Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Nguvu ya utamaduni. Huwaleta watu pamoja, huwafanya kuwa pamoja, huwaunganisha na Kuwapa nguvu yenye mshikamano imara sana!
Je tuna utamaduni wa mwafrika? Ni upi? Je tuna utamaduni wa Mtanzania? Ni upi?
Maana utamaduni ni uchumi, Utamaduni ni sera. Utamaduni ni siasa, Utamaduni ni imani
Utamaduni ni uhuru, Utamaduni ni maendeleo.
Hakuna utamaduni wa kukopea, hakuna utamaduni chotara, hakuna utamaduni wa kuiga.. Huo ni Utumwa na fikra finyu.. Utamaduni hauchakachuliwi.
Watu waliosimamia tamaduni zao hata uchumi wao uko imara, utaifa wao si wa mashaka na uzalendo wao ni wa vitendo kuliko maneno!
Mifano michache wa juu ya utamaduni. Waangalie wachina.. Chochote watakachofanya watajiangalia wao kwanza kama taifa, Waangalie waarabu. Waangalie wahindi nknk.. Halafu waangalie chumi zao zilivyo imara na wanavyoweza kujipenyeza nje ya mipaka Hao na kupata mafanikio makubwa!
Mchina popote alipo ulimwenguni haachi utamaduni wa kutumia vijiti kama vijiko.. Haachi utamaduni wa kuagiza vyakula toka kwao..! Matokeo yake huwaambukiza hata wenyeji na kujikuta nao ni wapenzi na watumiaji.. Je hapo wenyeji hawakuzi uchumi wa mgeni?
Vipi kuhusu kung fu na martial arts zingine!?
Utamaduni ni uchumi na ni biashara kubwa sana! Utamaduni wa Mtanganyika ni upi? Namaanisha Tanganyika kama taifa huru... Tulibakiwa na Wamasai kama kitambulisho cha utamaduni wa Mtanganyika nje ya mipaka.. Na kwa kutumia utamaduni wa Kimasai taifa limenufaika pakubwa kijamii kiuchumi na kibiashara pia!
Kwa kilichotokea Ngorongoro hivi karibuni ni mfano halisi wa kusimama na utamduni.. Mshikamano wenye sauti moja
Mifano halisi huleta uelewa wa haraka! Tanganyika tuna makabila zaidi ya 110.. Makubwa na madogo.. Ni makabila yale tu yaliyoweza kusimama na tamaduni zake ndio yaliyoweza kusikika zaidi na kunufaika zaidi katika nyanja karibia zote
Mfano halisi wa haraka watani zangu wachaga.. Hawa wapewe heshima yao kubwa!
Hivi ni katika kona gani ya Tanganyika utakosa haya mambo matatu? Mtori wenye nyama tatu.
Pombe ya mbege na kombe lake! Duka la mangi hata kama mmiliki si Mchaga?
Kuna tunu njema kubwa na ya ziada uchagani.. Thamani ya ardhi.. Mchaga atakupa kila Kitu lakini si ardhi yake huko uchagani
Tanganyika kama taifa huru hatuna utamaduni wetu bali tuna vitu vya kuletewa vilivyokosa uhalisia. Hivi ulishawahi kuona taifa linaendesha mashindano ya kutafuta vazi la taifa?
Tamaduni zilizo bora huyanufaisha na kuyainua mataifa yake kiuchumi, kiimani kijamii na kiulinzi. Tamaduni mbovu huziangusha himaya!
Kinachosimama na kusimamia tamaduni imara popote pale ni ardhi.. Hilo husemwa wazi na kwa sauti kubwa! Kwamba hapa ndio kwetu.. Hatuna pengine zaidi ya hapa! Kila kinachotuhusu sisi kitaanzia hapa!
Ardhi hufuatiwa na watu wenye kujielewa na kujitambua.. Watu hawa kutokana na ardhi yao huunda tamaduni zao
Tamaduni ni mila na desturi kwenye
Mavazi
Vyakula
Vinywaji
Urembo
Ala na midundo
Vyote hivi hufanywa na kufanyika juu ardhi na hufanywa na watu..!
Kwa baadhi ya makabila hakuna kitu kibaya kama kuuza ardhi.. Laana yake utauza mpaka nguo ya ndani na bado usifanikiwe wala usitosheke!
Je hii laana imeingia Tanganyika?
Je utamaduni wa Tanganyika ni upi?