sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nipo njia panda wakuu,
Zamani enzi zetu miaka ya nyuma kidogo kuna baadhi ya makabila kwenye koo flani ilikuwa ni lazima upewe kinga, haya mambo yalianza zamani sana tunaambiwa ni baada ya wahamiaji wapya, kuowa nje ya ukoo, kuchanganyana na koo mpya kukaanza kujitokeza mambo ya teknolojia ya giza kwa hio ndo hizi kinga zikaanza kutengenezwa na baadhi za koo kwenye kabila.
nakumbuka nikiwa mdogo mimi na watoto wa rika langu wa kwenye ukoo tulipashiwa maji yamoto kwenye chungu wajaweka dawa wakaanza kutumbukiza matawi ya mti flani tukaambiwa tuvue nguo zote tukaanza kama kuchapwa na hayo matawi mwili mzima, baada ya hapo tulichanjwa na nyembe na kuwekwa dawa na kupewa masharti tusije kula maini, tusije kula nguruwe, tusije kukalia kinu.
Kwangu binafsi nmeskia stori nyingi za shuhuda za hii ila kwa mimi kama mimi nilichoshuhudis ni watu wa karibu waliowahi kuniibia vitu hasa vya gharama nliwakuta navyo kabla hawajaviuza mara kadhaa, pia kuna mtaa niliwahi kupanga uswazi nikiwa chuo ili nibane pesa, ile nyumba baada ya siku 2 nikaanza kusikia vishindo darini, asubuhi wapangaji wakaniambia ni tatizo la muda, baada ya wiki 2 tatizo likajirudia, baada ya fujo za vishindo kwa dakika 5, kishindo kikubwa mno kililia batini mithiri ya mtu kudondoka na wapangaji wote tulitoka nje kuangalia juu kuna nini huku tukiwa na hofu ila hatukuona kitu, siku inayofata mtoto wa mama mwenye nyumba alikuwa kanikunjia sura huku mama yake hajatoka nje tangu asubuhi, nikahama siku hio hio na kuacha kodi yangu.
Ila masharti yake kiukweli ni mzigo, hutakiwi kukalia kinu, hutakiwi kula nguruwe na hutakiwi kula maini. ukienda kinyume na hapo ndo basi umeifuta na unatakiwa uende ku renew upya.
Sasa shida zote za nini hizi, Ninataka kujenga hoja ya namna ya jisi ya kuwaambia hao ndugu kwamba haya mambo kwa watoto wangu yatakuwa magumu, maana hata mama yao tu hachangamani kabisa na haya mambo,
sijui nifanye nini