Utamu na Faida za Tende kwenye mwili wa binadamu

<span style="font-family: comic sans ms"><font size="3">Hakuna chakula kilichothibitishwa kuongeza nguvu ya kiume, huo ni uongo. Simple as that.</font></span>
<br />
<br />
unaota wewe,,,hebu soma vizuri hapo namba 7;simple like that
 
nimekuwa mdau wa kula tende muda mrefu. ninakula kama pipi hivi ninapokuwa natazama tv home.
naombeni nijue health benefits of eating tende.
 
zinasaidia sana digestion, pia kwa wajawazito zinasaidia sn kufungua nyonga, zina mafuta, wanga, sukari hvy ni nzuri sn
 
Ngoja wadau waje ku2pa mafaida yake coz mie pia ni mdau wa tende.
 
Utamu na Faida za Tende

Tende mbali ya utamu wake zina faida nyingi sana mwilini
Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana mwezi wa ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Zijue faida zake. Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee.

Kwa leo tutazielezea baadhi ya faida za tende mwilini:

1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
Haya Waislam Wanaofunga wakati wa kufuturu kuleni sana Tende.

Chanzo MziziMkavu https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/71336-utamu-na-faida-za-tende.html
 
jamani ni lotion gani nzuri hasa kwa ngozi yenye mafuta mengi
Here are Some of the Best Body Lotions:
(note – most of them are drugstore, because I don’t see why you should spend more money than you need to, unless you really want to.)Vaseline Deep Condition Cocoa Butter Lotion – Cocoa butter helps to even skin tone and it gives skin a slight glow. Plus, cocoa butter is a very moisturizing ingredient, combine this with petroleum and you have a double whammy. This is my

favorite everyday lotion right now. It is very light, yet moisturizing, and it doesn’t leave the skin greasy. In fact, the Vaseline lotion line is great for people who hate lotion. Vaseline also makes this in a cream as well, which is perfect after a long relaxing bath or during the winter months. It will make you feel like you just went to the spa.

Au chagua hapa mojawapo kati ya hizi bonyeza hapa
13 BEST DRUGSTORE BODY LOTIONS 13 Best Drugstore Body Lotions
 
Nakumbuka Mwaka 2006 nlikua Udsm. Ghafla nikawa nasikia maumivu makali ya tumbo, kila nnavofanya bado, nikila chakula ndo linazidi linakuwa kama linawaka moto.

Nikaenda hospitali nikaambiwa nina gesi nikapewa vidonge, lakini bado hali ikazidi kuwa mbaya. Nakumbuka kuna siku nilienda haja nikatoka kinyesi cha kushangaza mno. Ikabdi nichukue simu yangu nikakipiga picha na kwenda nacho hospitali.

Daktari alipokiona akaniambia itakua nina vidonda vya tumbo na tena vinableed tumboni.

Basi nikaogopa hata kula kwani wali au chipsi au hata ugali vilikua vinanipa shida sana.

Kama bahati tu kuna jamaa alikua anauza tende na maziwa Msaud. Kwa vile njaa ilikua imenishika na sikujua nile nn, nikaamua ninunue tende pakti moja na maziwa glasi moja.

Amini usiamini siku ileile nikapata nafuu kubwa, basi ikawa kila nikisikia maumivu au njaa nakula kokwa moja. Kwa muda wa kama wiki moja nilikua sili kitu chengine chochote.

Mwishowe yale maumivu yakaondoka kabisa na hata hali yangu ya kiafya ikaimarika mno.
 
shukrani nimejifunza kitu zamani nilidhani menu za kiarabu.
 
zinasaidia sana digestion, pia kwa wajawazito zinasaidia sn kufungua nyonga, zina mafuta, wanga, sukari hvy ni nzuri sn

Hebu tufafanulie, ki namna gani zinafungua nyonga, nachelea kuita hizi ni hadithi za kufikirika. Njoo na hoja ya kisayansi ama maelezo yaliyoshiba.

Mwana JF waweza hesabu kuwa huo na ni uchafu, tupa kule ikiwa Angel Msoffe hatoweza kuitete hoja yake.
 
Unaposema nicotinic, una maana gani? Definition yake; nicotinic /nic·o·tin·ic/ (nik&#8243;o-tin´ik) denoting the effect of nicotine and other drugs in initially stimulating and subsequently, in high doses, inhibiting neural impulses at autonomic ganglia and the neuromuscular junction.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.
Mkuu hebu tufafanulie vizuri, moyo unaimarishwa ki namna gani? Ninachojua ni nkuwa moyo" huundwa" na misuli ya moyo, mishipa ya damu, neva za fahamu na kiwambo chembamba kikiufunika kwa nje. Sasa ni nini kilichopo katika tende kinachoimarisha moyo; ama nini kinaimarisha sehemu gani ya moyo.

3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.
Hili nalo linaleta kizungumkuti. Kama tende pekee ingekuwa inasaidia kupata hizo nguvu na stamina kwanini isilowekwe kwenye maji peke yake au kumung'unywa halafu ikupe matokeo uliyoyasema? Kwanini tusifikiri kuwa hizo nguvu zinatokana na maziwa ya mbuzi ama asali?. Maana hata maziwa halisi ya ng'ombe tunajua yanampatia mtu nguvu.
Jambo linalozidisha vurugu kwa kichwa ni hilo la kuibandika asali halafu hutaki kuipa sifa yake bali umekimbilia kwenye tende. Tunajua na imethibitishwa kuwa asali ina-free glucose, hivyo unapoila jua unapata free glucose, ikimaanisha haihitaji digestion.(Kumbuka end products of digestion of carbohydrates ni glucose that has to absorbed and later be assimilated by the body)

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.
Hapa tunadanganyana kweupe. Ili mwanamke ajifungue anahitaji sana misuli ya mji wa mimba (uterine muscles) ibane ile mtoto aweze kutoka tena ikisaidiana na misuli ya tumbo, wewe unaleta habari ya ajabu sana.Basi kuna haja gani ya kuwapatia wakina mama pitocin, ikiwa tunahitaji misuli ya mji wa uzazi/mimba ilegee ndipo ajifungue? Kuna umuhimu gani wa kuwataka wakina mama wajawazito wafanye mazoezi? Nani analiyekwambia ili damu isitoke sana basi misuli na itanuke,isibane?

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.
Mwanzoni, umetueleza nini kimo/kipo ndani ya tende. Ili kiwe chakula cha kupewa hadi uliyoitaja hapo juu utusaidie kwa kutuonyesha food value, its contents, in percentage.
Kwa mtazamo wangu, sidhani kama tende yaweza fikia hata maharage, soya, ama mtama. Prove me wrong kwa kutupa taarifa sahihi.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.
Mmmh!! Sijui tunaweza tukafika, ila tukiwa tumechoka saaana.

7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.
Ni kilichopo ndani ya tende mpaka kikawa kina-retard ageing? Ni kipi kilichomo ndani ya tende kinachosaidia kuondosha mabaka yatokanayo na kuungua na jua?

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.
Mkuu, mbona unachanganya madesa kihivyo, hapo awali umesema tende lina vitu vinne, na sasa unachomekea cha tano kiaina. Tukueleweje?

9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.
Hapa sihitaji uthibitisho kwa kumtafuta mwalimu wangu wa Biology aliyenifundisha" Food Substances" katika topic ya Nutrition (as one the characteristic features of living organisms) wakati niko form II, bali nitakwenda kwa mwalimu wangu wa Sayansi Kimu wakati niko darasa la tatu. Hivi kweli vitamini ni chanzo cha nguvu ambayo pia inaitwa nishati? Vitamini B1 and B2,you are so lucky to honoured that you are also the source of energy to liver. Oh My God!!

Mzizimkavu, hebu tufafanulie hoja nilizoziweka katika mfumo wa maswali ili isioneka ulichokileta hapa ni upupu.
 
Tender ina iron, hence helps kuzidisha damu..
Madhara, too much of it...welcomes diabetes, so watch out.
 
Tender ina iron, hence helps kuzidisha damu..
Madhara, too much of it...welcomes diabetes, so watch out.

Yes, too much of anything is harmful. However, if I'm going to eat 1/2 a tin of tende, am I prone to get diabete?
 
Shukrani kwa ma news mliyoyatoa na mwaka ujao iwe hivi hivi.
 
Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta?.
Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana Mwezi wa Ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu.

Ebu zijue faida zake.
Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee.

Baadhi ya faida zake mwilini ni kama ifuatavyo;

1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…