Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Umughaka sio kwamba hana akili ana mapungufu fulani tu kwenye kufanya maamuzi ya haraka, na kila mwanadamu ana mapungufu yakeMkuu UMUGHAKA kama kweli hivi visa unavyovisimulia in vya kweli basi naweza kuitimisha kwa kusema hujui kabisa kuzitumia akili ulizopewa na mwenyezi Mungu
Tukianzia kule kwa Monica ulikopakwa pakwa na kuchanjwa chanjwa na wachawi,tuje kule kwa akina Jipe ulikoamua kuwa jambazi eti kwa sababu rafiki yako Mutatiro alikubali.Tuje hapa kwenye hiki kisa chako cha kumuamini shetani ambako ulikabidhiwa kazi ya kufungua na kufunga chumba usichojua kimehifadhi kitu gani nawe ukakubali tu kama likondoo tena ukaambiwa uwe unalala kwenye gari nje bado hukuinusa hatari
Tuje hapa unaposema ulipelekwa kwa mganga huko Unguja bila kujua unakwenda fanya nini na wewe ukaenda kimya kimya bila hata kumuaga msela wako Steve
Kwa kutumia tu hayo matukio yako machache uliyoyaweka hadharani mpaka sasa naweza kusema ulikuwa na haki zote kupata zero advance na baba yako alikuwa na haki zote kukutimua nyumbani kwake uende ukaibiwe million 9 zako za ujambazi na mlevi Kiheri
Kwa jinsi alivyosimulia story zake zote kwa mtiririko mzuri na details nyingi kiasi hiki, inamuonyesha ni mtu mwenye akili na uwezo mkubwa wa kuweka kumbukumbu
Kitu kimoja nilichokiona kwake kama kasoro ni hana uwezo wa kujiamulia mwenyewe kwa haraka, maamuzi yake mengi ni ya kuchelewa au ya kuamuliwa na marafiki
Ngoja nitoe mifano michache, kule alipoenda kwa shemeji yake anayevua samaki, shemeji yake hakumlipa mshahara kama alivyoahidi kwa miezi kadhaa, lakini akawa anasita kumuuliza na kuondoka pale kwake
Kuna ile ya kupelekwa kwenye danguro alipofika Dar na kuomba kuonyeshwa gesti, alipoona ni Danguro palepale alitakiwa kuondoka na kutafuta gesti mwenyewe lakini akasita pia kuchukua uamuzi
Kuna hii alipoenda kwa mjomba wake na akawa anasaidia kutawaza mgonjwa, hapa alikuwa na haki ya kuondoka sababu ilikuwa inafahamika kwa wenyeji wake kuwa hakuja kukaa kwa muda mrefu na alitakiwa kuondoka baada ya siku chache tu, lakini akawa anasita tena, hadi akalazimishwa kuondoka na ile hostility aliyoonyeshwa na wenyeji wake
Kuna hili la Mpemba kumpeleka huko Chumbe, hapa alikua anajuà kabisa sio sahihi na ni hatari kwake, lakini pia akashindwa kumvaa usoni Mpemba na kuamua kumlatalia pale pale
Kuhusu kumuamini yule jamaa mlevi na kumpa milioni 9, hili hapa linaweza kumkuta yoyote, sababu ndio kwanza alikuwa ametoka kufanya biashara na Mtatiro, ambaye japo hakuwa ndugu yake walifanya kwa uaminifu mkubwa na kugawana faida, sasa saikolojia yake tayari inakuwa inawaza, kama Mtatiro ambaye sio ndugu yangu hajanitapeli, huyu ndugu wa damu moja hawezi kunitapeli, tutafanya vizuri kama Mtatiro (hapo hakuwa anajua kama ndugu ni mlevi)
Ni kasoro ambazo watu wengi tunazo, hata mimi kuna maamuzi mengi ya kipuuzi nafanya kisha najiuliza hivi kwa nini nisngeamua vile? Lakini sio kukosa akili, maana katika watu wenye akili Tanzania, mimi nipo, kwa mujibu wa NECTA
Lakini tupunguze kum judge tufurahie story, maana kila mtu akisimulia maisha yake haya, yatakuwa na blunder nyingi sana