Utamaduni wa Rushwa Polisi ni mkubwa sana

Utamaduni wa Rushwa Polisi ni mkubwa sana

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nashukuru Raisi ameunda kamati maalumu ukweli ni kwamba utamaduni wa rushwa ni mkubwa sana Polisi
 
Attachments

  • IMG_0344.MOV
    2.4 MB
Nafungua shule ya nidhamu kufundisha watoto kutokuwa wizi wala waongo na kutokuwa matapeli.

Maana naona wasomi wengi na wafanyakazi ni waizi tu kuanzia juu mpaka mfagiaji.

Rushwa inaimbwa eti adui wa haki, unaingia ofisi zao zimeandikwa kabisa kataa rushwa ila utaulizwa tu na utatoa
Ukishtaki kunakohusika nao wanawapigia uliowashtaki na kusema jamaa kawachoma anakuja na hela moto mzikatae.

Yaani hata Congo yapo haha.
 
Nashukuru Raisi ameunda kamati maalumu ukweli ni kwamba utamaduni wa rushwa ni mkubwa sana Polisi
Polisi ni genge la waporaji waliovalia nguo za majeshi halali; naamini picha mwendo hii akiiona mh Rais wa Zanziba Dk Hussein Ali Mwinyi atachukua hatua kama ilivyo ada kwake maana hapendi dhuluma kama hizi za walinzi wa mali na raia. Huyu anatakiwa aoneshwe mfano kwa kufunguliwa mashitaka mahakamani kuliko kumfukuza pekee; sifa mbaya wazungu wanazipeka kwao eti nchi imefunguliwa wakati watumishi wameoza kwa uhalifu.
 
Polisi ni genge la waporaji waliovalia nguo za majeshi halali; naamini picha mwendo hii akiiona mh Rais wa Zanziba Dk Hussein Ali Mwinyi atachukua hatua kama ilivyo ada kwake maana hapendi dhuluma kama hizi za walinzi wa mali na raia. Huyu anatakiwa aoneshwe mfano kwa kufunguliwa mashitaka mahakamani kuliko kumfukuza pekee; sifa mbaya wazungu wanazipeka kwao eti nchi imefunguliwa wakati watumishi wameoza kwa uharifu
Rushwa za polisi ni kama biashara, mara nyingi haziachi masizi wala malalamiko, rushwa hizi mlalamikaji hubaki kuwa ni kiongozi wa serikali anayeigiza kupambana nazo, si aliyetoa rushwa.

Lakini zile rushwa ambazo ni mbaya kabisa, mfano mahakamani, makazini, ktk vizuizi vya mipaka, ambavyo huacha alama na malalamiko mengi hata hasara kwa taifa, hakuna hata mtu mmoja anayejaribu kuhangaika nazo.

Shida yetu kama binaadamu ni unafiki. Amini amini amini nawaambia, haitakwisha rushwa miongoni mwetu, mpaka siku tumeamua kuwa waaminifu ktk nafsi zetu.
 
Polisi ni genge la waporaji waliovalia nguo za majeshi halali; naamini picha mwendo hii akiiona mh Rais wa Zanziba Dk Hussein Ali Mwinyi atachukua hatua kama ilivyo ada kwake maana hapendi dhuluma kama hizi za walinzi wa mali na raia. Huyu anatakiwa aoneshwe mfano kwa kufunguliwa mashitaka mahakamani kuliko kumfukuza pekee; sifa mbaya wazungu wanazipeka kwao eti nchi imefunguliwa wakati watumishi wameoza kwa uharifu
Hii ni ya kitambo sana, sijui hata kama huyo polisi alichukuliwa hatua zozote.
 
Back
Top Bottom