Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 12.




Alinikabidhi rasmi funguo wa ile nyumba pamoja kiasi cha Tsh 140,000/= ikiwa na maana ya kwamba kila siku nitakapokuwa hapo nyumbani kwake,basi itanipasa kutumia elfu 20 kwa ajili ya chakula cha usiku,aliniambia sipaswi kabisa kurudi nyumbani kwa muda huo atakao kuwa ametoka.Kabla hajaondoka alinionyesha gari miongoni mwa magari mawili mapya yaliyokuwa yamepaki pale ndani ya fensi.

Kulikuwa na magari mawili mapya,moja lilikuwa Audi A4 nyeusi isiyokuwa na Number Plate na nyingine ilikuwa ni Mercedes benz C63 nyeupe,hii pia haikuwa na Number Plate,hizi gari zite zilikuwa na mpya kabisa.Jamaa aliniambia mimi ninapaswa kuwa nalala kwenye Audi A4.

Baada ya yale maelekezo huku akionyesha uaminifu mkubwa kwangu Ally Mpemba alisafiri kuelekea huko Unguja kama alivyokuwa ameniambia hapo awali.Baada ya jamaa kuondoka,mimi niliendelea na shughuli zangu za usajili wa line kama kawaida na ilipofika mida ya saa 12 jioni niliondoka zangu kupanda gari kuelekea nyumbani kwa Ally Mpemba.

Nilifanikiwa kufika nyumbani kwa Ally Mpemba kabla ya saa moja,nilisukuma geti nikaingia ndani kisha nikalirudishia,sasa nilisogea moja kwa moja hadi kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ndani,nilifungua ule mlango na kuzama ndani,nilipofika ndani nilianza kuikagua ile nyumba lakini vyumba vyote nilikuta vimefungwa na yawezekana funguo atakuwa alikuwa ameondoka nazo au aliziweka mahali,chumba ambacho nilikuwa na funguo zake ni kile alichonipa kazi ya kukifungua na kukifunga!.Ile nyumba ilikuwa ni kubwa na ilikuwa niya kifahari,ulikuwa ukiingia ndani kulikuwa na nakshinakshi za gharama kubwa(Nadhani nyumba za waarabu au wahindi huwa mnaelewa zinavyokuwaga).

Ile nyumba ulikuwa ukiiangalia kwa nje ilionekana ya kawaida tu ila kwa ndani ilikuwa nzuri sana na usingeamini kama pale anaishi mtu mmoja.

Ilipofika mida ya saa 1 usiku nilienda mpaka kwenye kile chumba nikakifungua na kiukweli sikuweza kuvumilia ilibidi nisogeze shingo karibu na mlango,niliwasha taa kutazama ndani,nilipotazama ndani nilikuta kuna kitanda ambacho kilikuwa kimetandikwa kwa unadhifu wa hali ya juu,pia kulikuwa na makabati ya nguo pamoja na vitu vingine vya kawaida ambavyo huwa vinapatikana vyumbani.Niendelea kutazama kwa makini lakini hakukuwa na mtu wala,sasa niliamua kuondoka mle chumbani na nilikiacha wazi kama alivyokuwa ameniambia Ally.

Niliwasha taa za nje ya ile nyumba kisha nikafunga mlango,niliondoka zangu usiku ule kuelekea kutafuta chakula ili nile nirudi kulala kama kawaida kwenye gari ambalo Ally Mpemba aliniambia ninapaswa kulitumia kama kitanda.Baada ya kupata chakula,niliamua kurudi kwenda kulala ili asubuhi na mapema niamke niende kukifunga kile chumba,kiukweli sikutaka kumuangusha Ally Mpemba na nilitaka aniamini ili kama kuna mambo makubwa zaidi anionyeshe ili na mimi niweze kufanikiwa.

Wakati natoka kupata msosi ilikuwa mida ya saa 3,sasa nikaona niingie kwenye gari niweze kulala,kwakuwa funguo ya gari alikuwa ameniachia,nilipoingia kwenye gari niliwasha AC ili niendelee kupata kiyoyozi huku nikiutafuta usingizi,nilishusha kiti cha dereva kwa kurudi nyuma kisha nikaanza kuusaka usingizi,sasa wakati nikiwa nimepitiwa na usingizi nilishitushwa ghafla na mlio wa vitu vikiwa vinatupwa mle ndani kwenye nyumba ya Ally Mpemba.

Niliamka na taratibu na kutega sikio kwa makini ili nijiridhishe yawezekana nilisikia vibaya,ile sauti iliendelea na ndipo nikatelemka kwenye ile gari nikaelekea mlangoni kutega sikio vizuri,nilipofika pale mlangoni niliendelea kusikia glass,sufuria za kupikia pamoja na vyombo vingine vikitupwa chini kama vile kulikuwa na watu wanapigana,kiukweli niliingiwa na hali ya hofu sana ikabidi nirudi kwenye gari.Nilichukua simu nikawa namtafuta Ally Mpemba lakini simu yake haikupazikana,niliendelea kumtafuta sana lakini simu yake haikupatikana,sasa niliamua nikae kwenye gari nisitoke hadi asubuhi,muda huo ilikuwa yapata saa 7 usiku,sasa ile hali ya kutupa vitu iliendelea hadi ilipotimu mida ya saa 10 usiku,kiukweli sikupata usingizi hata kidogo na nilikuwa najiuliza kulikuwa na kitu gani mle ndani hadi vyombo kupigizwa kiasi kile,japo nilikuwa jasiri katika mambo mengi ambayo niliwahi kuyapitia lakini kwa mara ya kwanza ile hali ilinitisha sana.

Iilipofika mida ya 12 :00 nilienda kufungua ule mlango kwa umakini mkubwa kisha nikaingia ndani,nilipoingia ndani nikawasha taa ili niweze kutazama vizuri kwasababu kulikuwa bado na giza,sasa ile nimewasha taa na kutazama vizuri,nilikuta uaribifu wa kiwango cha juu sana,kiukweli nimepitia mambo mengi ya kutisha na kushangaza lakini lile tukio lilikuwa ni moja ya matukio yaliyonishangaza sana kwa ile siku.

Nilikuta vyombo vimepigizwa chini kila mahali,glass zilikuwa zimevunjwa vunjwa pale sebuleni hadi jikoni kulikuwa hakutamaniki,kiukweli sikuweza kufahamu ni kitu gani kilikuwa kimefanya uaharibifu kiasi kile.Nilisogea hadi kwenye kile chumba na safari hii sikutaka kabisa kichungulia ndani ilibidi nikifinge haraka.

Baada ya kufunga kile chumba nilitoka nje nikafunga mlango kisha nikarudi kwenye gari kwanza kutulia,kiukweli nilikuwa nina maswali mengi sana ambayo nilikuwa najiuliza lakini sikuwa na majibu.Nilikaa kwenye ile gari hadi mida ya saa 2 asubuhi ndipo nikatoka nikaelekea kwenye bomba kunawa uso na kusukutua maji mdomoni na baada ya hapo nikafunga geti nikaondoka zangu kuelekea ofisini Buguruni kwenye kikao.Kikao kilivyoisha nikaondoka kuelekea Kkoo kazini kama kawaida.

Kwa muda huo yule dada yake na Ally Mpemba aliyekuwa akiitwa Farah hakuwahi kujua kabisa kwa wakati huo kama mimi na Ally tulikuwa tumeshibana kiasi kwamba mpaka Ally kuniachia funguo za nyumba yake,sasa wakati Ally ameondoka,ile Range ilikuwa imepaki nyumbani kwake.

Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi simu yangu ikawa inaita na nilipoitazama alikuwa ni Ally akinipigia,niliipokea ile simu kisha akawa ananiuliza maendeleo tangu alipoondoka.

Ally Mpemba "Unaendelea vema lakini wewe?"

Mimi "Kaka naendelea vema lakini jana kuna jambo limetokea pale kwako!"

Ally Mpemba "Usiniambie umefanya ambacho sikukuelekeza"

Mimi "Hapana kaka siyo hivyo"

Ally Mpemba "Mmmh ni nin!,ama umeshindwa nilichokwambia?"


Mimi "Kaka jana wakati nimelala kwenye gari nilikuwa nasikia vitu vinatupwa chini na glass kuvunjwa,nilipoingia ndani asubuhi wakati naenda kufunga mlango nikakuta vyombo vimetapakaa sebuleni hadi Jikoni kaka"

Ally Mpemba "Mtumeeeee!"

Aliendelea "Hiyo TV haijavunjwa kweli?"

Mimi "Hapana kaka,samani za ndani ziko vizuri,vyombo vyote ndo vimetapakaa ndani?"

Ally Mpemba "Umefunga mlango?"

Mimi "Ndiyo kaka nimefunga kama ulivyoniambia"

Ally Mpemba "Vyombo je umevipanga?"

Mimi "Hapana kaka sijagusa kitu maana hukunipa maelekezo mengine zaidi ya yale ya juzi"

Ally Mpemba "Bado uko hapo nyumbani?"

Mimi "Hapana kaka mimi nipo Kkoo"

Ally Mpemba "Ok nakuomba niuazime muda wako master na nitakufidia nikirudi,nakuomba uende sokoni ukanunue kabeji kubwa tano,nunua na mboga za majani kisha nenda nyumbani uingie jikoni ufungue kabati lililoko karibu na friji kwa chini utakuta kitambaa cheupe,hicho kitambaa katandike pale sebuleni juu la ile meza ya kioo na kisha weka hayo mahitaji utakayokuwa umenunua!"

Mimi "Sawa kaka hakuna tatizo"

Ally Mpemba "Nilisahau kukwambia nilivyoondoka,nisamehe sana kaka"

Mimi "Usijali kaka,hizo mboga za majani ni aina gani?"

Ally Mpemba "Nunua zozote kaka ila ziwe za kutosha"

Mimi "Sawa kaka usijali"

Ally Mpemba "Farah hajakuuliza kitu kuhusu mimi?"

Mimi "Hapana kaka,kwanza huwa sinaga stori na mtu kaka mwenyewe unanijua"

Ally Mpemba "Nitakulipa mambo makubwa master kwani wewe ni muaminifu sana,nashukuru sana kwa kuwa muaminifu kwangu?"

Mimi "Usijali kaka!"

Ally Mpemba "Ngoja nimpigie simu Farah kuna hela nimwambie akupe halafu mimi nitamrudishia"

Mimi "Sawa"

Niliamua kufunga na kurudisha meza kule ambapo mara zote nimekuwa nikihifahdi ninapomaliza kazi,sasa nikiwa njiani napeleka kuhifadhi vifaa vyangu vya kazi,Ally Mpemba alinipigia simu.

Ally Mpemba "Nimemwambia Farah akupe elfu 50,itumie hiyo kununua mahitaji hayo niliyokwambia"

Mimi "Sawa kaka Usijali"

Nilirudi hadi kwa Aunt Farah kuchukua kile kiasi cha fedha kisha nikaondoka kuelekea kununua yale mahitaji aliyokuwa ameniambia Ally Mpemba,baada ya kununua mahitaji yote muhimu kama alivyokuwa amenielekeza,nilipanda gari kuelekea Magomeni ambako ndiko alikokuwa akiishi Ally Mpemba,nilipofika nilianza kukusanya vyombo vyote vilivyokuwa chini na vile ambavyo vilikuwa vimepasuka niliamua kuvikusanya na kuviweka kwenye dust bin kule jikoni.

Baada ya kumaliza lile zoezi la kusafisha mle ndani,niliingia jikoni nikafungua ile kabati aliyokuwa amenielekeza jamaa kisha nikatoa kitamabaa cheupe nikaenda kukitandika kwenye ile meza kama alivyokuwa amenielekeza,nilipomaliza kukitandika kile kitambaa nilichukua zile kabeji kubwa 5 pamoja na yale mafungu ya mboga za majani nakiyaweka pale mezani,mboga za majani nilinunua za kutosha na nilinunua na aina karibia zote kasoro matembele!.

Baada ya kumaliza lile zoezi kwa kuwa ilikuwa mapema,niliondoka kuelekea Gongo la Mboto kuoga na kubadili nguo,nilipofika niliamua kulala kabisa kwasababu nilikuwa nina usingizi wa kufa mtu.
Ilipofika mida ya saa 11 jioni niliamua kuondoka kutembea mdogo mdogo hadi stendi ya Gongo la Mboto kisha nikapanda gari za Masaki ili nikashukie Magomeni kisha nielekea kwa Ally Mpemba.

Nilipofika nilifungua mlango nikaingia hadi ndani,sasa kwakuwa muda wa kufungua ule mlango ulikuwa bado kidogo,niliona niwashe Luninga ili niendelee kupoteza muda,sasa wakati nikiwa natazama luninga,kule kwenye kile chumba nikawa nasikia sauti yenye mtetemo.


Itaendelea........

Muendelezo soma Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
Licha ya matukio hayo yote bado unakaa kwa sebule duu !
 
Kwenye story zake kuhusu stive sijui ni mimi lakini ukweli sikuona popote ambapo stive alikuwa ni rafiki sana mpaka kumshirikisha mambo yake binafsi...zaidi stive ndo alikuwa anaomba ushauri kwa huyu.

Huku mtaani ninako ishi wapo walokuwa wakifanya vizuri darasani lakini kimtaani, mtaa unawachakaza na kinyume chake..... Maisha hayana formula.
point sana..
 
Hili likurya lijinga sana halina akili hata kidogo litakuja kufa kifo cha kijinga sana,baba yake aliona mbali sana kulitimua nyumbani lingemuharibia watoto wake na hizo akili zake za kuuza pesa feki & kupiga debe sirari.Bangi zimeliharibu sana ubongo na humo kwenye uboda boda litakachotoamo ni ulemavu wa mwili maana akili tayari halina
Duh mbona makasiriko.. Enhe tuambie unaumia ukiwa wapi
 
Wanaodanganywa ni sisi na tunatega masikio, sasa wewe inakuhusu nini? Ndiyo swali langu,

Hili likurya lijinga sana halina akili hata kidogo litakuja kufa kifo cha kijinga sana,baba yake aliona mbali sana kulitimua nyumbani lingemuharibia watoto wake na hizo akili zake za kuuza pesa feki & kupiga debe sirari.Bangi zimeliharibu sana ubongo na humo kwenye uboda boda litakachotoamo ni ulemavu wa mwili maana akili tayari halina
ukiona mtu anamakariko ya hivi,jua hii story imemgusa,na anafanya haya mambo,sasa umughaka katoboa siri ya kilinge...
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 16.



Ukiachilia mbali kile kivuko cha Kigongo - Busisi pamoja na kupanda ile mitumbwi ya shemeji yangu(masamaki) kule kisiwani Ijinga sikuwahi kabisa kupanda Boti ya kisasa,hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya Kwanza kupanda ile boti nzuri naya kisasa.

Sababu za mimi na Ally Mpemba kwenda Chumbe zilikuwa mbili,moja;Ni kwamba baada ya mimi kumshuhudia yule kiumbe wa ajabu mle ndani,Ally Mpemba kuna miiko aliivunja kutokana na maelekezo ya mtaalamu wake,hivyo tulienda ili akaone namna ya kurekebisha kabla mambo hayajaharibika,pili; ilikuwa ni mimi kuzitaka mali baada ya ushawishi wa Ally Mpemba,sasa ilifika hatua na mimi nikashawishika na kuona ile kazi yangu ya usajili wa line ilikuwa ikinipotezea muda tu.

Baada ya kufika Unguja hatukutaka kupoteza muda,Ally Mpemba aliniongoza hadj kwa huyo mtaalamu aliyekuwa akimfahamu hapo Chumbe,mawazo yangu nilidhani uenda huyo jamaa angekuwa na makolo kolo kama ambavyo nilizoea kuwaona wataalamu wengi wa mikoani namna wanavyokuwa,ila yeye alikuwa kawaida tu!.Baada ya kufika kwa huyo mtu hatukumkuta na tulimkuta mwanamke aliyekuwa amevaa hijab akamwambia Ally Mpemba kwamba ameenda kuswali na tulichofanya tuliamua kumsubiri pale kwake.

Aliporejea kutoka kuswali alitukuta tukiwa tumekaa kwenye mkeka tukimsubiri,baada ya kumuona Ally Mpemba walisalimiana na mimi pia nikamsalimu.Alimuita Ally Mpemba akamwambia aingie ndani,baada ya mazungumzo ya takribani nusu saa,Ally Mpemba alirudi nje akiwa amebeba Vitu ambavyo sikuvielewa na akanitaka tuongozane nae.Nilimfuata nyuma Ally Mpemba hadi tukaifikia miti pori iliyokuwa kando ya Bahari.Nyuma yetu pia alikuwa akija yule mzee aliyekuwa amevaa kanzu huku mkononi akiwa amebeba Mkeka na vitu vingine,baada ya kufika eneo ambalo yeye aliona ndipo panafaa,alituambia tuvue nguo.

Mzee "Vua nguo zenu"

Mimi na Ally Mpemba tulivua nguo tukabaki kama tulilivyozaliwa,baada ya hapo alinikabidhi kichupa kidogo ambacho kilikuwa cha Gliselin,sasa kile kichupa ndani yake hakukuwa na Gliselin bali kilikuwa na kitu kama damu,baada ya kukipokea akanikabidhi na bangiri la chuma(Hili huwa wanapenda kulivaa watu mbalimbali mikononi).Sasa baada ya kukabidhiwa hivyo vitu alitutaka tukae chini kwenye ule mkeka,alitoa kopo kama chetezo kisha akaweka vitu kama tumbaku iliyokauka,baada ya kuona imeenea kwenye kile chombo akatoa kiberiti akawasha,baada ya kuwasha akaanza kuongea kwa kiarabu huku akiwa anatikisa mgongo kwa kwenda mbele na kurudi nyuma.Baada ya kuwasha kile chombo kulikuwa na harufu nzuri sana kama udi lakini yenyewe ilikuwa nzuri zaidi ya udi.


Alipomaliza kusoma kisomo aliniambia nisimame.

Mzee "Waiyona ile bahari?"

Mimi "Ndiyo naiona"

Mzee "Weye nenda pale,ukifika pale chukua hicho kikopo mwaga Baharini ukimaliza chota maji na hicho kikopo uyalete hapa"

Kweli niliondoka zangu kushuka baharini huku nikiwa mtupu kama nilivyozaliwa,yale maeneo hakukuwa na watu kabisa na kulikuwa na miti ambayo isingekuwa rahisi watu kuona mnafanya kitu gani,sikufahamu kama mara zote Ally Mpemba alikuwa akija Unguja analetwa hilo eneo au siku hiyo tulipelekwa tu kwa kazi maalumu.

Nilipofika lile eneo la wazi la bahari nilifanya kama mzee alivyoniambia kisha nikageuza kurudi,nilipofika nilikuta Ally Mpemba akiwa amelazwa kwenye ule mkeka akiwa anapakwa mafuta ambayo sikuyafahamu mgongoni hadi miguuni,sasa alipomaliza ile shughuli kwa Ally Mpemba akaniambia nikae chini kwenye ule mkeka.

Mzee "Sogea kaa hapa"

Baada ya kukaa kwenye ule mkeka akachukua kale kakopo ka Gliselin nilikokuwa nimeweka maji ya bahari akamimina yale maji kwenye chombo kidogo cha udongo kilichokuwa kama chungu lakini kilikuwa kidogo kisha akaanza kuchanganya kwa ndani na mikono,baada ya kumaliza akaanza visomo kwa lugha ya kiarabu,sikuelewa alichokuwa anamaanisha ni kitu gani,sasa baada ya kumaliza akachukua lile bangiri ambalo alikuwa amenipatia mwanzo kisha akalichovya kwenye ule mchaganyiko na kunitaka nivae.

Sasa baada ya kuvaa lile bangiri nikasikia limenibana mkono mithiri ya mtu kama kafungwa na waya mikononi,cha ajabu nikaanza kuona damu zinatiririka mkononi,damu zilipoanza kutitirika mkononi akachukua kile chombo kilichokuwa kama chungu akawa anazikinga matone yale yaliyokuwa yakidondoka.

Mzee "Unahisi maumivu?"

Mimi "Hapana"

Mzee "Ukihisi maumivu niambie"

Ile damu iliendelea kutoka kwa mfululizo pasipo kukoma ndipo nikaanza kuhisi maumivu mkononi nikamwambia yule mzee!.Baada tu ya kumwambia nahisi maumivu,alinishika akaanza kuongea maneno yaleyale kisha ile bangiri ikalegea na damu zikakoma kutoka.Alichukua kile chombo kilichokuwa kama chungu akakisogeza pembeni kisha akaniambia mimi na Ally tukae chini.


Mzee "Alfwat amekubali toba ya ndugu yako"

Aliendelea "Hakikisha hii hali haijirudii tena na nitamfungamanisha na Alfwat kama ulivyonieleza na atamsaidia kama anavyokusaidia wewe"

Basi baada ya maelezo hayo mafupi,alichukua ile bangiri ikiyokuwa imechovya kwenye damu pamoja na mchanganyiko wa dawa kisha akanitaka niivae.

Mzee "Hakikisha hii hauivui mkononi na kama ukipata tatizo inapaswa Ally Mpemba akulete kwangu!"

Mzee "Alfwat amekupenda na nilimueleza hilo suala ndugu yako hapa,unachopaswa kufanya ni kumtunza"

Aliendelea "Kwa ulichokifanya kama asingekuwa amekupenda kitendo cha kumvaa mkononi angekumaliza"

Aliendelea "Jambo la kwanza,inapaswa umvae huyu Alfwat na popote uendapo hakikisha unakuwa nae usimuache na kama nilivyokwambia kukiwa na tatizo utamwambia huyu bwana akulete,usithubutu kukanyaga huku ukiwa mwenyewe"

Mzee "Jambo la pili,hakikisha kila itakapokuwa inafika ijumaa ya mwisho wa mwezi,utachukua wembe na utajichanja chini ya mkono huu wa kushoto ambao ambao unavaa hii bangiri,baada ya kuchanja Alfwat atakuja na utamlisha,akishiba atakuacha na ndipo mambo yako yatashamiri "

Mimi "Nikioga nayo haina tatizo?"

Mzee "Hiyo haina tatizo wala usijali kuhusu kuoga na usije ukajaribu kuivua!"

Mimi " Sawa na nitajuaje Alfwat ameshiba?"

Mzee " Ukiona bangiri inakubana na ukahisi maumivu utashika bangiri na utaipaka mchanganyiko wa damu yako hii ambayo nimekuwekea kwenye kikopo kisha Alfwat atakuachia"

Mimi "Sawa nimekuelewa"

Baada ya maelezo hayo ya kina alituambia tunyanyuke na tukusanye kila kitu na kuondoka kurejea kwake,baada ya kufika kwake hatukukaa sana na tuliondoka kuelekea Unguja ambapo tulifikia kwa bwana mmoja aliyekuwa na asili ya kipemba na nilitambulishwa na Ally kama ndugu yake,tulilala pale kisha kesho yake tukaondoka kurejea Dar es salaam.

Muda huo nilikuwa nimevaa ile bangiri mkononi na kisha Ally Mpemba akawa ameweka vitu kadhaa ambavyo tulitoka navyo kwa huyo mzee aliyemfahamu yeye.

Baada ya kufika Dar es salaam nilielekea nyumbani nikaachana na Ally Mpemba pale bandarini,baada ya kufika nyumbani nilichukua kile kichupa kidogo nikakitunza ndani.Niliendelea kupambana kibishi na ile kazi yangu ya usajili wa line huku mkononi nikiwa nimevaa bangiri kama urembo kumbe haikuwa hivyo!.

Sasa ilipofika ijumaa ya mwisho wa mwezi Ally Mpemba alinitaka niende nyumbani kwake.


Itaendelea............
Lovelovie
 
Back
Top Bottom