Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Hii story imenikumbusha mara ya kwanza mimi kufika dar

kUna kaka angu mtoto wa baba mkubwa aliwah kuja kuishi kwetu kijijin mikoani alikaa muda mrefu sana na pale nyumbani kwetu walimtunza vizuri sana,nakumbuka hadi mama angu alikuwa anamfulia nguo

Sasa kuna kipindi nilkuwa nipo chuo morogoro,nilkuwa nikipata likizo narudi nyumbani kanda ya ziwa,sasa wakati fulani huyo kaka akawa ananipigia simu mara kwa mara na kunisihi siku nyingine nikiwa na likizo niende kwao dar badala ya kwenda huko mbali kanda ya ziwa

nIlipopata likizo nikamtaarifu kuwa siku fulani nitakuja,siku napanda gari nikiwa msamvu nikampigia akaahidi kunipokea,safari ikaanza,nimefika mlandizi napiga simu haipatikani,piga sana haipatikan,bahat nzuri kuna jamaa yangu nilisoma nae o level alikuwa nae yupo dar nae alikuwa ananiomba sana niende dar siku nikipata nafasi,kwahyo kwenda dar nilipata msukumo kutokana na watu wawili

Nilivyokaribia kabisa kufika bila kufanikiwa kumpata huyo kaka angu ikabidi nimpigie dada angu wakati huo alikuwa ni mwanachuo ifm ila akawa anaishi kigamboni,jamaa yangu niliesoma nae olevel yeye kila wakati alikuwa ananipigia simu kuniuliza nimefika wapi,kwahyo dada angu ikabid aje ubungo kunipokea pia jamaa yangu pia alikuwepo,jamaa yangu alikuwa akiishi tabata kimanga na kwa baba mkubwa ni tabata shule,kwavile nilipata mwenyeji wa tabata ikabid dada awahi chuo akaniacha na jamaa yangu ila ikabidi ampigie mama mkubwa kumjulisha ujio wangu pia akamwambia mbona simu ya kaka angu haipatikani,kaka angu kuambiwa ndo akaiweka simu hewani

Tumetoka ubungo tumefika tabata shule tukashuka tukategemea kaka tutamkuta kituoni lakin hatukumkuta ikabid tuanze kumpigia simu ilituchukua kama dk 30 kumsubiri,wakat kutoka kituo cha daladala mpaka nyumban hata sio mbali,basi alivyofika tukaongozana nae mpaka nyumban,yeye mbele mimi na jamaa yangu nyuma na begi letu.

Nilikaa pale kwa baba mkubwa kwa wiki 3 lakin niliona ni kama nimekaa miezi 6
 
Back
Top Bottom