SoC03 Utamaduni wa Kujiuzulu ni Uungwana na Njia Bora ya Uwajibikaji

SoC03 Utamaduni wa Kujiuzulu ni Uungwana na Njia Bora ya Uwajibikaji

Stories of Change - 2023 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Utangulizi
Katika mambo magumu katika nchi nyingi zinazoendelea hasa za Bara la Afrika, ni kujiuzulu au kwa maneno mengine, kuachia ngazi kwa viongozi katika nafasi wanazozishikilia pale ambapo mambo yanaharibika katika taasisi wanazoziongoza.

Ninapozungumzia juu ya kujiuzuli au kuachia ngazi, isitasfirike kwamba nawalenga viongozi wakubwa kama mawaziri na/au wakuu wa nchi pekee! La hasha, ni kuanzia viongozi wa kitongoji, kijiji/mtaa, kata, tarafa, wilaya, mkoa, na kuendeleza; viongozi wa vyama vya siasa; na viongozi wa taasisi, makampuni na vikundi mbalimbali katika sekta binafsi.

Kama viongozi wa ngazi za chini hawana utamaduni wa kujiuzulu nafasi zao pale mambo yanapoharibika, hata katika ngazi za juu, hali itakuwa hivyohivyo. Tumeshuhudia halmashauri na taasisi mbalimbali nchini zikibainika kuwa na ubadhirifu wa fedha na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa wa Hesabu za Serikali, lakini binafsi sijaona kiongozi aliyejiuzulu.

Utamaduni wa kujiuzulu, husaidia vyombo husika kufanya uchunguzi huru na kubaini chanzo cha tatizo, na kuchukuwa hatua stahiki, na endapo wale waliojiuzulu hawakupatikana na kosa, inakuwa fursa nzuri ya kuwasafisha kwa jamii na umma kwa ujumla.

Mfano wa Watu Waliowahi Kujiuzulu Nafasi Zao hapa Nchini
Kwa nchi yetu, wapo viongozi wachache wa ngazi mbalimbali ambao waliwahi kujiuzulu nyadhifa zao. Katika Makala hii, nitataja viongozi wawili ambao naamini wanafahamika sana; Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, miaka ya 1970; kipindi hicho kulitokea mauji maeneo ya Kanda ya Ziwa yaliyohusishwa na imani za kishirikina. Waziri Ali Hassan Mwinyi alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri wa Mambo ya Ndani kufuatia matukio hayo, ingawa hakuhusika moja kwa moja. Mwinyi huyu ndiye aliyekuja kuwa Raisi wa Zanzibar mwaka 1984 kufuatia kujiuluzu kwa Aboud Jumbe, na baaaye Raisi wa Jamuhuri ya Tanzania, mwaka 1985, baada ya Hayati Julius Kambarage Nyerere kung’atuka.

Mtu mwingine ni Hayati Julius Kambarage Nyerere, aliyeachia madaraka mwaka 1985 akiwa bado ana nguvu na akihitajiwa na wananchi. Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho hali ya Uchumi ilikuwa ngumu sana, na hivyo akaona ni busara kutoa nafasi kwa mtu mwingine, naye awe pembeni kutoa ushauri. Uamuzi huu ulimfanya kuwa mtu mashuhuri ndani na nje ya nchi, na ndio maana mpaka leo anaheshimika kama Baba wa Taifa la Tanzania.

Kumbe kuna faida ya kujiuzulu kwa faida ya umma. Ali Hassan Mwinyi alijuzulu kama Waziri wa Mambo ya Ndani, baadaye akaja kuwa Raisi wa Zanzibar, na muda mfupi baadaye akachaguliwa kuwa Raisi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hayati Julius K. Nyerere aliachia madaraka (aling’atuka) kama Raisi wa nchi, akapata heshima ya kuwa Baba wa Taifa.

Katika Nchi Zilizoendelea Kujiuzulu ni Jambo la Kawaida
Kwa nchi zilizoendelea hiki ni kitu cha kawaida, ambapo Mkuu wa Taasisi au Wizara na hata Mkuu wa nchi hujiuzulu mara moja kabla ya kupigiwa kelele na wale wanaowaongoza ikiwa kuna jambo halikufanyika, au limefanyika kinyume na matarajio ya wengi – hata kama hawakuhusika moja kwa moja na makosa hayo. Sababu ni kwamba, watu hawa, kwao uongozi unachululiwa kama wito na fursa ya kuonyesha uwezo na shauku ya kuwezesha maendeleo ya jamii au jumuiya husika. Kwa maana hiyo, uongozi huchukuliwa kama wito na fursa ya kuonyesha uwezo na ubunifu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii husika.

Kwa Nchi zinazoendelea, Ni Vigumu kwa Viongozi Kujiuzulu
Kwa upande wa nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, mara nyingi, uongozi huonekana kama fursa ya kujineemesha yeye pamoja na familia yake, badala ya jamii iliyolengwa, na ndiyo maana migogoro ya kutafuta vyeo haiishi iwe serikalini, katika taasisi mbalimbali (binafsi na za umma), na jamii kwa ujumla. Nchi nyingi zinazoendelea, hasa za barani Afrika, vurugu zinazotokea mara kwa mara, kwa kiasi kikubwa zinatokana na ubinafsi na uchu wa madaraka.

Watu Mashuhuri Duniani Walioachia Nafasi Zao
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi (Februari 18, 2015), Mwaka 2008 nchini Ufaransa, Mnadhimu wa jeshi alijiuzulu baada ya askari kutumia risasi za moto kwenye mazoezi na kujeruhi raia 17 (sio kuua).

Kwa mujibu wa Major Dan (Juni 9, 2020), baadhi ya viongozi wengine mashuhuri duniani walijiuzulu kwa sababu mbalimbali ni kama ifuatavyo:
Kaiser William German.png

1. Mfalme Kaiser Wilhem, Ujerumani, 1918;

Rais Richard Nixon USA 1974.png

2. Raisi Richard Nixon, Marekani, 1974;

Sarah Pallin Alaska 2009.png

3. Gavana Sarah Palin, Alaska, 2009;

King Edward VIII 1936.png


4. Mfalme Edward VIII, Uingereza, 1936;

Pope Benedict VII .png

5. Papa Benedict XVI, Roman Katoliki, 2023;

VP Spiro Agnew USA 197.png

6. Makamu Raisi, Spiro Agnew, Marekani, 1973;

Sir Anthony Eden UK.png

7. Waziri Mkuu, Sir Anthony Eden, Uingereza, 1957;

Mikhael Gorbachev USSR.png

8. Raisi Mikhael Gorbachev, USSR, 1991;

Ton Blair UK.png

9. Waziri Mkuu Sir Tony Blair, Uingereza, 2007; na

King Shah Iran 1979.png

10. Shah Mohammad Reza, Iran, 1979.

Chanzo: Major Dan (Novemba 9, 2020)

Mapendekezo

Serikali, ikishirikiana na wadau mbalimbali, itengeneze mfumo maalum, sera na sheria vitakavyosimamia Uwajibikaji na Utawala Bora katika sekta zote kuanzia ngazi za chini (mashinani) hadi ngazi za juu.

Elimu endelevu ya uraia inayosisitiza uwajibikaji na utawala bora katika sekta zote, itolewe kwa kiasi kikubwa, katika sekta ya elimu (kuanzia shule za msingi hadi vyuoni); katika taasisi nyingine mbalimbali (za serikali na za binafsi); na kwa umma, kupitia mikutano ya hadhara, makongamano, na vyombo vyote vya habari.

Hitimisho
Utamaduni wa kujiuzulu ukihimizwa kuanzia ngazi za chini katika sekta zote, matukio ya uzembe kazini, ubadhirifu, rushwa aina zote, manyanyaso, na mambo mengine mabaya katika nafasi za kazi au uongozi vitapungua kama si kutokomezwa kabisa; na kwa muktadha huu nchi itapiga hatua kubwa katika maendeleo ya jamii na ya kiuchumi.

Marejeo
Major Dan (Novemba 9, 2020), “Leaders Who Quit, Abdicated, or Resigned”.

Mwananchi (Februari 18, 2015), Utamaduni wa Viongozi Kujiuzulu Haupo Nchini
 
Upvote 3
Kuachia madaraka pale unapoona mambo hayaendi vyema, ni kujitengenezea heshima ya kudumu.
 
Back
Top Bottom