Utamkumbuka Edward Lowassa kwa mambo gani?

Utamkumbuka Edward Lowassa kwa mambo gani?

Habari Wadau,

Leo Februari 10, 2024 Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametangaza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mgombea Urais wa CHADEMA mwaka 2015 Edward Ngoyai Lowasa

Soma: Breaking News: - Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Katika mwaka enzi za uhai wake Mzee alipata kuwa na ushawishi Mkubwa nchini kiwango cha kuweza kujaza mikutano katika Uchaguzi wa Urais mwaka 2015.

Binafsi ntamkumbuka sana kwa uthubutu wake wa kuweza kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu alipohusishwa na tuhuma za ufisadi.

Wewe utamkumbuka Lowassa kwa mambo gani?
Ufisadi wa Richmond amekufa pasipo kutoa siri ya Richmond ilikuwa niyanani kati ya Yeye na Mkwere.Lowassa nikati ya wanasiasa waliochangia umasikini kwa watanganyika kwa ufisadi wao na Mkwere,by Dk Slaa voice.
 
Habari Wadau,

Leo Februari 10, 2024 Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametangaza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mgombea Urais wa CHADEMA mwaka 2015 Edward Ngoyai Lowasa

Soma: Breaking News: - Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Katika mwaka enzi za uhai wake Mzee alipata kuwa na ushawishi Mkubwa nchini kiwango cha kuweza kujaza mikutano katika Uchaguzi wa Urais mwaka 2015.

Binafsi ntamkumbuka sana kwa uthubutu wake wa kuweza kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu alipohusishwa na tuhuma za ufisadi.

Wewe utamkumbuka Lowassa kwa mambo gani?
Alithubutu Kuvuta na kutumia Maji ya ziwa Victoria Mwanza , Shinyanga,Kahama,Nzega,Tabora ,Igunga.
 
Habari Wadau,

Leo Februari 10, 2024 Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametangaza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mgombea Urais wa CHADEMA mwaka 2015 Edward Ngoyai Lowasa

Soma: Breaking News: - Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Katika mwaka enzi za uhai wake Mzee alipata kuwa na ushawishi Mkubwa nchini kiwango cha kuweza kujaza mikutano katika Uchaguzi wa Urais mwaka 2015.

Binafsi ntamkumbuka sana kwa uthubutu wake wa kuweza kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu alipohusishwa na tuhuma za ufisadi.

Wewe utamkumbuka Lowassa kwa mambo gani?
kwa maamuzi magumu shule za kata
 
Hatotokea kiongozi yeyote tanzania akaachia nafasi kubwa kama hiyo kama lowasa alivyo fanya.

Aliwajibika kwa makosa ambayo hakufanya alionesha usomi na uelewa wa kiwango cha juu.

Nilimpigia kampeni ati nilitembea kata zote 19 kwa miguu kuwaelimisha wananchi kuhusu kwa nini aliachia cheo cha waziri mkuu.

Nyie zile pilikapilika za 2015 sio za kusahau.

1.Team lowassa
2. Team ulipo tupo

Lowassaaaaaaaa mabadiliko, mabadilikooooooooooooo lowasa.

Roho nyeupe, ngozi nyeupe, nywele nyeupe mapema asubuhi mpaka Ikulu.🤣

Bibi yangu mimi ilikuwa ni lazima apige kura sasa yeye alicho kuwa akijua ni ccm na nyerere,

Bibi yeye anasema atampigia kura wa chama cha nyerere, sasa tukachukuwa picha ya lowasa tukamuekeza kuwa lowasa ni mtoto wa nyerere, alivyoona zile nywele nyeupe akase, maaaaaaaawe anamfanana baba yake nyerere ona hizo nywele kweli nampigia kura🤣

Siku ya kupiga kura mapema vijana walishamfata na pikipiki mpaka kituo cha kupigia kura, si hajui kusoma, alivyouliza bibi unampigia kura nani akasema wa chama cha nyerere🤣

Wakamuuliza unamjua picha yake? , si alisha oneshwa picha ya lowasa na nywele zake akawaonesha huyu hapa mwenye nywele nyeupe🤣 imeisha hiyo.
RIP BIBI YANGU
RIP LOWASSA
 
Namkumbuka kwa mambo mawili. Kudai uchumi wetu ni sawa na nyama ya kasungura kadogo, na kujiharishia jukwaani Chato.
 
2014 pale dodoma mlipo potezana mkawa kama mafungu ya nyanya mpaka mkaamua kujichagulia yoyote.
"tuna matumaini naye heeeee"
 
  • Kuwasimamia wakueugenzi n.k;
  • Huhamasisha na kusimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata;
Note: Kwa maoni yangu, hatijawahi kuwa na PM matata toka EL ajiuzulu.
Zama hizi hata mkuu wa mkoa anamvimbia PM hadharani. Dah!
 
Ni mtu wa watu, anaye pendwa na kila rika.

Ni miongoni mwa Mawaziri wakuu wafuatiliaji wa mambo kwa ukaribu ukimwacha Moringe. alikuwa ni mtu Mwenye akili kubwa ya kutafakari na kubuni mambo kwa masilahi ya wananchi.

Alikuwa hachelewi kuchukua hatua mara moja, asiye kuwa na nidhamu ya uoga bali heshima ya ukweli.

Pumzika kwa amani EL.
Daima tutakuombea.
 
Idadi ya nyumba na majengo aliyokuwa anamiliki mzee Lowassa ni mengi mno hata majengo mengine familia haitazikumbuka.
Familia poleni sana Kwa msiba mkubwa.
 
Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere itakuwa alikuwa Team Jakaya maana alishinikiza Lowassa ajitoe kwny mbio za Urais 1995 otherwise anarudisha kadi ya Chama
 
Back
Top Bottom