Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 23.



Sikutaka kabisa kupoteza muda,baada ya kufanikisha lile zoezi la ununuzi wa chupi nilimtafuta Rehema nikajaribu kuongea nae na kumshawishi kuhusu ile zawadi.

Rehema "baby sasa size yangu umeipatia kweli?"

Mimi "Nimejitahidi baby wala usijali!"

Rehema "Zikinibana utazirudisha?"

Mimi "Nitakununulia nyingine!"

Rehema "Mmh haya bwana!"

Aliendelea "Uko wapi?"

Mimi "Natoka mjini naelekea nyumbani"

Rehema "Umefika wapi?"

Mimi "Bado nipo mjini"

Rehema "Pita basi Sokoni unisubiri nikusanye madeni yangu halafu tuondoke wote nyumbani!"

Mimi "Ila sina gari nimeipeleka gereji!"

Rehema "wewe pita bana kwani mpaka uwe na gari?"

Mimi "sawa nakuja mama"


Niliondoka kupanda gari nikashukia pale Ilala sokoni ambapo nilimpigia simu Ray akawa ameniambia nimsuburi mahali kwanza achukue hela zake,sasa baada ya kumalizana na watu wake alikuja akiwa amevaa mini sketi na tisheti nyupe iliyompendeza kupita kiasi,jioni ile sasa ndipo niliuona uzuri na umbo la Rehema kwa umakini na kiukweli alizidi kuichanganya akili yangu,kiukweli ni mwanamke ambaye Mungu alimjaalia umbo zuri sana,ingawa alikuwa na sura ya kawaida na alikuwa ni mwanamke fulani asiyekuwa na makuu,ulikuwa ukimuangalia kichwani alipenda sana kusuka Yeboyebo,pamoja na shepu yake kunichanganya lakini nilijikuta tu kadiri siku zilivyokuwa zikisonga ndipo nilimpenda kuzidi.

Mimi "Umependeza!"

Rehema "Sasa nimependeza na nini!"

Mimi "Kwahiyo wewe hujioni?"

Rehema "mmh aya bwana"

Aliendelea "Nipe basi hela ninunue mahitaji twende tukapike!"


Nilichukua elfu 20 nikampatia akawa ameniachia mkoba wake nimshukie na yeye aliondoka kuelekea tena sokoni kwa ajili ya kununua mahitaji.Baada ya kukamilisha alirejea tena akiwa amefungasha mazaga ya kutosha kwenye mifuko.

Mimi "Madumu ya juisi umeyaweka wapi?"

Rehema "Leo namshukuru Mungu nimemaliza mapema,nilirudi tu kuchukua hela maana watu wateja wangu wengi huwa wananilipa jioni hivyo huwa narudi kwanza nyumbani"

Mimi "sawa"

Tulipanda gari kuelekea Gongo la mboto na tulipofika tu nyumbani Rehema hakutaka mambo yawe mengi,aliniambia nimpatie chupi zake nilizokuwa nimenunulia kama zawadi azijaribu,alichukua lile begi langu ambalo ndani niliiweka ile dawa pamoja na zile chupi akawa amefungua zipu na kutoa zile chupi akaanza kujaribu moja baada ya nyingine,chupi zote zilimtosha kana kwamba alikuwa ametengenezewa yeye!,alifurahi sana.

Rehema "Kweli unanipenda nimeamini!"

Mimi "Kwanini?"

Rehema "Kama nimekuvulia chupi mara moja na umekiona kiuno changu na hujakosea basi wewe ndiye mume wangu naamini!"

Kauli ile ya Rehema ilizidi kunichanganya sana kiakili.Nilipaswa zile chupi nizitie dawa kabla ya kuzivaa ili akishaivaa ile nyekundu kazi ianze mara moja lakini nilijikuta ndiyo upendo unakolea sana na nilipokuwa nikimtazama ile shepu yake wakati anabadili zile chupi ni hakika ni kichaa tu ndiye angekubali kumpoteza Rehema.
Sasa baada ya Rehema kuanza kuweka mazingira ya kupika kule nje,niliichukua ile dawa nikaiweka mfukoni nikawa nimetoka nje.Sasa mahali nilipokuwa nikikaa mimi hakukuwa mbali na lerini(leri ya kati),niliondoka kuelekea huko lerini na nilipofika niliitupa ile dawa pembezoni mwa leri vichakani kisha nikarudi zangu nyumbani mdogo mdogo!.

Nilipofika nyumbani nikiwa nimewasha luninga naangalia,ghafla simu ya Ally Mpemba ikawa inaita,niliingalia ile simu kidogo nisiipokee ila niliamua kuipokea.

Ally Mpemba "Habari ya jioni master"

Mimi "Nzuri kaka,za huko"

Ally Mpemba "Uko wapi?"

Mimi "Nipo nyumbani kaka"

Ally Mpemba "Nilikuamini ila umejikosesha mwenyewe,jitafakari?"

Aliendelea "Kuna mtu naomba umkabidhi funguo wa nyumba yangu"

Mimi "Lakini kaka nimefanya mistake tu "

Ally Mpemba "wewe bado dogo haya mambo yatakugahrimu,shauri yako!"


Baada ya jamaa kuniambia vile akawa amekata simu,mimi niliamua likalotokea ngoja litokee lakini kiukweli sikutaka kabisa kumtoa kafara mwanamke mzuri Rehema ambaye hakuwa na hatia hata kidogo ingawaje pia nilikuwa nikimpenda sana tu!.Wakati nikiwa sebuleni Rehema alikuja kuniita ndani akisema kuna mtu ananiita nje.
Sasa nilipotoka nje nilikutana uso kwa uso na Farah na kiukweli mwanamke yule alikuwa akifanana sana na Maya na sikuwahi kuelewa alikuwa ndiye wa dukani pale kkoo au huyu yeye alikuwa ni nani?maana yule wa kkoo yeye aliwahi kuniambia hakuwepo kwa muda wa wiki 2,sasa Je huyu ni nani?,hilo lilikuwa ni swali gumu sana kwasababu hakuna aliyeweza kunipatia majibu.

Farah "Habari yako Master?"

Mimi "Nzuri dada Farah "

Farah "Naomba funguo wa nyumba"

Niliingia ndani kuchukua funguo kisha nikamletea,baada ya kumpatia ule funguo akanishukuru kisha akawa anatoka nje nami nikawa namsindikiza,sasa lengo langu ni tutoke nje nimuombe aongee na Ally Mpemba aniombee msamaha kwa kile nilichokuwa nimekifanya,sasa baada ya kutoka nje niliikuta ile Range ikiwa imepaki na sikutaka kabisa kusubiri ikabidi nimuulize funguo wa ile gari ameitoa wapi wakati mara zote nilikuwaga nikiiacha ndani ya ile nyumba na funguo wa nyumba ndiyo alikuwa amekuja kuuchukua!.Nilibaki nikishangaa sana.

Mimi "Dada nilikuwa nakuomba niongee nawe kidogo!"

Farah "Kesho tuonane!"

Mimi "Sawa"


Alipanda kwenye gari akawa ameondoka.Nilidhani uenda yeye alikuwaga na funguo wa lile gari lakini nilizidi kuchanganyikiwa kwasababu lile geti la ile nyumba lilikuwa limefungwa.Sikutaka kabisa maneno na Ally Mpemba kwasababu ni mtu aliyekuwa akiniamini sana na nilitaka kufanya kila kinachowezekana nimuombe msamaha.

Rehema "Huyo ni nani?"

Mimi "Ni mdogo wake na bosi wangu!"

Ilikuwa ni mara chache sana mimi kulala pale nyumbani kwangu tangia nimejuana na Ally Mpemba kila mara anapokuwa akisafiri,mara zote ambazo anakuwa hayupo nilikuwa nikilala pale kwake kwenye ile gari ndogo ambayo alinipatia.Sasa kwakuwa nilikuwa nishaharibu alinikataza kabisa mimi kulala pale kwake hadi nifanye jambo nililokuwa nimeelekezwa na Mzee wa Chumbe.

Ilipofika asubuhi baada ya kuamka nilijiandaa ili nielekee kwenye kazi yangu ambayo ilinipeleka pale Kkoo,nilipoondoka nyumbani niliamuacha Rehema akiwa amelala na niliamuambia akiondoka afunge nyumba na funguo aziache kwa demu wa Steve.Sasa nilipofika kkoo nilikuta tayari dada Farah amekwisha kufungua duka na swali lake la kwanza ni mbona tangia juzi sikuonekana?.

Farah "Sijakuona tangia juzi,kwema lakini?"

Mimi "Tangia juzi dada wakati jana umekuja nyumbani!"

Farah "Nije kwako hata napajua?"

Mimi "Dada wewe si jana umefata funguo wa nyumbani kwa kaka Ally!?"

Farah "Weeeee!....mjini hapa,isije ukawa umetapeliwa funguo za nyumba ya watu!"


Aliponiambia vile ndipo nikazidi kuchanganyikiwa na nikaona yawezekana kuna mchezo akawa uenda ananichezea pasipo mimi kufahamu!.

Mimi "Kwani dada nyie kwenu mko mapacha?"

Farah "Kwanini?"

Mimi "Nimeuliza tu!"

Farah "Hivi kweli wewe uko sawa?,nisije kuwa nazungumza na chizi!"

Mimi "Tangu lini nimekuwa chizi Aunt Farah?"

Farah "Vitu unavyoongea sikuhizi havieleweki kabisa master,umekuaje?"

Mimi "Dada mimi mbona niko kawaida!"

Farah "Ni juzi tu umetoka kuniambia nimefungua duka wakati mimi sikuwepo,haya leo tena umekuja na mpya kwamba nimekuja kwako kuchukua funguo za Ally?"

Aliendelea "Umewahi kuniona hata sura?"

Baada ya swali lake sikujua nimjibu nini kwasababu kila nilochokuwa nikimwambia alikuwa akiniona kama mwendawazimu na mara zote imekuwa ngumu sana kumjua Farah kwasababu amekuwa akivaa Nicab asubuhi hadi atakapofunga duka.Sasa ile siku aliyokuja kuchukua funguo wa gari ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumuona uso wake na wakati ananipigia simu aliniambia anaitwa Farah hivyo nikajua ni huyo mdogo wake na Ally Mpemba.Kiukweli hali ilikuwa mbaya sana.

Farah "Halafu pia umemfanya nini Ally?"

Mimi "Kwanini dada?"

Farah "Alinipigia simu akasema upishe karibu na duka "

Aliendelea "Ila sijamjibu"

Mimi "Mbona dada hakuna baya nililomfanya kaka Ally"

Basi baada ya yale maneno ya Aunt Farah nilifahamu kabisa hali ishakuwa mbaya sana,kibaya zaidi jamaa anahitaji niondoe biashara yangu kando ya duka lake,nilikaa kimya nikarudi kuendelea na kazi lakini kiukweli ni kama moyo ulikuwa ukinifukuta sana,nilinyanyuka kurudi dukani kwa Farah ili nimuulize swali na akinijibu nikishaelewa ningejua pa kuanzia.

Mimi "Kwani dada wewe huwa unapacha wako?"

Farah "Kwetu hatukuzaliwa mapacha!"

Mimi "Je,unamjua Maya?"

Farah "Maya?,ndiyo nani tena huyo mdogo wangu?"

Mimi "Kuna dada mmoja huwa mmefanana sana ndiyo maana nikadhani mlizaliwa mapacha"

Farah "Wewe unavituko sana,unamfananishaje mtu na mimi wakati hata sura yangu hujawahi kuiona!?"

Mimi "Sawa dada,Je Zahra unamjua?"

Farah "Zahra?"

Aliendelea "Eeh wewe umemfahamia wapi Zahra?"

Mimi "Unamfahamu?"

Farah "Ndiyo namfahamu!"

Mimi "Ni nani?"

Farah "Kwani wewe una nini?mbona naona mapicha picha tu!"

Mimi "Tafadhali Aunt Farah naomba uniambie kuna kitu utanisaidia na mimi nitakusaidia!"

Farah "Zahra alikuwa dada yangu toka ni nitoke ila kwasasa ni marehemu!"

Sasa kuna muda tunaongea tulikuwa tunasuburi wateja waondoke kisha wateja wakiondoka tunaendelea,kiukweli baada ya kumtajia Farah jina la Zahra alishituka sana na kushangaa,mimi kiukweli niliamua liwalo na liwe kwasababu ilivyoonekana ni kama Ally Mpemba alikuwa amenikataa na hata kama ningejipendekeza vipi asingenielewa.

Farah "Kaka Ally ndiyo alikwambia kuhusu Zahra?"

Mimi "Hapana dada!"

Farah "Ok wewe Zahra umejuaje na kuna kitu gani kumuhusu?"


Itaendelea.................
Kudadadeki nina siri zako halafu unaanza kuniletea ujeuri...

Liwalo na liwe..

Stori ni nzuri kwa kweli hongera mtunzi.
 
Msikie huyu,πŸ˜‚πŸ˜‚
katika kipindi nipo kwenye peak ya mapenzi ndiyo hichi ndiyo maana hata humu sipo nimeteqwa, likinikuta jambo narudi humu tena maana ndiyo pa kupunguzia machungu..!!
Hivi yule yule jamaa ambaye ulikuja unanililia na unataka ujitoe uhai maana mateso anayokupa ni zaidi ya mkuki wa moto moyoni ndo huyu unaemzungumzia hapa kuwa amekuteka na Penzi amelikoleza....?

Yule yule uliyesema amesababisha uwaone vidume wote ni mbwa ndio huyu aliyekufikisha KIBO ya mapenzi kiasi kwamba umepagawa...huambiliki?

Lahaulah!!!!! Pamoja na kukwambia uachane nae ndo kwanza umenigeuka?

Ngoja nishike jembe nikalime
 
Lucha ukuje kama masihara nimekutana na new episode naona bro kashindwa kutoa kafara kwa ajili ya ule mzigo nawaza anagekutana na flat screen zetu yan chap angetoa kafara, aisee kuna haja ya kwenda turkey kuondoa flat screen la.sivyo kifo nje nje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Turkey ukafanye nini wewe baby zu wengine tunapenda macho tu hata hapohapo kwenye niqab sasa utakua kila siku unarud turkey, ukirekebisha shape na sura tunaanza kupenda urefu , ukirud mrefu tunaanza kupenda mashavu si utamaliza nauli
 
Usiwaseme vibaya mkuu, hiyo ni kwa maoni yako. huyo demu unayesema anamtindi kuna mtu anaweza akamuona mzuri tu. Mfano mimi sipendi matako makubwa, sipendi demu mweupe, napenda demu mwenye umbo na rangi kama ya msanii ruby
Sio mimi nimewasema vibaya mkuu, mwenyewe nimewaonea huruma incase wakapita kusoma hapa watajisikiaje. Tunakosoana uumbaji wa Mungu as if tunaweza umba.
 
Mimi binafsi nimekutana na members wawili wa kike wa humu jf, wote wawili hawakuwa na mvuto. Mmoja alikuwa bonge mweusi ana maziwa makubwa hivi na nyuma kapigwa pasi, sikumtafakari sana maana tulikuwa tunafanya mabadilishano ya bidhaa kwa pesa. Mwingine alikuwa mfupi mweupe angalau alikua na muonekano, humu jf profile picture yake kamuweka mwanamke mrembo sana tofauti na yeye alivyo.

So kwangu kwa kutumia sample ya hao wawili nimeconclude kuwa wanawake humu wengi wao sio wazuri, labda wenzangu kama walikutana na warembo.
Mkuu nadhani shida yako ni nyota.

Binafsi nimekuwa close sana na wadada watatu (3) kutoka JF ambao hata kesho Jf ikifungwa nitakuwa proud sana kukutana nao.

Kwanza ni warembo, afu wako smart upstairs na ni watu ambao tunaexchange ideas, tunajoke na mambo mbalimbali ya maisha.

Wawili nimekutana nao face to face nyakati tofauti and I was proud to have met them and am so sure hata wao huko wanafurahia kumfahamu Fohadi.

Point yangu ni moja. Usifanye Generalization. Pili uzuri wa kitu upo kwenye macho ya mtazamaji. Pengine we unamuona huyo dada ni flatscreen ila kuna mtu mmoja kutoka sehemu moja ya dunia anateseka kwa ajili yake.

Tatu badili mindset yako, sio LAZIMA kwenye engagement ya mwanamke na mwanamme kutokee mahusiano. Ruhusu muda mwingine kupata new friends, business partners au exposure na ujifunze vitu kupitia wao pia. Life is so sweet when you create new friends.

Kingine, huko uliko umezungukwa na pisi kibao ambazo unaziona na kuzifanyia analysis hata kabla hujaziapproach. Sasa kwanini uhangaike kubet kwa anonymous? Yaan unatafuta pisi kwa kuangalia avatar?

Tahadhari tu. Kuna wanawake humu wana miandiko ya Kiume na vice versa. Kuna ndugu yetu mmoja (Mungu amrehemu) 98% ya wana JF tulijua ni mwanamke kwa aina ya threads alizokuwa analeta humu. Na usikute ukawa mmoja wa watu mliomfata PM kumnyapia...Ila siku amefariki ndo tukajua kumbe alikuwa mwanamme.

So, sio kila unayekutana naye unataka awe mwanajamii na wewe (mjamiiane), sometimes nenda na dhamira nyingine, pata exposure afu acha mambo mengine yatokee naturally in Long run.

Hizi betting unazofanya ndio maana unaokota hao unaowaita Wabovu maana hata huku duniani kwenye Mikeka betting ni ngumu.

Nakuacha na misemo hii

1. Expectations and reality are totally different....Punguza matarajio, utapata warembo.

2. The more you need them, the more you lose. Fanya kama unaipotezea hiyo dhamira yako afu uone kama hujakutana na pisi
 
Hivi yule yule jamaa ambaye ulikuja unanililia na unataka ujitoe uhai maana mateso anayokupa ni zaidi ya mkuki wa moto moyoni ndo huyu unaemzungumzia hapa kuwa amekuteka na Penzi amelikoleza....?

Yule yule uliyesema amesababisha uwaone vidume wote ni mbwa ndio huyu aliyekufikisha KIBO ya mapenzi kiasi kwamba umepagawa...huambiliki?

Lahaulah!!!!! Pamoja na kukwambia uachane nae ndo kwanza umenigeuka?

Ngoja nishike jembe nikalime
mtseeeeuuuuw' maphiiii...!!
Acha uongo uende mbinguni mdogo wangu mzuri, sijawahi kukuletea kesi yoyote ya mtoto wa mama mkwe wangu na unajua hili vyema...!!
 
Mkurya ume anza pigo za kike.andika vitu virefu

π‘¨π’•π’‚π’Œπ’‚π’† π’π’Šπ’‹π’Šπ’ƒπ’– 𝒑𝒐𝒗𝒖 π’π’Š π’Žπ’Œπ’† π’˜π’‚π’π’ˆπ’–
[emoji4][emoji4] unataka kutuoa kilazima mkuu
 
Mkuu nadhani shida yako ni nyota.

Binafsi nimekuwa close sana na wadada watatu (3) kutoka JF ambao hata kesho Jf ikifungwa nitakuwa proud sana kukutana nao.

Kwanza ni warembo, afu wako smart upstairs na ni watu ambao tunaexchange ideas, tunajoke na mambo mbalimbali ya maisha.

Wawili nimekutana nao face to face nyakati tofauti and I was proud to have met them and am so sure hata wao huko wanafurahia kumfahamu Fohadi.

Point yangu ni moja. Usifanye Generalization. Pili uzuri wa kitu upo kwenye macho ya mtazamaji. Pengine we unamuona huyo dada ni flatscreen ila kuna mtu mmoja kutoka sehemu moja ya dunia anateseka kwa ajili yake.

Tatu badili mindset yako, sio LAZIMA kwenye engagement ya mwanamke na mwanamme kutokee mahusiano. Ruhusu muda mwingine kupata new friends, business partners au exposure na ujifunze vitu kupitia wao pia. Life is so sweet when you create new friends.

Kingine, huko uliko umezungukwa na pisi kibao ambazo unaziona na kuzifanyia analysis hata kabla hujaziapproach. Sasa kwanini uhangaike kubet kwa anonymous? Yaan unatafuta pisi kwa kuangalia avatar?

Tahadhari tu. Kuna wanawake humu wana miandiko ya Kiume na vice versa. Kuna ndugu yetu mmoja (Mungu amrehemu) 98% ya wana JF tulijua ni mwanamke kwa aina ya threads alizokuwa analeta humu. Na usikute ukawa mmoja wa watu mliomfata PM kumnyapia...Ila siku amefariki ndo tukajua kumbe alikuwa mwanamme.

So, sio kila unayekutana naye unataka awe mwanajamii na wewe (mjamiiane), sometimes nenda na dhamira nyingine, pata exposure afu acha mambo mengine yatokee naturally in Long run.

Hizi betting unazofanya ndio maana unaokota hao unaowaita Wabovu maana hata huku duniani kwenye Mikeka betting ni ngumu.

Nakuacha na misemo hii

1. Expectations and reality are totally different....Punguza matarajio, utapata warembo.

2. The more you need them, the more you lose. Fanya kama unaipotezea hiyo dhamira yako afu uone kama hujakutana na pisi
Asipoelewa hapa hawezi kuelewa tena
 
Back
Top Bottom