Utakapokuwa Askari Usisahau mambo haya

Utakapokuwa Askari Usisahau mambo haya

Dalili moja wapo ya Askari Muovu ni kujipendekeza na kiherehere, ujapokuwa kiherehere Watawala watakutumia kwenye kazi zao Ovu na hatari, nawe utashindwa kukataa Kwa sababu unapenda kuwafurahisha, pengine ukafikiri watazidi kukupenda lakini sivyo, kwani utaangamia Kwa Uovu wako mwenyewe.
Dalili ya mtu mwovu ni kujipendekeza na kiherehere.......Hii nimeichukua Tycoon
 
kuna wajinga wataona kama umewasema watu flani flani . natamani kila askari asome.

sijawahi kusoma uzi mkali na uliosimama kama huu. kuna muda nilikuwa nahsi kama nasoma kipande cha biblia kilichokataliwa.
Huu uzi umekaa kama kitabu cha Hekima ya Suleiman
 
Usibishane Na Mkuu wako akuagizapo, ukijua kuwa Mkuu wako amekuagiza kutokana na jinsi ulivyojionyesha tangu siku ya Kwanza. Ukiona amekutuma kwenda kudhulumu basi jua wewe ni mdhulumaji na ulijitambulisha hivyo kimatendo.
Jamaa wewe ni hazina. huu ni Wahayi sio maneno yako. Nahisi ujumbe huu watoka kwa Malaika Gabrieli.
 
Mkuu ROBERT HERIEL hii inafaa tuiwekee misitari na iongezwe kwenye Biblia kabisaa
Naunga mkono hoja. Biblia ni muunganiko wa vitabu. Havikupatikana kwa siki moja. Hiki naona kilosahaurika au kilikuwa hakijatufikia. Tukiongeza kitakuwa cha 78 kwa Hypocripher au cha 67 kwa Duetrocanon
 
Wadanganye wenye mawazo kama yako,askari anaruhusiwa kufanya hivyo endapo muharifu anahatarisha maisha yake au ya watu wengine ndio maana wanakuwa public armed na kwa kumbukumbu zaidi rejea kwa hamza move za waarabu zilimdanganya akavuna alichopanda.
Niliwahi kusoma katika historia kuhusu vita ya dunia kwamba kuna kabila hapa Afrika lilikuwa na wastani wa akili asli (IQ) chini ya wastani au pungufu. Mtu wa kabila hilo aliposhitukizwa akashikwa na adui mmoja tu, adui alikuwa na kiburi cha kumuuliza mateka achague anataka auawe vipi. Mwishowe adui alimwamuru mateka achimbe kaburi ili amzike akiwa hai! Na kweli yule mateka akafanya hivyo! Ikumbikwe hata kwenye sheria za kimataifa, ukisha mdhibiti adui huruhusiwi kumwua au kumtesa isipokuwa kama hafuati masharti ya mateka! Mwandishi wa Vita anauliza kuwa kwa nini huyu Mkabila hakuchagua afe akipigana pengine angeshinda kuliko alivyoamua afe kwa kuchimba kaburi lake azikwe hai bila kujaribu bahati yake kwa kupigana; kwamba kote ni kufa lakini kupigana matokeo yake ni kama kutupa karata. Ndiyo maana akili asili hapo inahusushwa! Leo Watanzania wazima mnaamini askari ana ruhusa ya kumwua au hata kumtesa raia kwa amri ya kiongozi bila kufuata sheria! Mjue kuwa kwa mujibu wa sheria, hata askari anayejitetea anatakiwa atumie nguvu kiasi ya kumshinda adui tu na si zaidi ya hapo. Nchi ye yote inayotawaliwa kwa misingi ya demokrasia na haki za binadamu jambo moja la muhimu kabisa katika Katiba yake ni kulinda, kudumisha uhai wa raia na mali za raia wake.Mazingira yanayoruhusu askari kutoa uhai wa mtu yameainishwa katika sheria. Kama mmezoezwa raia kuuawa au kupigwa sasa mmefikia kiwango cha kuwaasa askari ambao ni walinzi wenu namna ya kuwafanyia jinai kwa huruma, kwa mfano kuwapa fursa za sala na kadhalika kabla hawajatoa roho zenu, basi inaonesha uelewa wenu ulivyo duni. Lakini kuwa na thubuti ya kuandika kutetea hoja kama hiyo hadharani kama mnavyoandika kwenye uzi huu INATISHA na ni AIBU; pia inaonesha ambavyo katika Tanzania yetu UELEWA wa mambo unavyoporomoka! Ndiyo maana awali niliuliza Tanganyika tulipigania uhuru wakati tulikuwa tunatawaliwa na mkoloni ili iweje kama siyo kujihakikishia na kulinda uhai, utu, mali na maendeleo yetu!!
 
Ndiyo maana akili asili hapo inahusushwa! Leo Watanzania wazima mnaamini askari ana ruhusa ya kumwua au hata kumtesa raia kwa amri ya kiongozi bila kufuata sheria! Mjue kuwa kwa mujibu wa sheria, hata askari anayejitetea anatakiwa atumie nguvu kiasi ya kumshinda adui tu na si zaidi ya hapo
Kwamba ukihatarisha usalama anaruhusiwa kukuua,,, ila yeye akihatarisha usalama wako huruhusiwi kufanya lolote....

Hii nchi awareness ya sheria bado ni ndogo sana,, na hawataki Raia wazijue kwasababu wakizijua uonevu utaisha,, na pia werevu wakiwa wengi ni mwiba kwa watawala
 
Taikuni aisee Bila kujipendekezi kwa vyombo vyetu vya bongo hutoboi
 
Back
Top Bottom