Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Hivi kuna uwezekano wa kuindoa kura yangu huyu umughaka alikua anaitaji kura tu ameona zimemtosha kashinda ametuzarau wapiga kura wake
 
Ila jamaa alianza vizuri sana lakini naona kwa kadri muda unavyokwenda anaishiwa stori! Ninadhani kwamba alianza na kisa cha kweli ambacho kinagusa sana! Badala ya kuishia kwenye kisa cha kweli akaamua aongezee "ukwaju" ili stori iwe ndefu kidogo!! Matokeo yake anaharibu!!
 
Hivi kuna uwezekano wa kuindoa kura yangu huyu umughaka alikua anaitaji kura tu ameona zimemtosha kashinda ametuzarau wapiga kura wake
Usipanic relax… unavotishia kumnyima KURA je umewaza yeye anavopoteza muda wake na BUNDLE LAKE kutuburudisha sisi BURE ?? Huu ni mkasa wa 3 Umughaka anatuhadithia na zote alimalizia HAKUISHIA NJIANI na zote zinazidiana kwa uhondo. Nae ni Binadam maybe yupo Busy kula Christmas na Family yake au busy na Wateja. TUSIWE WABINAFSI.
 
Kwanza ile tumeingia ndani wakati tumefika,mabegi yakawekwa sebuleni baadae akaitwa mama alivyokuja tukamsalimia,kaka akanitambulisha,nikaulizwa naondoka lini,nikamwambia nitakaa kwa wiki 3

Baada ya siku mbili baba mkubwa akapigiwa simu,huwa anaishi marekani akaanza kunilalamikia kwanini nimeenda pale bila taarifa,eti natakiwa nitoe taarifa maana hapo ni mjini.Yaan familia ya watu walioko vizuri kiuchumi lakini wanaogopa wageni maana mama alikuwa mhasibu BoT

Kaugali wanapika kadogo afu kila mtu anakula kwa muda wake,siku zingine kaka angu anagomba eti tumemwachia ugali mdogo,kuna siku mama alikuta ninakula akaniambia niwe na kataka ugali kidogo ili nimwachie na kaka maana huwa anagomba na wakati huo nimekata kaugali kenye ukubwa wa vipande viwili vya mkate

Muda wote niliokaa pale nikuoga maji ya chumvi wakati maji baridi yapo na nilikuwa nanunua kwa pesa yangu,kuna wakati huyo mama anakuwa na beki 3 nikipita naona kabisa wananisema kwa kilugha na wanacheka,huyo mama alikuwa ni mtu wa tanga
Duu pole sana, hata kama nina roho mbaya lakini si hivyo jamani labda aanze mgeni mwenyewe kinifundisha tabia mbaya [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 05



Jamaa wa duka "Oooh poti mtu mbaya"

Kileri "We mpemba acha zako"

Aliendelea "Jamal yuko wapi?"

Jamaa wa duka "Hapo nje hayupo?,alikuwa anaongea na simu hapo nje"

Kileri "Sijamuona"

Jamaa wa duka "Vipi unataka mzigo?"

Kileri "Ngoja kwanza nichonge na Jamal"


Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Kileri(Mtoto wa baba yangu mkubwa) na Jamaa mmoja mwenye asili ya Pemba tuliyemkuta kwenye duka kubwa la vyombo vya ndani hapo Tandika.Sasa nilibaki kushangaa yale mazungumzo kwasababu Kileri alichokuwa ameniambia ni kwamba tulikuwa tunakwenda kuliona duka letu(Mimi na yeye) ambalo tulikubaliana kufungua.Nialiamua kutulia uenda hapo tulipita kwa rafiki zake ambao alikuwa akifahamiana nao hivyo tungeondoka muda si mrefu kuelekea kwenye duka lenyewe.

Baada ya dakika kadhaa kuna Jamaa mwingine aliingia dukani ambaye pia alikuwa na asili ya pemba na Kileri alipomuona alimuita ili waongee nje lakini jamaa ni kama akawa anamkataa!.


Jamaa "Tatizo lako poti mpaka tuanze kusumbuana kwenye simu,mzigo tunakupa lakini kona nyingi"

Kileri "Jamal eeh hebu njoo tuzungumze kaka"

Jamal " Kama ni hii ishu ya vyombo sitakuelewa lakini kama ni ishu nyingine sawa"

Kileri "We siunanijua lakini mimi ni mtu wa dili!"

Basi yule jamaa aliyeitwa Jamal alitoka nje na Kileri akawa ameniambia nimsubiri abonge kwanza na jamaa.Mimi nilikaa pembeni ambako sikuweza kusikia walichokuwa wanazungumza,baada ya mazungumzo ambayo Kileri alikuwa anamsisitiza sana jamaa,walimaliza ndipo jamaa(Jamal) alikuja akaingia dukani kisha wakawa wanaongea na Kileri kama mwanzo.

Jamal " Sasa nadhani Poti hesabu zetu tutazipiga mwezi ujao ili tujue tunafanyaje katika gawio,au unasemaje?"

Kileri "Mi nakuamini sana Jamal hapo hakuna tatizo"

Aliendelea "Basi sawa mi naondoka"

Baada ya mazungumzo yale mafupi Kileri aliniambia tuondoke zetu,sasa tukiwa njiani Jamaa alikuwa akinieleza mambo mengi ambayo sikuyaelewa na mimi niliamua kunyamaza ili niuone mwisho wake utakavyokuwa kwasababu wahenga wanasemaga "Njia ya muongo ni fupi".
Kileri "Wa kwetu lile duka ndipo nimeweka mtaji wako na wangu,hivyo hao jamaa mara nyingi ndio ninaofanya nao biashara na niwatu wema sana"

Mimi "Kama ndivyo haina shida"

Mimi "Kwahiyo faida tunagawanaje?"

Kileri "Faida tunaigawana kulingana na mtaji,kama ambavyo duka unaliona lilivyokubwa na bado kuna stock nyingine iko stoo,hivyo kila mtu huwa anapata chake kulingana na mtaji"

Aliendelea "Mimi sikutaka kuwaambia ya kwamba nipo na mdogo wangu ila pesa niliyowapa waiweke kwenye mtaji wao wanafahamu kama niya kwangu,hivyo tukigawana faida sisi ndiyo tutakuwa tunagawanya faida yetu tunagawana"

Mimi "Kama ndivyo ni jambo jema"

Kileri "Pia mwanzo nilikuwaga nachukua vyombo kwa mkopo natembeza barabarani na majumbani lakini baada ya kupata mtaji niliona niongee na jamaa wakakubali na ndiyo maana wakati tunaongea nilikushauri uje huku tuifanye hii biashara kwasababu ina faida sana"

Hatimaye tulipanda gari tukawa tumeondoka kurudi nyumbani,muda huo mimi nilikuwa naendelea kushangaa pilika pilika za watu katika jiji la Dar es salaam.

Tulivyofika nyumbani kwa jamaa,yeye alitoka akawa ameelekea kusiko julikana mimi nikabaki pale nyumbani huku nikiendelea kutazama mazingira ya hapo nyumbani,mafundi siku hiyo hawakuja kuendelea na ujenzi lakini walikuwa wamemaliza kiweka vigae vyumba viwili.

Mke wa Kileri "Shem ingia ndani tule"

Mke wa jamaa baada ya kuivisha chakula cha mchana akawa amenikaribisha ndani.

Mke wa Kileri "Baba Nyangi ameenda wapi?"

Mimi "Tumefika wote lakini naona sijui atakuwa ametoka!"

Mke wa Kileri "Hawezi kuona kuna mgeni akatuliza miguu"

Mimi "Ngoja nimpigie simu uenda atakuwa jirani"

Mimi "Ndugu pande zipi?,msosi tayari huku"


Kileri "Nyie kuleni wa kwetu nimetoka kidogo ila sichelewi kurudi"

Mimi "Sawa kaka"

Basi sie tuliendelea kula chakula kama kawaida.Ilipofika usiku mida ya saa 2 jamaa bado alikuwa hajatokea,nakumbuka baada ya kumaliza kula niliingia chumbani kutulia kwasababu ile nyumba hakukuwa na umeme hivyo walikuwa wanatumia taa ya mafuta au siku nyingine mshumaa,sasa sikutaka kukaa sana sebuleni kwasababu hakukuwa na cha maana zaidi ya kushangaa kenchi.

Sasa nikiwa nimepitiwa na usingizi,niliamshwa ghafla na kelele za mtu akiita kwa nguvu.Nilipoangalia saa ilikuwa mida ya saa 5 usiku.Nilipoendelea kusikiliza kwa makini kumbe ilikuwa ni sauti ya Kileri,sasa kumbe jamaa alikuwa amelewa chakari na alikuwa akimuita mkewe amfungulie.

Kileri "Wewe mama Nyangi "

Aliendelea "Mama Nyangi fungua mlango"

Baada ya mkewe kuwa kimya,jamaa alikuwa akifyonza huku akiendelea kugonga geti kwa nguvu,sikufahamu kama mkewe ni kweli alikuwa hasikii au aliamua tu kujikausha.Ilibidi niamke nitoke kwenda kumfungulia jamaa geti kwasababu ilikuwa usiku.

Mimi "Kaka nadhani shemeji atakuwa amepitiwa na usingizi"
Kileri "Wakwetu ngoja niingie kulala tutaonana asubuhi"

Jamaa alikuwa amelewa sana na hata kutembea vizuri akawa anashindwa.Sasa baada ya kuingia chumbani ile nimenilaza kidogo nikaanza kusikia anamfokea mkewe akitishia kumpiga,mkewe nae hakuwa mnyonge kwani alikuwa akimjibu kwa hasira na namna ambavyo nilielewa ni kwamba,jamaa tabia ya ulevi ilikuwa ni kawaida yake na yule mwanamke alionekana kumchoka kwasababu hakuwa na msaada wowote.Baada ya muda ulipita ukimya na nilifahamu jamaa atakuwa alilala fofofo.

Asubuhi nilipoamka sikumuona jamaa na baada ya kumuuliza mkewe akawa ameniambia aliwahi kuamka saa 12 asubuhi akaondoka.Sasa niliamua kuchukua jembe nikaenda kumsaidia mkewe ambaye alikuwa anapalilia bustani aliyokuwa amelima bamia pamoja na matemebele sasa tukiwa pale bustanini,mkewe akawa ananiambia kuhusu tabia za jamaa na aliamua kuniambia nikiwa kama mdogo wake na ndugu yake wa karibu ikiwezekana nimshauri jamaa.

Mke wa Kileri "Shemeji usingeamka ungeacha alale nje,mimi unadhani naamkaga usiku?"

Aliendelea "Tena nadhani alirudi kwa ajili yako,mara zote akijua amelewa huwa harudi kwasababu anajua hata akirudi nani wa kumfungulia geti?,kuna siku amerudi sikumfungulia alilala nje ndipo akaanza tabia akienda huko kulewa harudi hadi kesho yake"

Mimi "Aisee mbona ni hatari"

Mke wa kileri "We acha tu shemeji napitia mambo magumu sana kama mwanamke"

Mimi "Mbona Kileri hakuwaga na hizi tabia?"

Mke wa Kileri "Wewe kileri umeanza kumjua tangu lini unasema hizo tabia alikuwa hana?"

Mimi "Kileri nimekaa sana kwao maana ni kwa baba yangu mkubwa hivyo ninamfahamu vema na hakuwaga na tabia hizi za ulevi"

Mimi "Labda alipokuja Dar ndipo amenza hizi tabia"

Mke wa Kileri "Ndugu yako amenikuta Nauza dagaa kutoka Mwanza na nilikuwa na mtaji mkubwa tu,nilipoingia na Kileri kwenye mahusiano nikajua ni mwanaume nimepata kumbe nilikuwa najidanganya"

Aliendelea "Nilikuwa nampatia hela nikijua mwenzangu anaongezea mtaji kwenye biashara kumbe pesa yote niliyokuwa nikimpatia yeye alikuwa akiipeleka kwa malaya zake"

Mke wa kileri "Nilipokuja kugundua shem nakwambia ilikuwa ugomvi mkubwa sana,baadae aliniomba msamaha ikabidi nimsamehe tuendelee kuishi ila sikumpatia hela yangu tena"

Aliendelea "Hii nyumba unayoiona niliijenga na kuisimamia mimi kwa pesa yangu ya niliyokuwa naipata kwenye biashara ya dagaa,japo kiwanja ni cha kwake lakini naamini nisingejenga angekuwa amekwisha kiuza"

Baada ya maelezo ya mkewe kidogo nikabaki kushangaa kwasababu mimi niliamini ile nyumba itakuwa imejengwa na ndugu yangu kumbe haikuwa kama nilivyodhani,yule mwanamke alikuwa ni mzuri japo ilionekana kabisa maisha mabaya naya umasikini ndiyo yalikuwa yakimchosha.

Mke wa Kileri " Tangia mwezi uliopita naona analeta mafundi wanakarabati humo ndani kwa kuweka vigae na hata kile choo anekijenga upya maana cha kwanza kilikuwa cha mabati"

Aliendelea "Mimi hata simuulizi shem maana niliyofanya yanatosha,na yeye sasa ni zamu yake"

Mimi "Kwani Kaka yeye ukiacha biashara ya vyombo huwa anafanya kazi nyingine"

Mke wa Kileri "Biashara ya vyombo?,ndiyo alikwambia anafanya biashara ya vyombo?"

Mimi "Ndiyo,hivyo ndivyo ninavyofahamu"

Mke wa Kileri "Biashara ya vyombo alikuwa anaifanya hata kabla hatujaishi wote,kupitia biashara hiyo ya vyombo ndipo mimi na yeye tulikutana kwasababu alikuwa anapenda sana kunipitishia vyombo kwenye banda langu"

Aliendelea "Kwa namna alivyokuwa mpole na mnyenyekevu nikajua mwanaume ndiyo huyu"

Mimi "Kwahiyo auzi tena vyombo?"

Mke wa Kileri "Biashara ya vyombo kidogo impeleke jela shem,kuna vyombo sijui alikuwaga anakopa kwa tajiri sasa kumbe alikuwa anauza na hela hapeleki hivyo mwenye vyombo vyake akataka kumfunga ndipo ikabidi nichukue hela yangu nikampatia alipe hela ya watu na wakati huo ndiyo tulikuwa wapenzi"

Baada ya maelezo ya mke wa kileri kiukweli moyo wangu uliuma sana kwasababu niliamini hela yangu jamaa atakuwa ameila!.

Mke wa kileri "Angekuwa anafanya kazi kila siku tushindie matembele?"

Aliendelea "Binti yake tu hata viatu vya shule saa nyingine ni mtihani,hadi niwapigie simu ndugu zangu nianze kuomba omba"

Mimi "Mimi nilijua anafanya biashara ya uuzaji wa vyombo na hata kuja Dar nimekuja kwa shughuli hiyo!"

Mke wa Kileri "Kama alikwambia hivyo alikudanganya"

Mimi "Jana tulienda Tandika kwenye duka moja la vyombo akadai hela niliyompatia ameiweka hapo pamoja naya kwake ili kuongeza mtaji na faida ikipatikana tutakuwa tunagawana na wale jamaa"


Mke wa kileri "Ulimpatia shi ngapi shem?"

Mimi "Nilimpatia milioni 9"

Mme wa kileri "Mungu wangu!,unasemaaa!"


Mme wa Kileri alipata mshangao baada ya kusikia nimempatia mume wake pesa nyingi kiasi hicho!.

Mke wa Kileri "Mbona mimi sijamuona na hela?"

Aliendelea "Hiyo hela shemeji andika maumivu,hiyo atakuwa amepelekewa hawara yake"

Mke wa Kileri " Ndiyo maana naona anajitutumua kuweka vigae ndani nikawa najiuliza huyu katoa wapi hela"

Aliendelea "Mwanaume hana chochote cha maana anachofanya na watu walishamfahamu hawampi hata kazi kwasababu ya ujuaji wa mjini(utapeli)"


Kiukweli niliumia moyo sana na nilimwambia mkewe akae kimya asimwambie chochote lakini mkewe akuvumilia ile hali akaamua siku hiyo hiyo kumtwangia simu,jamaa alipojua mkewe amefahamu hakuwahi tena kurudi nyumbani kwa takribani wiki mbili.

Kwakuwa sikuwa na kazi ilibidi niingie mtaani kuanza kusaka kazi ya kufanya ili kujipatia kipato.


Itaendelea......
Duu pole sana, lakini tukirudi nyuma kabisa UMUGHAKA, hiyo hela chanzo chake ulikopata ni pesa ya ukakasi yawezekana Mungu alitaka uwe msafi [emoji3][emoji3] kwahiyo ilirudi kwao, ila pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mil 2 tu huwezi mpa mtu wa namna hiyo. Jamaa ana fail sana. anaamini anasimulia watu wote wenye akili ndogo. Anatakiwa anapotunga asicheze mbali na uhalisia.....
Nashukuru kwa kuliona Hilo mnk humu kumefurika mazuzu wasio weza kuhoji Wala kuuliza wao Ni kusimuliwa tu Kisha nakunyamaza kwangu mm no umughaka akizingua namcchana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hello


Wakuuu kwema?,mnaendeleaje humu ndani?

Niwatakie wakristo wote wanaosherehekea Christmas HERI YA CHRISTMAS na niwaombe mshehekee kwa kumtukuza Mungu na siyo kuitukuza Anasa na kuipatia dhambi sifa!.

Bado sijapata mualiko ndugu zangu.
Duh ww umejeukia Tena kuwa Tisha watu na maisha Yao walio chagua kuishi ?
Tukisema akili huna watu wako wanatujia juu Sana

Sasa umeandika nn hapo siyo kila kitu unajifanya Bab ushauri kila mtu amechagua maisha yake

Wee shusha story achana na ushauri

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom