Utajiri wako uko kwenye uaminifu, kujituma, na kuweka aibu pembeni

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Ukiona maisha yako hayaeleweki eleweki, kupata milo miwili au mitatu ni shida, juwa una mapungufu katika hivi vitu vitatu:-​
  • Uaminifu​
  • Kujituma​
  • Unaona aibu​
Wapo watu wengi wana mitaji midogo midogo na mikubwa, ila wanakosa watu wa kusimamia shughuli zao, kwa sababu vijana wengi wana ona aibu kwa kubagua kazi, hawana uaminifu, na wakati mwingine hawako tayari kujituma.

Kwa mazingira haya; vijana tuamke.​
 
Mchungaji anasema, usinifuate mimi ninavyoishi bali fuata neno ninalokuhubiria.
Swali, kwa nini walimu walio wafundisha viongozi, wao sio viongozi?
Inabidi wewe ndio uwe mfano ili tujifunze kupitia wewe ..
Sasa tuambie utajiri wako ni kiasi gani, una miliki nini? Ili tuone picha halisi ya ulichokiandika..
 
Ukiona maisha yako hayaeleweki eleweki, kupata milo miwili au mitatu ni shida, juwa una mapungufu katika hivi vitu vitatu:-​
  • Uaminifu​
  • Kujituma​
  • Unaona aibu​
Wapo watu wengi wana mitaji midogo midogo na mikubwa, ila wanakosa watu wa kusimamia shughuli zao, kwa sababu vijana wengi wana ona aibu kwa kubagua kazi, hawana uaminifu, na wakati mwingine hawako tayari kujituma.

Kwa mazingira haya; vijana tuamke.​
Maisha ni kupambana bila kuchagua kazi.
 
Ingekuwa hivyo, kusingekuwa na waandishi wa vitabu
Waandishi wa vitabu wengi ni matajiri mkuu. Na siyo kwa sababu ya vitabu, bali wanandika vile wanapitia KATIKA maisha ..mfano master Kiyosaki yule ni millionaire na vitabu vyake vingi vimempa pesa kwa sababu ameandika vitu ambavyo anaishi..
 
Achana na vitabu vya stori; naulizia vitabu tunavyotumia vyuoni na mashuleni
 
Daah ishu ya utajiri imekaa kiroho zaidi! Ndo maana sio kila mtu ni tajiri! Labda unazungumzia utajiri upi? Huu wa kuwa na kazi ya kuajiliwa, gari na nyumba?
Saa nyingine utajiri ni Bahati vile mwenyezi Mungu alishakuandalia mapema.
Kuna watu wanapambana sana hawatoboi.
Utajiri/kuwa tajiri ni Dhana pana sana.
 
Ukiona maisha yako hayaeleweki eleweki, kupata milo miwili au mitatu ni shida, juwa una mapungufu katika hivi vitu vitatu:-​
  • Uaminifu​
  • Kujituma​
  • Unaona aibu​
Wapo watu wengi wana mitaji midogo midogo na mikubwa, ila wanakosa watu wa kusimamia shughuli zao, kwa sababu vijana wengi wana ona aibu kwa kubagua kazi, hawana uaminifu, na wakati mwingine hawako tayari kujituma.

Kwa mazingira haya; vijana tuamke.​
Mimi ningekubaliana na wewe endapo ungebadilisha heading ya uzi ingesomeka"Jinsi ya kupata hela ya kula/kujikimu" na sio utajiri,unapoongelea utajiri sio jambo la masihara.
Kwa maisha ya sasa wanaotusua au kutajirika ni wale watu wanaofanya smart work not hard work plus connection.
Bila smart work na connection utakesha na kufanya kazi masaa 24 kila siku ila utaishia kupata ya kununua ugali na maharage kisha watoto waende chooni basi ila sio kuwa tajiri.
 
Kweli kabisa abadilishe heading! Iwe ishu ya kujikimu! Utajiri una mambo mengi sana sana!
 
If you want to be rich do what richests done.

Embrace honest
Work smart
Shameless.

Mkuu tajiri hata ukimfilisi peza zote then baada ya muda unamkuta ametoboa tena.

Na masikini hata umpe kila aina ya Mali ataishia kutapanya ili aaweze kurudi katika nafasi yake.
 
Anatoba ni kwa sababu Siri ya utajiri wake anaujua yeye mwenyewe ndo maana anaweza kutoboa!
Haya mambo ya work smart, sijui honest, sijui shameless utayafata na hutatoboa abadani mpaka mtu anaingia kaburini! Labda kuishia hela ya kupata kubadilisha mboga.
Utajiri una mambo mengi sana na umekaa kiroho zaidi ndo maana si kila mtu ni tajiri.
 
Yeah kuna watu wako honest ila kila siku wanalizwa na kupata hasara bado huwezi kutajirika.
Hakuna mtu atakayekusifia kwa wema wako au uaminifu wako na kukupa unachostahili sana sana watakusifia baada ya kufa.
 
Uongozi ni kipaji sio kufundishwa shule.
Ni wapi uliona watu wanafundishwa kuwa mbunge au kuwa mkuu wa mkoa?
Ni sawa na kuwa mjasiriamali; wapo wanaofundishwa na kufanya na pia wapo waliozaliwa na kipaji hicho
 
Back
Top Bottom