Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

And you think that you are already educated? Kiswahili tumekufundisha na bado hata unaandika unakosea. Acha kiingereza its not your mother tongue i cant blame you for that. Hii dunia tenda wema wende. Unajiona tayari nawe ni super star? Umetukuta lakini.
Sasa mother tongue na kuandika vinahusianaje?
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 16.



Ukiachilia mbali kile kivuko cha Kigongo - Busisi pamoja na kupanda ile mitumbwi ya shemeji yangu(masamaki) kule kisiwani Ijinga sikuwahi kabisa kupanda Boti ya kisasa,hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya Kwanza kupanda ile boti nzuri naya kisasa.

Sababu za mimi na Ally Mpemba kwenda Chumbe zilikuwa mbili,moja;Ni kwamba baada ya mimi kumshuhudia yule kiumbe wa ajabu mle ndani,Ally Mpemba kuna miiko aliivunja kutokana na maelekezo ya mtaalamu wake,hivyo tulienda ili akaone namna ya kurekebisha kabla mambo hayajaharibika,pili; ilikuwa ni mimi kuzitaka mali baada ya ushawishi wa Ally Mpemba,sasa ilifika hatua na mimi nikashawishika na kuona ile kazi yangu ya usajili wa line ilikuwa ikinipotezea muda tu.

Baada ya kufika Unguja hatukutaka kupoteza muda,Ally Mpemba aliniongoza hadj kwa huyo mtaalamu aliyekuwa akimfahamu hapo Chumbe,mawazo yangu nilidhani uenda huyo jamaa angekuwa na makolo kolo kama ambavyo nilizoea kuwaona wataalamu wengi wa mikoani namna wanavyokuwa,ila yeye alikuwa kawaida tu!.Baada ya kufika kwa huyo mtu hatukumkuta na tulimkuta mwanamke aliyekuwa amevaa hijab akamwambia Ally Mpemba kwamba ameenda kuswali na tulichofanya tuliamua kumsubiri pale kwake.

Aliporejea kutoka kuswali alitukuta tukiwa tumekaa kwenye mkeka tukimsubiri,baada ya kumuona Ally Mpemba walisalimiana na mimi pia nikamsalimu.Alimuita Ally Mpemba akamwambia aingie ndani,baada ya mazungumzo ya takribani nusu saa,Ally Mpemba alirudi nje akiwa amebeba Vitu ambavyo sikuvielewa na akanitaka tuongozane nae.Nilimfuata nyuma Ally Mpemba hadi tukaifikia miti pori iliyokuwa kando ya Bahari.Nyuma yetu pia alikuwa akija yule mzee aliyekuwa amevaa kanzu huku mkononi akiwa amebeba Mkeka na vitu vingine,baada ya kufika eneo ambalo yeye aliona ndipo panafaa,alituambia tuvue nguo.

Mzee "Vua nguo zenu"

Mimi na Ally Mpemba tulivua nguo tukabaki kama tulilivyozaliwa,baada ya hapo alinikabidhi kichupa kidogo ambacho kilikuwa cha Gliselin,sasa kile kichupa ndani yake hakukuwa na Gliselin bali kilikuwa na kitu kama damu,baada ya kukipokea akanikabidhi na bangiri la chuma(Hili huwa wanapenda kulivaa watu mbalimbali mikononi).Sasa baada ya kukabidhiwa hivyo vitu alitutaka tukae chini kwenye ule mkeka,alitoa kopo kama chetezo kisha akaweka vitu kama tumbaku iliyokauka,baada ya kuona imeenea kwenye kile chombo akatoa kiberiti akawasha,baada ya kuwasha akaanza kuongea kwa kiarabu huku akiwa anatikisa mgongo kwa kwenda mbele na kurudi nyuma.Baada ya kuwasha kile chombo kulikuwa na harufu nzuri sana kama udi lakini yenyewe ilikuwa nzuri zaidi ya udi.


Alipomaliza kusoma kisomo aliniambia nisimame.

Mzee "Waiyona ile bahari?"

Mimi "Ndiyo naiona"

Mzee "Weye nenda pale,ukifika pale chukua hicho kikopo mwaga Baharini ukimaliza chota maji na hicho kikopo uyalete hapa"

Kweli niliondoka zangu kushuka baharini huku nikiwa mtupu kama nilivyozaliwa,yale maeneo hakukuwa na watu kabisa na kulikuwa na miti ambayo isingekuwa rahisi watu kuona mnafanya kitu gani,sikufahamu kama mara zote Ally Mpemba alikuwa akija Unguja analetwa hilo eneo au siku hiyo tulipelekwa tu kwa kazi maalumu.

Nilipofika lile eneo la wazi la bahari nilifanya kama mzee alivyoniambia kisha nikageuza kurudi,nilipofika nilikuta Ally Mpemba akiwa amelazwa kwenye ule mkeka akiwa anapakwa mafuta ambayo sikuyafahamu mgongoni hadi miguuni,sasa alipomaliza ile shughuli kwa Ally Mpemba akaniambia nikae chini kwenye ule mkeka.

Mzee "Sogea kaa hapa"

Baada ya kukaa kwenye ule mkeka akachukua kale kakopo ka Gliselin nilikokuwa nimeweka maji ya bahari akamimina yale maji kwenye chombo kidogo cha udongo kilichokuwa kama chungu lakini kilikuwa kidogo kisha akaanza kuchanganya kwa ndani na mikono,baada ya kumaliza akaanza visomo kwa lugha ya kiarabu,sikuelewa alichokuwa anamaanisha ni kitu gani,sasa baada ya kumaliza akachukua lile bangiri ambalo alikuwa amenipatia mwanzo kisha akalichovya kwenye ule mchaganyiko na kunitaka nivae.

Sasa baada ya kuvaa lile bangiri nikasikia limenibana mkono mithiri ya mtu kama kafungwa na waya mikononi,cha ajabu nikaanza kuona damu zinatiririka mkononi,damu zilipoanza kutitirika mkononi akachukua kile chombo kilichokuwa kama chungu akawa anazikinga matone yale yaliyokuwa yakidondoka.

Mzee "Unahisi maumivu?"

Mimi "Hapana"

Mzee "Ukihisi maumivu niambie"

Ile damu iliendelea kutoka kwa mfululizo pasipo kukoma ndipo nikaanza kuhisi maumivu mkononi nikamwambia yule mzee!.Baada tu ya kumwambia nahisi maumivu,alinishika akaanza kuongea maneno yaleyale kisha ile bangiri ikalegea na damu zikakoma kutoka.Alichukua kile chombo kilichokuwa kama chungu akakisogeza pembeni kisha akaniambia mimi na Ally tukae chini.


Mzee "Alfwat amekubali toba ya ndugu yako"

Aliendelea "Hakikisha hii hali haijirudii tena na nitamfungamanisha na Alfwat kama ulivyonieleza na atamsaidia kama anavyokusaidia wewe"

Basi baada ya maelezo hayo mafupi,alichukua ile bangiri ikiyokuwa imechovya kwenye damu pamoja na mchanganyiko wa dawa kisha akanitaka niivae.

Mzee "Hakikisha hii hauivui mkononi na kama ukipata tatizo inapaswa Ally Mpemba akulete kwangu!"

Mzee "Alfwat amekupenda na nilimueleza hilo suala ndugu yako hapa,unachopaswa kufanya ni kumtunza"

Aliendelea "Kwa ulichokifanya kama asingekuwa amekupenda kitendo cha kumvaa mkononi angekumaliza"

Aliendelea "Jambo la kwanza,inapaswa umvae huyu Alfwat na popote uendapo hakikisha unakuwa nae usimuache na kama nilivyokwambia kukiwa na tatizo utamwambia huyu bwana akulete,usithubutu kukanyaga huku ukiwa mwenyewe"

Mzee "Jambo la pili,hakikisha kila itakapokuwa inafika ijumaa ya mwisho wa mwezi,utachukua wembe na utajichanja chini ya mkono huu wa kushoto ambao ambao unavaa hii bangiri,baada ya kuchanja Alfwat atakuja na utamlisha,akishiba atakuacha na ndipo mambo yako yatashamiri "

Mimi "Nikioga nayo haina tatizo?"

Mzee "Hiyo haina tatizo wala usijali kuhusu kuoga na usije ukajaribu kuivua!"

Mimi " Sawa na nitajuaje Alfwat ameshiba?"

Mzee " Ukiona bangiri inakubana na ukahisi maumivu utashika bangiri na utaipaka mchanganyiko wa damu yako hii ambayo nimekuwekea kwenye kikopo kisha Alfwat atakuachia"

Mimi "Sawa nimekuelewa"

Baada ya maelezo hayo ya kina alituambia tunyanyuke na tukusanye kila kitu na kuondoka kurejea kwake,baada ya kufika kwake hatukukaa sana na tuliondoka kuelekea Unguja ambapo tulifikia kwa bwana mmoja aliyekuwa na asili ya kipemba na nilitambulishwa na Ally kama ndugu yake,tulilala pale kisha kesho yake tukaondoka kurejea Dar es salaam.

Muda huo nilikuwa nimevaa ile bangiri mkononi na kisha Ally Mpemba akawa ameweka vitu kadhaa ambavyo tulitoka navyo kwa huyo mzee aliyemfahamu yeye.

Baada ya kufika Dar es salaam nilielekea nyumbani nikaachana na Ally Mpemba pale bandarini,baada ya kufika nyumbani nilichukua kile kichupa kidogo nikakitunza ndani.Niliendelea kupambana kibishi na ile kazi yangu ya usajili wa line huku mkononi nikiwa nimevaa bangiri kama urembo kumbe haikuwa hivyo!.

Sasa ilipofika ijumaa ya mwisho wa mwezi Ally Mpemba alinitaka niende nyumbani kwake.


Itaendelea............
Lucha ukuje useme kama ungeweza kuvua nguo zote😂😂😂😂😂
 
Ha ha ha... Mimi kiuchumi sina tatizo nasikitika tu jamaa kaingizwa mjini ameshazoea sasa....haya yote heri lakini....🤣
You played your part (if any at all) maana hata sisi tulitambulishwa duniani tukasomeshwa na wazazi halafu tukifanikiwa tunawaacha vijijini bila msaada, sembuse we kumtambulisha mtu aliyeshika 🔫 ambayo we unaiona ikiwa imebebwa na askari? Kuna tajiri wa mabasi ya Sauli Dar hana makazi kabisa ye ni chunya na mbeya tu. Kutangulia mjini sio kufanikiwa jombaa
 
Ameshaniita mimi sina akili siwezi bishana naye tena. Huyu kijana nimehusika sana katika ukaaji wake hapa Dar. Ila basi kama leo hii mimi punguani. Namshukuru.
Kwenda huko Acha kujipa umuhimu kwenye Maisha ya watu, ungekuwa umeshiriki kivyovyote vile katika Maisha ya jamaa basi usingekuwa na chuki za wazi namna hii Kwa jamaa

Ungekuwa unajuana na mshkaji naimani tofauti zenu mngezimalizia huko huko mlikofamiana na sio nyuma ya keyboard

Unaonekana una wivu sana juu ya Mwamba,We pia ulikuwa na vistory vyako uchwara na watu tukasoma ila hukubahatika kutrend kama mshkaji na maisha ndio yapo hivo

Ata kama mnafanya kazi moja hamuwezi kuwa sawa, kila mmoja atabaki na upekee wake, kwahiyo badala ya kujenga chuki hebu angalia positivity za mshkaji ujifunze vitu ambavyo vitakusaidia katika uandishi wako nawewe

Umekazana na kumshtumu jamaa juu ya story zake kuwa ni za kutunga Tunga, sasa ili ujue kama kutunga story ni ngumu sana hebu kaendeleze story zako za kukopi na kupest huko ulipoziachia

Kwa sasa we kubali tu ata kimoyo moyo kuwa jamaa ni wamoto, sasa nawewe ingia chimbo ulete story wasomaji sie tupo tu ata ulete story ya vibata vidogo vidogo vinaogelea tutasoma tu
 
Ungenifundisha bila shaka ningekuwa na utindio wa Ubongo zaidi yako.

Ulianzisha uzi wako kule kwa kunitaja ila shukuru kwa bahati nzuri huwa sijibu watu wasio kuwa na akili timamu,nakujibu hapa kwasababu umekuwa ukijipendekeza kwangu sijui unachotaka ni kitu gani,kwanini usipambane na nyuzi zako?
Daah mkuu kinaniuma unavyo poteza Energy yako kwa watu mapochopocho kama huyo Chizi ambaye sijui maarifa kayatoa wapi...[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
Watu wanahoji walipokuwa unguja nani alikuwa anafungua mlango ili kuhalalisha story kuwa ya hovyo na kuwa hakuna mwingine zaidi ya master anaweza kufanya hiyo kazi lkn hawahoji kabla ya master nani alishika hiyo kazi au baada ya master kuondoka nani atafanya hiyo kazi.
Mim ndo niliifunga na kufungua.
Na mim nilikua nalala hapo hapo ndani na maya
 
Back
Top Bottom