Utamaduni wa kututanganzia viongozi wakuu na wastaafu wanapoumwa haupo, inapotokea tunapata mashaka

Utamaduni wa kututanganzia viongozi wakuu na wastaafu wanapoumwa haupo, inapotokea tunapata mashaka

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Ukweli usemwe tu!

Kiongozi anapoumwa hapa nchini kwetu imekuwa kama kasumba kuficha ficha sana kutoa taarifa.

wakati ni haki ya umma kufahamishwa alipo mtumishi wao wanayemlipa!
Hata taarifa zinapotoka huwa kwa mbinde sana!

Na taifa hilihili linapotoa taarifa kirahisi pasipo kuombwa ombwa basi taarifa hiyo rahisi ya kiongozi kuumwa mara nyingi hufuatiwa na taarifa mbaya ya msiba!

Hii inatupa tafsiri gani kama wananchi; kama nikuficha bora iendelee kubakia kuwa siri maana mnatuchanganya!

Unless serikali iseme wazi leo kwamba haitaficha ficha tena kiongozi yoyote anapaumwa kama wenzetu huko ulaya hawafichi kitu hata rais akianguka bahati mbaya wanasema wazi kaanguka!
 
424748227_699789145679373_4700732109160916132_n.jpg
 
Labda akifariki ila Sababu hasa ya kutaka kujua kila anapougua tuambiwe ni ipi hasa?

Akifariki anachaguliwa/anateuliwa mwingine hivyo lazima uma ujulishwe. Kama ni raisi mstaaf kama Mwinyi wala hakuna uchaguzi/uteuzi.
 
Kwanini wanaotutangazia tu ndo wanakufa? Maana yake taarifa zao huwa hazina lengo zuri la kuufahamisha umma
 
Salim Ahmed imetangazwa siku nyingi anaumwa na bado yuko hai

Mzee wa mia 98 kunaweza kuwa na sababu gani ya kushangaza kuumwa au kufariki?
 
Back
Top Bottom