alikuwa anambabaisha sana Steve kwa kufahamu alikuwa anampenda,na wewe fikiria pesa zote jamaa ambazo alikuwa akipata kama Kamisheni kwa kusajili laini alikuwa akikapa hako kademu.

Zubeda "Ndiyo maana nimekwambia ngoja niondoke,kwanini unafungia mlango?"

Mimi "Shem hebu yaacheni haya mambo bana"

Zubeda "Mimi unadhani basi nina tatizo shem,ni huyo mwenzio ndiyo ananifikiria vibaya"

Basi baada ya usuluhishi kutoka kwa msuluhishaji wa migogoro ya kimapenzi(Rejea kwa Ema na Deborah) niliyekuwa na uzoefu wa kutosha,niliamua kuondoka mle chumbani kwa jamaa ili wao wenyewe waendelee kupambana.

Kuna muda nilikuwa namshauri Steve aachane na yule demu lakini ni kama nilikuwa nampigia mbuzi gitaa,yule demu alikuwa na sifa mbaya kiasi kwamba kuna masela kadhaa pale mtaani tulipokuwa tunakaa nilikuwa nasikia wanapita nako na kila nikijaribu kumueleza jamaa anajifanya kama ameelewa lakini kumbe yanapitia huku yanatokea kule.

Sasa kuna siku nikiwa kariakoo napiga kazi,kuna dingi mmoja alikuwa na duka pembeni ya ile nyumba akawa amenipigia simu.

Itaendelea........
Chezea wadada wa mtwara hasa masasi ha ha ha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 09.

Mwenye duka "Mambo vipi?"

Mimi "Shwari"

Mwenye duka "Jamaa yako anahama nini!"

Mimi "Nani?"

Mwenye duka "Jamaa yako na Mmakonde wake!"

Mimi "Steve?"

Mwenye duka "Eeh!"

Mimi "Wanahama lini?"

Mwenye duka "Naona wanapakia vitu kwenye Suzuki carry"

Mimi "Mbona hajaniambia!"

Mwenye duka "Nyie si marafiki!,ina maana rafiki yako anahama wewe hujui!"

Mimi "Labda wameona waondoke kimya kimya kaka"

Mwenye duka "Sawa bhana baadae"

Baada ya huyo mwenye duka kukata simu nilibaki kushangaa kwasababu zilikuwa ni sababu zipi zinafanya Steve ahame bila kunipa taarifa kama mshikaji wake wa karibu?,nilidhani uenda aliamua kuhama kwasababu alishachoka maneno mengi kuhusu huyo mkewe yaliyokuwa yakizungumzwa hapo mtaani,niliamua kumpigia simu ili kufahamu kilichokuwa kinaendelea na kwanini asiniage kama rafiki yake?

Nilipopiga simu yake ikawa inaita tu bila kupokelewa,nikapiga tena lakini ikawa haipokelewi,baada ya dakika 15 jamaa akanipigia yeye mwenyewe.

Steve "Kaka nilikuwa bize na mteja,nambie mwanangu"

Mimi "Uko Tandika?"

Steve "Yeah niko Tandika"

Mimi "Duuu mi nadhani uko maskani!"

Steve "Mapema yote hii kaka nyumbani nitafute nini?"

Mimi "Kwani pale nyumbani unahama?"

Steve "Nahama?,nahama naenda wapi?"

Mimi "Mbona nimepigiwa simu na mzee beda anasema mkeo anapakia vyombo kwe gari hivyo alidhani mnahama!"

Steve "Unasema?"

Mimi "Mpigie mzee beda umuulize"

Baada ya mazungumzo hayo ambayo ni kama yalimshitua Steve,alikata simu akawa amempigia yule jamaa aliyekuwa na duka kando ya nyumba tulivyokuwa tumepanga.Haukupita muda Steve akawa amenipigia simu tena.

Steve "Kaka ngoja kwanza niwahi nyumbani"

Mimi "Ni kweli?"

Steve "Ni kweli kaka"

Mimi "Anapeleka wapi vyombo au anatoroka?"

Steve "Ngoja niwahi kaka!"

Jamaa alionekana kupagawa sana na asijue ni kitu gani cha kufanya,kiukweli yule demu nilishamshauri sana kama mshikaji wake aachane nae lakini jamaa nikama alikuwa amerogwa,yule demu alikuwa akimfanyia vituko vya kila aina lakini Steve alikuwa haambiliki wala ashauriki,sikuwahi kuelewa ni kitu gani kilimfanya Steve apagawe kwa kile kitoto cha kimakonde.Pasipokuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea,mimi niliendelea kupiga zangu kazi kama kawaida.

Ilipofika mida ya saa 11 jioni,Steve akawa amenipigia simu tena akiwa analia kana kwamba kafiwa.

Steve "Kaka Zubeda kaondoka"

Mimi "Acha kulia mwanangu nakuja muda siyo mrefu"

Steve "Kaka Zuu wangu wamemchukua"

Mimi "Nakuja kaka wewe nisubiri"

Jamaa alikuwa akilia kama tahira,sikujua Steve alikuwaga akisimbuliwa na kitu gani kwasababu jamaa alikuwa na sura ya kirembo(Handsome) na kiukweli ungemuona usingedhani kama alikuwa mpumbavu wa kulilia mwanamke kiasi kile.Ilipofika saa 11 : 30 niliamua kukunja ile meza pamoja na mwamvuli nikapeleka mahali ambapo nilikuwa natunzia kila siku,mwaka ule ilipokuwa ikifika saa 12 : 00 jioni na usajili pia ulikuwa unasitishwa,sasa wakati naondoka yule brother wa lile duka la simu(Sitamtaja jina lake halisi kwasababu maalumu,hivyo nitampatia jina la Ally Mpemba) akawa ameniita na mara zote nikiwa pale alikuwa akiniita "Master",alipenda kuniita kwa utani hivyo kwasababu alikuwa akiona shughuli niliyokuwa nikiifanya ndipo akawa ananiita hivyo Master,alikuwaga ananiambia "Aisee wewe nakukubali sana,wewe ni master wa hizi kazi".Kwahiyo ikaenda kimzaha mzaha hivyo hadi akawa ananiita master,jamaa alikuwa ni mpemba lakini vilevile alikuwa mwarabu,nadhani tunafahamu jamaa wanavyokuwaga.

Ally Mpemba "Mbona wawahi kufunga leo,kunani!"

Mimi "Ndiyo muda wenyewe huu kaka"

Ally mpemba "Aaah Master siyo kawaida yako!"

Mimi "Kuna ishu naiwahi maskani kaka"

Ally mpemba "Kesho nikitoka kuswali,tuonane basi!"

Mimi "Tutaonana kaka,si utakuwepo?"

Ally mwarabu "Nadhani nitakuwa kule Aggrey,hapa atakuwepo dada yako"

Mimi "Sawa kaka haina tatizo"

Sasa kumbe mara zote mimi nimekuwa nikifikiria yule Aunt ninayemkuta pale dukani anayependa kujifunika Nikabu ni mkewe kumbe alikuwa ni dada yake;baada ya mazungumzo na Ally niliondoka zangu kwenda kufukuzana na magari ya Gongo la mboto.

Namshukuru Mungu niliingia Gongo la mboto mida ya saa 1 usiku,nilipofika pale nyumbani nilikuta Steve amekaa kwenye mlango wa chumba chake,nilipitiliza moja kwa moja hadi kwa Steve.

Mimi "Vipi?"

Steve "Ali siyo poa kaka"

Niliingia ndani ya kile chumba nikakuta vitu muhimu vyote vimekombwa na yule demu wake,alichokuwa ameacha ni vyombo vya kupikia tu,lakini TV chogo,friji,jiko la gesi,mashuka na vitu vidogo vidogo vyote alikomba.

Mimi "Aiseee,sasa utafanyaje?"

Steve "Nampigia simu zangu hapokei!"

Mimi "Kwani mligombana jana?"

Steve "Tangu siku ile kaka huwezi amini sijagombana nae"

Mimi "Kwani kwao ni wapi?"

Steve "Kwao Mtwara kaka ila yupo dada yake pale Mombasa ndipo alipokuwa anakaa kabla sijamchukua"

Mimi "Dada yake ushampigia simu?"

Steve "Nimempigia akaniambia huyo hawezi kwenda sehemu nyingine zaidi ya kwa bwana ake wa zamani kwasababu hapa mjini hana ndugu mwingine tofauti na yeye"

Mimi "Kwahiyo na wewe umekubali aondoke na vyombo vyako kwenda kwa bwana ake huyo?"

Steve "Sasa kaka nitafanyaje?"

Kiukweli nilitamani kumzibua mabao ya kutosha yule jamaa kwa upumbavu alokuwa akiongea mbele yangu lakini niliamua kuwa mtulivu kwasababu mambo yao yalikuwa hayanihusu,kilichokuwa kinanikwaza ni namna Steve alikuwa akiumia lakini kila ukimuongelea huyo demu vibaya ni kama anachukia,sikujua yule jamaa alipewa nini na yule demu aisee!.

Mimi "Huyo mshikaji wake unamfahamu?"

Steve "Kama ndiye huyo dada yake aliyeniambia namfahamu kaka na mara kadhaa tu nimekuwa nikimfata hapo"

Mimi "Daaah ila wewe jamaa nae,sasa unafahamu kabisa demu wako anakusaliti halafu bado unaendelea nae kweli,hata kama ni kupenda mwanangu wewe umepitiliza"

Steve "Nisindikize kaka mi nikafate vyombo vyangu tu"

Mimi "Ni wapi?"

Steve "Ni hapo Pugu kajiungeni"

Sasa nilitoka nje kwenda kupiga strori kadhaa na yule jamaa wa dukani na kweli alisema ile Suzuki carry ilielekea uelekeo wa njia ya Pugu na jamaa pia alishangaa namna Steve alivyokuwa bwege kiasi kile.

Tuliondoka huo usiku kuelekea Pugu kajiungeni,tulipofika Steve aliamua kuniongoza hadi hapo kwenye hiyo nyumba aliyokuwa anakaa huyo jamaa ambaye alikuwa anamgonga huyo demu wake.Tulipofika Steve akaanza kugonga kile chumba ambacho kilikuwa kimefungwa kwa ndani,baada ya kugonga sana alitoka jamaa mmoja chokoraa tu akiwa kifua wazi.

Jamaa "Vipi"

Steve "Poa,Zuu yupo?"

Jamaa "Zuu?,Zuu yupi?"

Steve "Sadi hebu achana na maswali ya kisenge,ina maana wewe leo humjui Zuu?"

Jamaa "Zuu wapo wengi sijui wewe unamtafuta yupi!"

Steve "Demu wangu"

Jamaa "Sasa demu wako hapa kafata nini!"

Muda huo niko pembeni nasikiliza yale malumbano nilikuwa nimechukia kishenzi,kibaya zaidi kuna majirani ambao nao walikuwa wamepanga kwenye ile nyumba walikuwa nje wakipika huku wakisikiliza na kujionea lile sekeseke.Baada ya kuona wanaigiza niliamua kusogea karibu na kumuuliza swali yule dogo.

Mimi "Wewe zuu unamjua au humjui?"

Jamaa "Brother,huyo Zuu anayemuongelea huyu ni demu wangu"

Mimi "Yupo au hayupo?"

Jamaa "Yupo!"

Mimi "Basi muite"

Jamaa baada ya kuona niko serious alifunga ule mlango akarudi ndani kisha akawa ametoka na kile kidemu.Baada ya kutoka Steve alibaki kujing'ata ng'ata hata kuongea ni kama alishindwa.Baada ya kuona jamaa haongei anabaki kushangaa ilibidi niingilie kati.

Mimi "Vitu vya jamaa viko wapi?"

Zubeda "Vitu gani?"

Mimi "Kwani wewe umechukua vitu gani?"

Zubeda "Vitu nilivyochukua ni vyangu,mmh kuna swali lingine!"

Mimi "Steve hebu pambana na demu wako mi naondoka"

Steve "Kaka usiniache"

Mimi "Kilichotuleta huku ni vitu na unasikia anasema si vyako,sasa hapa tunafanya nini?"

Steve "Zuu hivyo vitu ni vyako unauhakika?"

Zubeda "Nishasema vitu nilivyochukua ni vyangu,vyako nimekuachia nadhani umevikuta"

Steve "Naomba nichukue vitu vyangu nisije kufanya vurugu hapa"

Zubeda "Weeeee ishia hapo hapo,ina maana ulikuwa unanitomba bure!"

Aliendelea "Ina maana ulikuwa unanifira bure?"

Zubeda "Acha ujinga firauni wewe"

Aliendelea "Yaani ulidhani huu mwili niwa kushikwa bure bure tu!"

Yale maneno machafu yalipelekea wale kina mama kuanza kucheka,nilimwambia Steve tuondoke,japo jamaa alikuwa akitetemeka lakini niliamua kumuondoa lile eneo na kuondoka zetu,kiukweli kile kidemu hakikuwaga na aibu hata kidogo na nilikuwa namshangaa sana Steve anawezaje kuwaacha mademu wakali wa pale ofisini akaenda kutembea na kile kichakubimbi.

Mimi "Vitu vinanunuliwa we tuondoke!"

Steve "Kaka ila Zuu nampenda,siwezi kuondoka nikamuacha kaka ni bora nife"

Mimi "Yaani unaona bora ufe kwa ajili ya mwanamke?"

Mimi "Ok,rudi ukafe!"

Niliondoka zangu lile eneo nikamuacha jamaa akiwa amekaa chini machozi yakimtoka kama tahira.Baada ya kufika nyumbani nilipika msosi nikala kisha nikaingia chumbani kulala.

Itaendelea.........
Alisagiwa limbwata la kimakonde [emoji3][emoji3][emoji3]

Kichakubimbi 😅😅😅

ili neno limenikumbusha kanda ya ziwa enzi hizo -maana yake kimalaya
 
in
Duu pole sana, lakini tukirudi nyuma kabisa UMUGHAKA, hiyo hela chanzo chake ulikopata ni pesa ya ukakasi yawezekana Mungu alitaka uwe msafi [emoji3][emoji3] kwahiyo ilirudi kwao, ila pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
una akili sana,wengi wana laumu tu,ooh utampaje mtu m9,kirahisi hivyo we mjinga,kumbe hawajui ukiua kwa upanga,na wewe utauwawa kwa upanga,maisha ni mzunguko,yale unayofanyia wengine yawe mabaya au mazuri,siku moja yatakurudia tu na nyongeza juu,hiyo ni kanuni ya maumbile ya asili ambayo Mungu ameifanya,inajiendesha yenyewe automatic,upende usipende lazima siku moja yatakurudia tu...
 
Usipanic relax… unavotishia kumnyima KURA je umewaza yeye anavopoteza muda wake na BUNDLE LAKE kutuburudisha sisi BURE ?? Huu ni mkasa wa 3 Umughaka anatuhadithia na zote alimalizia HAKUISHIA NJIANI na zote zinazidiana kwa uhondo. Nae ni Binadam maybe yupo Busy kula Christmas na Family yake au busy na Wateja. TUSIWE WABINAFSI.
heri ya christmas mkuu karibu malinyi tumwage mpunga mvua imechanganya matrekta yakugombania n'gombe wakugombania kila mwenye kitendea kazi anaringa
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 10.

Nilishitushwa na sauti ya Steve akiwa ananiita na kunigongea akitaka nimfungulie mlango,nilipochukua simu na kutazama muda ilikuwa imefika saa 4.Niliamka nikaenda kumfungulia jamaa mlango,kiukweli alionekana hayuko kawaida na sikutaka kumpa presha,nilimwambia aingie alale atulize akili.

Namshukuru Mungu kulipokucha,mimi niliwahi kuondoka nikamuacha jamaa akiwa amelala,kabla ya kwenda Kariakoo ilikuwa ni lazima kila msajili line kupitia pale ofisini Buguruni kusikiliza kikao na mambo mapya kisha kuelekea kwenye kituo chake cha kazi,nami ndivyo nilivyofanya!.Nilipofika Kariakoo nilielekea eneo ambalo nilikuwa nikihifadhia vitu vyangu vya kazi na kuja kuanza kupiga kazi.

Sasa wakati nafika pale,lile duka la Ally mpemba lilikuwa bado halijafunguliwa,mi niliweka zangu meza nikaanza kupiga kazi kawa kawaida,kiukweli kwa kipindi kile kulikuwa na wateja wengi mno,yaani ilikuwa ukifungua tu ile saa 2 asubuhi wateja wanaanza.Ilipofika mida ya saa 3 asubuhi,kuna gari aina ya Range Sport nyeusi iliyokuwa na Private Number iliyoandikwa " SALIM " ilisimama pembeni yangu kisha ukafunguliwa mlango akawa ameshuka yule Aunt ndugu yake na Ally Mpemba.

Aunt "Leo umeniwahi"

Mimi "Leo nimekuwahi Aunt,salama lakini"

Aunt "Mie niko salama kabisa sijui wewe huko utokako"

Mimi "Salama kabisa"

Wakati nikiwa naendelea kuzungumza na Aunt ile gari ikawa imeondoka kuelekea Kamata.Yule Aunt pamoja na ndugu yake Ally Mpemba walikuwa wakizungumza kiswahili cha kipwani pwani kama ambavyo wazanzibar wakizungumza!.

Ilipofika mida ya 5 asubuhi,alinipigia simu Steve na akawa ananiambia ya kwamba,yule demu wake wamekubaliana arudi nyumbani na yeye amemsamehe ili mambo mengine yaendelee,mimi kwakuwa nilishamshauri sana kuonekana kama natwanga maji kwenye kinu nilimwambia sawa,hakuna tatizo,sikutaka kabisa kuwashauri kwasababu niliona ni kama nilikuwa napoteza muda.

Mimi "Kwahiyo vitu anarudisha?"

Steve "Ndo naenda kuvichukua kaka"

Mimi "Kwahiyo Leo hujaenda Tandika"

Steve "Leo siendi kaka ngoja kwanza nikamchukue huyu"

Mimi "Poa,kama ukitoka funguo utaniwekea juu ya mlango hapo"

Steve "Leo sina ratiba ya kutoka kaka"

Mimi "Sawa,baadae"

Safari hii niliamua nikae pembeni katika kushuri kwasababu nilichokuja kugundua ni kwamba,mambo yote ya msingi niliyokuwa nikimshauri jamaa kuhusu demu wake,yeye alikuwa akimwambia kila kitu na hivyo mimi kuonekana mchonganishi!,hivyo nikaamua sitokaa tena nimshauri na kama ni kufa yeye afe tu!.

Ilipofika mida ya saa 9 mchana,Ally Mpemba akawa amekuja akiwa ndani ya kanzu nyeupe,alipofika pale nje kabla ya kuingia ndani ya duka lake akawa amenisalimu.

Ally mpemba "Assalam aleykum"

Mimi "Alekom salam"

Ally mpemba "Kwema?"

Mimi "Kwema kaka"

Ally mpemba "Leo wafunga saa ngapi?"

Mimi "Kama kawaida kaka saa 12"

Ally mpemba "Basi utanipa muda wako kidogo Leo sheikh"

Mimi "Sawa kaka"

Sasa mida ya saa 10 alasiri alipokuwa anatoka pale dukani akawa ameniomba kama itawezekana tuondoke wote kuelekea Aggrey.

Mimi "Si hakuna haja ya kutoa vitu vyangu"

Ally mpemba "We viache tu,nishamwambia Farah atakuangalizia usijali"

Niliondoka na Ally kuelekea mtaa wa Aggrey ambako huko nako nilikuta kuna duka kubwa la simu na ndani yake kukiwa na wafanyakazi kama 4 wakisaidiana kuuza,sasa tofauti na kule ni kwamba lile la kule niliko lilikuwa dogo na la pale Aggrey lilikuwa kubwa.

Ally mpemba "Mi huwa nashinda hapa mara zote,nisipokuwa kule basi wanipata hapa"

Mimi "Ok sawa kaka lete maneno"

Ally mpemba "Kuna kazi nataka unisaidie Master"

Mimi "Kazi gani tena kaka?"

Ally Mpemba "Ni kazi ya kawaida tu!"

Aliendelea "Mimi ninahusika pia na mambo ya caterings na nimewaajiri ndugu wa familia na watu wengine lakini ndugu zangu ni watu wa ovyo sana huwa hawapendi kazi za kujishughulisha wao wanapenda kukaa kama hivi unavyowaona"

Ally Mpemba "Sasa kila ninapokutazama nakuona wewe ni mpambanaji mtu wa bara na ndiyo maana nakuita Master"

Aliendelea "Mimi nataka tu unisaidie kitu kimoja na offcouse siyo msaada bali nataka tufanye kazi"

Mimi "Sawa kaka"

Ally Mpemba "Kwani huko Tigo mnalipana shi ngapi?"

Mimi "Kaka kule ninalipwa kwa kamisheni"

Ally Mpemba "Sawa naelewa ni kamisheni lakini malipo yao huwa yapoje?"

Mimi "Inategemea na laini nilizosajili na matumizi ya wateja kwa mwezi husika"

Ally Mpemba "Doo kwahiyo mteja asipotumia laini hulipwi!"

Mimi "Ni mara chache mteja aje kusajili line na asiitumie,sema huwa malipo yanategemea,kuna muda yanapungua na kuna muda yanaongezeka"

Ally Mpemba "Ok sasa mimi nataka unisimamie kwenye mradi wangu hata kwa muda wa mwezi tu Master halafu nikipata mtu muaminifu nitamuweka halafu wewe utaendelea na shughuli zako:

Mimi "Kaka kwanini mimi?"

Allya Mpemba "Mi unajua nilikuwa sikutilii maanani sana,kuna siku Farah akaniambia wewe ni mtu poa sana hata namna unavyo behave,kwa maana nilipokuta umeweka meza yako kando ya duka langu nilimwambia Farah unapaswa utoke pale ila akaniambia wewe ni mtu poa sana"

Aliendelea "Ninachotaka mimi ni kwamba,wafanyakazi wapo ila wewe ukanisimamie tu maana alikuwa anasimamia mama yangu mdogo lakini yuko Unguja anamuuguza me wake!"

Aliendelea "Wewe niambie tu unataka niwe nakulipa shi ngapi?"

Mimi "Kaka unajua sijawa na uzoefu na kazi unayotaka niifanye,hivyo itakuwa ngumu kujua unilipeje kaka"

Ally Mpemba "Sasa fanya hivi,wewe nenda kahifadhi vitu vyako halafu uje twende nyumbani mara moja"

Basi niliondoka zangu kurudi gerezani nikachukua meza,kiti pamoja na mwamvuli nikawa nimerudisha mahali ambapo nilikuwa nahifadhia.Baada ya hapo nikawa nimeondoka hadi Aggrey kisha Ally Mpemba akanichukua kuelekea Msimbazi uelekeo wa kituo cha polisi,tulitembea hadi pale Big Bon ambapo nikaona anatoa funguo wa gari kwenye kanzu yake kisha akabonyeza ile gari ikawaka taa na milango ikafunguka,ilikuwa ni ile ile Range ambayo asubuhi niliona dada yake akiwa anashushwa ambayo ilikuwa na Private Number,sasa kwa mara ya kwanza mwanaume kutoka Kijiji cha Mogabiri huko Ukuryani Tarime nikapanda Range,aisee asikwambie mtu na ndiyo maana kuna watu wako tayari kufanya kila aina ya ovu ili kujipatia fedha wanunue magari,ile ilikuwa ni moja ya gari nzuri kuwahi kupanda katika maisha yangu ya umasikini!.

Tuliondoka lile eneo tukaikamata Morogoro Road kisha safari ikaanza kwa spidi ya wastani,baada ya muda tukawa mbele ya nyumba moja maeneo ya magomeni Mikumi,ile nyumba ilikuwa ya kawaida sana kwa muonekano wa nje ila nilipoingia ndani kiukweli ilikuwa nzuri mno na usingedhani kama muonekano wa nje unasadifu kilichomo ndani!.

Baada ya kupiga honi na kufunguliwa geti gari ikawa imeingia pale uani na kupaki,sasa tulipoteremka kuna vitoto vya kike viwili vya kiarabu(Kipemba) tulivikuta hapo ndani vikawa vinamkimbilia Ally na kumrukia kwa furaha!.

Ally Mpemba " Hawa ni watoto wa Farah "

Mimi "Ooh sawa kaka"

Sasa pale nje nilikuta kuna vyombo vingi sana vya kisasa na majiko makubwa ya Gesi na mkaa,na ndivyo vilikuwa vyombo vilivyokuwa vinatumika kwenye shughuli za catering.

Ally Mpemba "Nimekuleta hapa ili ujionee mwenyewe,na ukishajionea najua utaniambia nikulipe kiasi gani master"

Aliendelea "Sasa wewe kazi yako utakuwa unahakikisha vyombo vyote vinaondoka hadi kwenye events na baada ya hapo utakuwa unahakikisha vyombo vyote vinarudi kama vilivyokuwa,baada ya hapo utakuwa unasimamia ishu ya usafi wa vyombo"

Aliendelea "Kikubwa wewe utakuwa msimamizi"

Baada ya yale maelezo angalau sasa ndipo nikaanza kupata uelewa wa kazi nitakayoenda kuifanya.

Ally Mpemba "Na bahati nzuri ni kwamba,events siyo kila siku,kama kutakuwa hakuna events yeyote wewe utakuwa unaendelea na shughuli zako,mimi nahitaji tu msimazi hadi pale atakaporudi mama mdogo au nitakapompata mtu sahihi,ila nakuomba kwa sasa unisaidie kwenye hili"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa"

Ally Mpemba "Ok sasa niambie niwe nakulipaje!"

Mimi "Wewe nilipe utakavyoona kaka"

Ally Mpemba "Wewe niambie kiasi utakachoona kwako kinafaa maana hii siyo shughuli nyepesi kama unavyodhani!"

Mimi "Tufanye hivi kaka,tukianza kazi ndiyo nitajua,nadhani kwasasa tusubiri kwanza "

Ally mpemba "Ok hakuna tatizo maadamu umeamua hivyo!"

Baada ya mazungumzo yale tuliingia kwenye gari tukawa tumeondoka kuelekea Kariakoo,sasa wakati tunarudi tulipitia njia ya Kigogo na tulipofika pale Karume,jamaa alinipatia elfu 20 ya nauli mi nikashuka kwenye gari yeye akawa ameondoka.Nilienda upande wa pili kupanda gari za Gongo la mboto na kuondoka zangu maskani.

Itaendelea.......
Niliwahi kuwa team leader wa kampuni ya Airtel. Unayosimulia yote kuhusu kusajili line, footsoldier, gate meeting pamoja na kamisheni naamin kuwa haya unayosimulia ni kweli na siyo ya kutunga mzee.

Endelea kususha episodes za kutosha.
 
Back
Top Bottom