Wordsworth
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,191
- 3,360
Nyerere, pamoja na matatizo yake yote alikomboa maskini kwa njia ya redistribution of resources. (ingawa angefanya kwa njia nyingine) Hakuwa na watendaji wazuri na viongozi wenzake wakati ule hawakumulewa (ni ngumu sana kumuelewa idealist na mtu mwenye vision ya miaka zaidi ya 100 ijayo).
Ninachotaka kusema kwamba yasingefanyika yale yaliyofanyika miaka hio, leo hii mwenye nacho angebaki nacho na asiyenacho asingekuwa na namna yoyote yakufanya ili na yeye awe nacho.
Pamoja na matatizo yote tuliyonayo Watanzania bado tuna uwezo wa kutafuta na kupata (social mobility). Hii ni kwa sababu rasilimali kama vile ardhi bado vipo mikononi mwa wananchi. Sisi siyo kama Kenya, Nigeria au mataifa yaliyoendelea ambapo wenye ardhi ni watu wachache sana na wanaobakia wanateseka na inabidi watafute njia nyingine ya kuingiza kipato. Ardhi ni ya thamani sana hatujui tu.
Huku Tanzania watu wengi wana ardhi za kurithi za mababu zao. Sipendi kujumlisha watu kwenye category moja lakini ukweli lazima usemwe tu. Vijana wengi wa Kitanzania na Watanzania kwa ujumla ni wavivu. Yaani wewe mtu na akili zako na nguvu zako unaondoka shambani unafuata mkumbo wa kwenda mjini eti kwa kisingizio cha kutafuta kipato. Unafika unaenda kukalisha makalio yako kibandani kwenye njia ya wapita miguu unauza dodoki. Eti na wewe unatafuta riziki. Huwezi hata kujiuliza hii shughuli ninayofanya hapa inasaidia vipi katika kuimarisha uchumi wa nchi.
Unamuacha mzee kijijini alime, wewe kijana mwenye nguvu unaenda kujikalisha mjini. Unashindwa kweli kufanya kilimo? Hapa najua majibu yenu ni kwamba kilimo ni kigumu blah blah blah nyingi. Ni hivi hakuna kitu kirahisi na kama unataka njia za mkato utaishia pabaya tu. Mpe hiyo ardhi uliyoikimbia Mnigeria au Mkenya akuoneshe. Au unyanganywe ndio utaelewa umuhimu wake?
Haya basi umelazimisha kuhamia mjini. Wakati wa Kikwete masoko ya machinga yalijengwa yakutosha ili wafanyabiashara wadogo wafanye kazi. Waliyakataa. Yaani mtu unakimbia sehemu ambayo ni rasmi ambapo ungetambulika kwenye mifumo yote ya nchi? Upo tayari kufanya biashara ambayo hata ukiumwa huwezi kuingiza kipato? Mnajua umuhimu wa kutambulika? Mnafahamu kwamba mngeweza kujikusanya na kupata mikopo ya vijana isiyo na riba halmashauri na kwenye baadhi ya mabenki?
Unakaa barabarani huna ujuzi wowote, hata kwenda VETA? Ukiingiza bando la mtandaoni ni kushinda kwenye udaku na kubeti hamna unachojifunza ili kuboresha maisha yako. Unaoa na kuolewa na unapata watoto. Unategemea kuwalisha kwa biashara za barabarani? Ukiumwa au mkitimuliwa inakuwaje? Ukizeeka utabaki kulalamika na kutamani urudishe miaka nyuma
Narudia tena hakuna kitu kirahisi lazima ujitume kimwili na kiakili. Kuwepo kwenye mifumo rasmi ni muhimu sana. Leo na kesho ukiumwa au ukifa bado biashara yako itaendelea. Watoto wako watarithi kibanda chenye uhakika. Mnafikiri familia zenye pesa (naongelea old money siyo hawa new money wanaorudi kwenye umasikini baada ya kizazi kimoja) muda wote wanapesa tu hawaishiwi? Wanaishiwa, lakini kwa sababu wanatambulika kwenye mifumo wana kopesheka na wana bima za kutosha hawawezi kuwa masikini. Uliyejikalisha hapo barabarani una hata bima ya afya?
Ninachosema hapa hakiwezi kutatua tatizo la umaskini katika jamii, umasikini ni mfumo na kinachohitajika ni jitihada za kutosha zikiongozwa na serikali kulitatua tatizo hili.
Ninachosema ni hatua mtu binafsi anazoweza kuchukua ili kuhakikisha anaboresha maisha yake yeye na ya watoto wake. Mifumo inafanya tajiri aendelee kuwa tajiri na masikini aendelee kuwa masikini. Hakikisha unakuwa katika mfumo rasmi ili uondokane na hili janga la umasikini. Tupo kwenye nchi ambayo bado matabaka kwenye jamii hayajakomaa. Huko baadaye yakikomaa utajutia kweli ujana wako na kwa nini hukutaka kuhangaika.
Na serikali nayo imelala sijui imekufa. Mipango miji ilitenga maeneo ya huduma za jamii ikiwemo masoko madogo kwenye maeneo ya makazi ya watu. Hayo maeneo yako wapi? Mliwauzia watu binafsi au?
Mwenye masikio na asikie.