Utajiri wa siri wa mchoma mahindi

Nilikoma kula mahindi dar yanawekewa mpaka chachandu na limao kwani wanakula wajawazito
 
Mnaongeaga kirahisi sana na mnakuwa na mawazo makubwa sana ya biashara yenye ndoto za "faida" tu hamkadirii risks zinazoambatana na biashara husika na dynamics za soko. Kwamba mtu akichukua mahindi 400 atauza amalize yote siku hiyo hiyo, na itakuwa hivyo daily? Kayasafirisha vipi? Kayachoma juani hajatumia mkaa? Bei yake huwa hiyo hiyo throughout the year nq hayaadimiki? Unauzia wapi na je unalipia eneo/ ushuru? Unauza peke yako (ushindani) kama upo? Nk. Nk.

Ndugu zangu maisha yangekuwa kama mnavyowaza nyie mnaojiita "motivational speakers" ambao infact mna-deliver utopian thoughts kwa vitu ambavyo hamkuwahi vifanya basi hakuna ambaye angelia shida na sisi wote wenye kima cha chini tungeenda kuuza mahindi.

Biashara sio mteremko wa maisha kwamba ukishindwa vyooote basi unafanya tu simply "unafanikiwa". Inahitaji kutulia kifikra, uzoefu na kazi ngumu kama kazi zingine zote tu otherwise utakesha kwa masangoma uchanjwe hadi sehemu za kukalia na ufanye vitu vya ajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…