Utalipwa Dola $200,000 ikiwa utatoa sura na sauti kwa Roboti

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Utalipwa Dola $200,000 ikiwa utatoa sura na sauti kwa Roboti



Kampuni ya kuunda Maroboti toka Russia Prompt imeweza kutoa ofa ya Dola $200,000 kwa mtu Yeyote anayetaka kuchukua sura yake apewe Roboti pamoja na sauti kwa ujumla.

Roboti huyo ataweza kuwa na hati miliki kamili kuanzia sura na sauti yako ambayo itaweza kutumiwa Maeneo ya hotelini, migahawani, hospitali na Maeneo mengine ya umma.

Kampuni hiyo imesema Tayari imeshapokea zaidi ya maombi ya watu 20,000 ambapo wanasema wameshangazwa muitikio wa watu umekua mkubwa hawakutegemea kabisa. Mchakato mzima wa kuunda Roboti kwenye muundo wa 3D ambapo ataweza kufanana kama alivyo mwanadamu.



Endapo utachaguliwa kuweka sauti yako kwa Roboti basi utaweza kurekodi sauti yako ndani ya masaa 100 ya hotuba ili kuweza kutoa sauti kamili na taarifa nyingi ili Roboti aweze kuzungumza vyakutosha kampuni hiyo ilisema.

Kwa sasa matumizi ya Roboti kwa nchi za ulaya yamekua makubwa kwani zinatumika mahali tofauti unaweza safiri kwenye usafiri wowote wa umma ukapanda na Roboti kwenye nyumba za kuishi, mikusanyiko nk.
 
Unajiungaje?
 
Sura na sauti tu? Kuna watu watatoa hata figo.
 
Nitawafanyia laki naomba utaratibu
 
Link ya kuapply iko wapi?
 
Nimepokea reply email yao baada ya kuomba miezi 3 iliyopita wanasema niko peke yangu Afrika.
Hapa nakula mayai tu na urojo, asali mbichi, kujiweka sawa kwa kuingiza sauti.

Link nitaiweka hapa, punde
 
Mbona hii habari ni ya 2021 desemba.
 
Dollar 200,000 Kwa gharama ya leo 1$ ni TShs. 2,658.92

200,000 x 2,658.92=531.7M

Hizo ni hela nyingi sana Kwa kuweka sauti na Sura yangu Kwa robot

Wailete Afrika hiyo offer tuichangamkie
that is not a problem the issue is what if your twin robot will do any violence..?
can't that be a problem to you because all police they'll be after you..! hizo dollar zitageuka shubiri..🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…