Utandawazi (Globalization): Adui hatari wa Afrika asiyesemwa kwa undani madhara yake

Yeye bandiko lake lote linataka tuwe na chama kimoja, halafu rais awe Magufuli! Msingi wa bandiko lote refu ni hapo. Anataka kuhalalisha ccm kupita bila kupingwa kwa kigezo cha kwamba tumejitambua, na vyama vingi vililetwa na wazungu ili kututawala. Halafu anajiita msomi. Nyuzi hizi za kutaka chama kimoja zimeanza kuwa nyingi sana hapa jukwaani, na wote wanataka chama kibaki ccm, na rais awe Magufuli!
Kwani hutaki watanzania kusupport rais wao ambaye analeta maendeleo na yanaonekana tena kwa kasi kubwa?
 
Niongelee moja la viwanda kwenye mada yako hafifu;
1.Wakati wakoloni wanakuja walikuta mna kiwanda chochote.
2.Viwanda walivyoanzisha wazungu unasema waliviua hao hao wazungu, huu uongo umeutunga kwa faida ya chama au faida yako binafsi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Utachekwa wewe, kama hujui kitu usiseme kitu!!. Viwanda vilivyokufa vya Mutex na vingine vilijengwa na wazungu?. Shame on you poor guy
 
Kwani hutaki watanzania kusupport rais wao ambaye analeta maendeleo na yanaonekana tena kwa kasi kubwa?

Kuna tofauti kubwa ya kumsupport na kushurutisha watu kumsupport. Kwenye uchaguzi ndio mtu hupata support, lakini ukiona kwenye uchaguzi kunafanyika ukatili na uzandiki wa wazi ili yeye na chama chake watawale hiyo haikubaliki. Hakuna maendeleo yoyote ya ajabu aliyoyaleta mpaka apate uhalali wa kuua mfumo wa vyama vingi, au kuhatarisha demokrasia yetu. Ogopa mtu anayeua mfumo wa ushindani na kuleta Monopoly kwenye kuongoza nchi. Magufuli angeweza kuwa rais mzuri kwenye karne iliyopita, ila sio kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia. Mbinu zake za kuongoza nchi ni zile outdated ambazo zitaishia kuliingiza taifa hili kwenye madeni, na kuitenga nchi yetu na dunia kwa kukwepa kuwa muwazi na kuhojiwa.
 
Wakihoji kuhusu demokrasia,uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa kuongea,haki za binadamu n.k mna waita mabeberu...

Ila wakiwapa hela za mikopo na ufadhili mbalimbali kama ujenzi wa vyoo vya shule..mnawaita wawekezaji na wadau wa maendeleo.

Akili kumkichwa.
#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha lazima waitwe mabeberu kwa sababu vitendo hivyo vyote kwao vipo lakini mbona hatuwahoji...au kwa sababu sisi ni wachanga haturuhusiwi kuwahoji...jomba..Trump juzi kaua kamanda wa iran, mbona mmekaa kimya hamuhoji..huo sio uvunjaji wa haki za binadamu au ni aina mpya ya demokrasia jomba..embu jibu haya ili tuendelee na mazungumzo...Trump alituambia waafrila ni shitholes, tumekaa kimyaaaa hatuhoji...why...ni upumbavvv....hivi.wewe unaonaje haya
 
So are you fit to survive?
Mimi silalalamiki napambana hata hao mabeberu wananiheshimu, kwa kuwa wanajua Niko vizuri upstairs

Tuwekeze kwenye elimu bora tuwakomboe watoto wetu ili wapambane na dunia.
Huu ujinga mnahubiri sijui elimu Bure ni takataka tu.

Hayo mavitu unaandika ni outdated watu kwenye akili watakucheka bro.
 
Ndugu zangu poleni na majukumu. Leo nimeona tukumbushane jambo muhimu la kuliewa sote Waafrika.

Nimeona tujikumbushe ni wapi wakubwa wa dunia wanatupeleka sisi tuitwao dunia ya tatu. Ni kwamba kuanzia karne ya 14 hadi 16 huko Ulaya tayari vijitaifa (nation states) vilikuwa vimeanza kupata nguvu za kidola na kiuchumi.

Hivyo kwasababu ya ubabe, matumizi ya nguvu kujitanua kidola kuliibuka vita kubwa sana iliyopiganwa kwa takribani miaka 30 huku vita hiyo.kwa upande mwingine ikibebwa na imani ya katoliki dhidi ya waasi wake walioongozwa na Martin Luther.

Mwaka 1648 Uliitishwa mkutano wa amani uitwao Westphalia ambapo vijistate hivyo vilikubaliana mambo kadhaa ikiwemo kusitisha vita na kila mmoja kuheshimu mipaka ya mwingine na kamwe kutoingilia uhuru wa.maswala ya ndani ya nchi mwingine (sovereignty).

Baada ya hapo uchumi wao ulikua sana na kuka wa na hitaji la masoko na wafanyakazi wenye gharama nafuu wa viwandani na mashambani.

Mwaka 1884/1885 waliitana wakubwa hao chini ya Chancellor wa Ujerman Bismack wakatugawana sisi waafrika kwaajili ya kututawala na kupata malighafi za viwanda vyao na nguvu kazi isiyo na gharama.

Hapo ndipo dhana ya utandawazi (globalization ) ilipoanza. Waafrika tulinyonywa sana hadi damu wakati huo. Babu zetu walichukuliwa kwwnda kutumikishwa Ulaya na Amerika.

Kwa mchango wa nguvu kazi za babu zetu na wizi wa malighafi na rasilimali zetu waliweza kuendeleza nchi zao kwa kujenga mifumo imara ya mitaji na faida kwaajili ya maendelwo zaidi.

Ukoloni ulipokwisha miaka ya 1960 wakubwa hao walikaa tena miaka ya 1980 wakasema lazima tuurudishe ukoloni Afrika tena kutokana na kunogewa na wizi na uporaji.

Walikuja na mpango wa marekebisho ya kimfumo (Structural Adjustment Program- SAP) ukiwa ni.mpango uliolenga kuuzima mpango kababmbe wa waafrika kudai marekebisho mapya ya mfumo wa uchumi duniani (New International Economic Order) ambao uliitaka jumuiya ya kimataifa kurekebisha mifumo nyonyaji ya kibiashara kupitia WTO, IMF na WB ili waafrika nao wawe na mazingira sawa ya ushindani wa kibiashara na kiuchumi.

Hivyo SAP ililazimisha waafrika kuhurisha mifumo yao yankiuchumi (liberalozation of economy) kwa kuruhusu masoko huria (free markets) na mfumo wa siasa za vyama vingi.

Wakubwa hao walijua fika kuwa waafrika hatuna uwezo wa kufanya investments kubwa hivyo kwa uhuria huo wa.masoko ungewapa nafasi wao kutawala biashara na shughuli zingine za kiuchumi Afrika.

Aidha kupitia mifumo ya vyama vingi vya siasa walijua kuwa tutagawanyika na hivyo watatutawala kirahisi kupia vyombo vyake vyankinyonyaji vya IMF, WTO na WB. Baada ya kufanikiwa katika maeneo hayo tunashuhudia Afrika ikiwa na migogoro mingi ya kisiasa huku wao wakiendelea kuchota rasilimali zetu kilaini kabisa.

Viwanda vingi vilivyoanzishwa wakati wa mwanzo baada ya uhuru katika nchi.nyingi za Afrika vimekufa si kwasababu nyingine bali kwa mikono ya wakubwa hao kutotaka tupate mifumo imara ya kiuchumi ya kututoa huku tuliko.

Ndugu zangu utandawazi kwa maana halisi si kama watu mnavyoutafsiri kirahisirahisi, huo ni ukoloni kabisa unaotumia nyenzo na vyombo vya kimataifa kuinyonya Afrika.

Madeni makubwa ya nchi za Afrika ambayo yanadaiwa na WB yanatengenezwa kimkakati (si rahisi nikaeleweka hapa) ili nchi za Afrika ziendelee kuwa tegemezi.

Hivyo kwa picha hiyo, ni vema tuelewe malengo ya wazungu kwetu sisi waafrika kuwa siyo.mazuri. Na ni vema mkajua kuwa.wakubwa hao hawapendi.kusikia nchi masikini zinajitambua na kuanza kupambana kujikomboa.

Tanzania ilipo sasa imejitambua na hongera sana Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kuutambua ulaghai wa wakubwa hao na hivyo kuamua kwa dhati kuikomboa Tanzania.

Kelele unazopigiwa kuhusu madai ya udikteta na kujaribu kukuharibia taswira ili uchukiwe na wananchi wako ili mwishowe wao wajihalalishie kukutoa madarakani.

Ninakuomba, simama imara kwani Watanzania wenye akili kama mimi tuko wengi na tunakuunga mkono. Unapoipeleka Tanzania kila mwenye akili timamu anaona.

Kasi ya maendeleo si ya kuridhisha kama tulivyozoea kuimbiwa bali wakati huu kasi ni kubwa kiasi inawatisha wakubwa hao. Pigana Jemedari tuko nyuma yako.

Watanzania wote niwaombe tumuunge mkono Rais wetu na tusikubali kwa namna yoyote adhalilishwe na manyang'au na.majizi. Tumuombee aongoze ukombozi wa kweli.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa. Siku si nyingi Afrika itahesabiwa haki na hao wanaotutawala na kutunyonya na kututesa. Mungu amewaandalia mahali pao stahiki.

Unalaumu globalization kwa your incompetence to compete and guard your own country?

Yaani unalaumu mashindano kwa uzembe wako wa ******* wa kutokushindana?

Your weakness is yours,dont blame the game,blame yourself for your own weaknesses and incompetencies!

Bure kabisa!
 
hahaha lazima waitwe mabeberu kwa sababu vitendo hivyo vyote kwao vipo lakini mbona hatuwahoji...au kwa sababu sisi ni wachanga haturuhusiwi kuwahoji...jomba..Trump juzi kaua kamanda wa iran, mbona mmekaa kimya hamuhoji..huo sio uvunjaji wa haki za binadamu au ni aina mpya ya demokrasia jomba..embu jibu haya ili tuendelee na mazungumzo...Trump alituambia waafrila ni shitholes, tumekaa kimyaaaa hatuhoji...why...ni upumbavvv....hivi.wewe unaonaje haya

Sisi tunahoji watanzania wenzetu wanapofanyiwa ukatili na kunyimwa haki zao za kibinadamu. Ingekuwa Trump kaja hapa nchini tungemuhoji kupata wapi hayo mamlaka ya kutunyima haki yetu. Huyo Trump aliposema kuwa nchi zetu ni shithole countries alimaanisha viongozi wetu, na alikuwa sahihi. Hatumpingi eti kwakuwa ni mzungu, bali tunaangalia tunampinga kwa kipi.
 
Kuna tofauti kubwa ya kumsupport na kushurutisha watu kumsupport. Kwenye uchaguzi ndio mtu hupata support, lakini ukiona kwenye uchaguzi kunafanyika ukatili na uzandiki wa wazi ili yeye na chama chake watawale hiyo haikubaliki. Hakuna maendeleo yoyote ya ajabu aliyoyaleta mpaka apate uhalali wa kuua mfumo wa vyama vingi, au kuhatarisha demokrasia yetu. Ogopa mtu anayeua mfumo wa ushindani na kuleta Monopoly kwenye kuongoza nchi. Magufuli angeweza kuwa rais mzuri kwenye karne iliyopita, ila sio kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia. Mbinu zake za kuongoza nchi ni zile outdated ambazo zitaishia kuliingiza taifa hili kwenye madeni, na kuitenga nchi yetu na dunia kwa kukwepa kuwa muwazi na kuhojiwa.
hahahaah jomba hivi wewe una akili kweli..Magufuli ameua mfumo wa vyama vingi kwa vipi...unazungumzia mfumo huu ambao umejaa mafisadi wa kula pesa tu wao na familia zao au mfumo upi...hahahah..rejea report ya CAG, au Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo ilisema mabilioni mangapi hayajulikani yalipo kutoka vyama vyenu hivyo, chademaa, ACT etc...hahaha huo ndio mfumo unaouzungumzia au..excuse me...mbona hamhoji hayo mapesa yameenda wapi...mnajifanya hamuoni..st.up.iddd..msitufanye wote hatuna akili..jomba. haya unazungumzia madeni gani hayo ambayo nchi itaingia...serikali hii ambayo imeweza kukusanya kodi na kununua madege ya mabilioni kwa cash..ndio unasema italeta madeni...hahahah..hivi unajua tuna madeni tangu enzi za uhuru..na yanalipwa sasa...sijui unajua...hivi unajua serikali hii imekwisha lipa madeni ya kiasi gani ndani ya miaka hii minne tangu iingie madarakani..na madeni yapi yamelipwa...unajua msizungumze kwa kubwabwaja bila tafiti yoyote jomba.hata kama umetumwa lakini tumia pia na akili yako ya kuzaliwa..au hukuzaliwa na akili jomba....kalagabaho..
 
Kwani hutaki watanzania kusupport rais wao ambaye analeta maendeleo na yanaonekana tena kwa kasi kubwa?
Unaandika Ujinga tu. Maendeleo mnayosema mnayaona kwa kutumia darubin gani?
Bado tunahitaji ushindani wa Sera ili aje mwingine afanye zaidi ya huyu aliyepo sasa,
 
Sisi tunahoji watanzania wenzetu wanapofanyiwa ukatili na kunyimwa haki zao za kibinadamu. Ingekuwa Trump kaja hapa nchini tungemuhoji kupata wapi hayo mamlaka ya kutunyima haki yetu. Huyo Trump aliposema kuwa nchi zetu ni shithole countries alimaanisha viongozi wetu, na alikuwa sahihi. Hatumpingi eti kwakuwa ni mzungu, bali tunaangalia tunampinga kwa kipi.
jomba sijakuelewa..majibu yako..ulizungunzia mabeberu wakituhoji kuhusu ukiukaji wa haki sijui nini tunawaita mabeberu..nikasema mbona sisi hatuwahoji kwa matendo yao wanayofanya nikiyotaja mifano...why for them its ok..wakati nao kama ni matendo ya hovyo ndio wanaongoza..tell us
 
hahahaah jomba hivi wewe una akili kweli..Magufuli ameua mfumo wa vyama vingi kwa vipi...unazungumzia mfumo huu ambao umejaa mafisadi wa kula pesa tu wao na familia zao au mfumo upi...hahahah..rejea report ya CAG, au Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo ilisema mabilioni mangapi hayajulikani yalipo kutoka vyama vyenu hivyo, chademaa, ACT etc...hahaha huo ndio mfumo unaouzungumzia au..excuse me...mbona hamhoji hayo mapesa yameenda wapi...mnajifanya hamuoni..st.up.iddd..msitufanye wote hatuna akili..jomba. haya unazungumzia madeni gani hayo ambayo nchi itaingia...serikali hii ambayo imeweza kukusanya kodi na kununua madege ya mabilioni kwa cash..ndio unasema italeta madeni...hahahah..hivi unajua tuna madeni tangu enzi za uhuru..na yanalipwa sasa...sijui unajua...hivi unajua serikali hii imekwisha lipa madeni ya kiasi gani ndani ya miaka hii minne tangu iingie madarakani..na madeni yapi yamelipwa...unajua msizungumze kwa kubwabwaja bila tafiti yoyote jomba.hata kama umetumwa lakini tumia pia na akili yako ya kuzaliwa..au hukuzaliwa na akili jomba....kalagabaho..

Kama ni ripoti ya CAG kuanzia ccm mpaka vyama vingine vinaonyesha hati chafu, tena ccm ikiongoza, mbona huhoji huko? Kama serikali inalipa madeni mbona hayapungui yanazidi tena kwa kasi kuliko ilivyokuwa huko nyuma? Weka ilikuta deni kiasi gani na imelipa kiasi gani. Kununua madege kwa cash ni ulimbukeni wala sio dalili kuwa hali ni nzuri. Kwani wote walionunua magari hapa mjini ni dalili kuwa mambo yao ni mazuri?
 
hahahaah jomba hivi wewe una akili kweli..Magufuli ameua mfumo wa vyama vingi kwa vipi...unazungumzia mfumo huu ambao umejaa mafisadi wa kula pesa tu wao na familia zao au mfumo upi...hahahah..rejea report ya CAG, au Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo ilisema mabilioni mangapi hayajulikani yalipo kutoka vyama vyenu hivyo, chademaa, ACT etc...hahaha huo ndio mfumo unaouzungumzia au..excuse me...mbona hamhoji hayo mapesa yameenda wapi...mnajifanya hamuoni..st.up.iddd..msitufanye wote hatuna akili..jomba. haya unazungumzia madeni gani hayo ambayo nchi itaingia...serikali hii ambayo imeweza kukusanya kodi na kununua madege ya mabilioni kwa cash..ndio unasema italeta madeni...hahahah..hivi unajua tuna madeni tangu enzi za uhuru..na yanalipwa sasa...sijui unajua...hivi unajua serikali hii imekwisha lipa madeni ya kiasi gani ndani ya miaka hii minne tangu iingie madarakani..na madeni yapi yamelipwa...unajua msizungumze kwa kubwabwaja bila tafiti yoyote jomba.hata kama umetumwa lakini tumia pia na akili yako ya kuzaliwa..au hukuzaliwa na akili jomba....kalagabaho..
CAG huyu huyu aliyeibua upotevu wa sh. Tril. 2.4 akaishia kufukuzwa

Kama unaamini ripoti za GAG ungekuwa wa kwanza kumwambia raisi ajiuzuru

Ni CAG huyu aliripoti kuwa matumizi zaidi ya bil. 600 hayakufuata sheria ya manunuzi,

Alafu unashabikia ujinga
 
Unaandika Ujinga tu. Maendeleo mnayosema mnayaona kwa kutumia darubin gani?
Bado tunahitaji ushindani wa Sera ili aje mwingine afanye zaidi ya huyu aliyepo sasa,
yupi sasa mwenye sera unayoijua..huyo mwingine.acha ujinga wa kukariri maisha. huyo ynayemtegemea atafanya zaidi ni nani uliye muandaa..asilimia karibu 50 ya viongozi wa upinzani wameenda kum support.Magufuli..sijui unalijua hilo..ni kwanini unadhani..sasa waliobaki wako wapi. tueleze...tuache ujinga wa kufanya experiment ya kujenga uchumi...hao wenye sera mbadala CAG anawadai mabilioni ya pesa ambayo hayajulikani yalipo...yaani yameliwaaa upo.! jitambue jomba
 
CAG huyu huyu aliyeibua upotevu wa sh. Tril. 2.4 akaishia kufukuzwa

Kama unaamini ripoti za GAG ungekuwa wa kwanza kumwambia raisi ajiuzuru

Ni CAG huyu aliripoti kuwa matumizi zaidi ya bil. 600 hayakufuata sheria ya manunuzi,

Alafu unashabikia ujinga
CAG aliibua mabilioni mangapi yameliwa kwenu upinzani..mbona hili unalikwepa..jibu na hili basi maana naona una ushabiki wa kizandiki
 
hivi CAG alifukuzwa...embu tujuze
 
jomba sijakuelewa..majibu yako..ulizungunzia mabeberu wakituhoji kuhusu ukiukaji wa haki sijui nini tunawaita mabeberu..nikasema mbona sisi hatuwahoji kwa matendo yao wanayofanya nikiyotaja mifano...why for them its ok..wakati nao kama ni matendo ya hovyo ndio wanaongoza..tell us

Sisi hatuna platform ya kuwahoji US ila tunahoji hapa nchini kwetu huu uhayawani mnaofanya. Nyinyi mtawahoji US kwa usafi gani mlionao, na wala hawajawakataza kuhoji, mnaweza kuwahoji hata leo mkitaka. Hao US hawawajibiki kwetu wala hao wanaofanyiziwa hawatuhusu. Siku wakitufanyia sisi matendo ya hovyo tutawahoji kama tunavyowahoji nyinyi hivi sasa.
 
yupi sasa mwenye sera unayoijua..huyo mwingine.acha ujinga wa kukariri maisha. huyo ynayemtegemea atafanya zaidi ni nani uliye muandaa..asilimia karibu 50 ya viongozi wa upinzani wameenda kum support.Magufuli..sijui unalijua hilo..ni kwanini unadhani..sasa waliobaki wako wapi. tueleze...tuache ujinga wa kufanya experiment ya kujenga uchumi...hao wenye sera mbadala CAG anawadai mabilioni ya pesa ambayo hayajulikani yalipo...yaani yameliwaaa upo.! jitambue jomba
Kama hakuna mbona hamtaki siasa za ushindani ili wajitokeze wanaoweza kumchallenge huyo Mungu MTU wenu.
 
CAG aliibua mabilioni mangapi yameliwa kwenu upinzani..mbona hili unalikwepa..jibu na hili basi maana naona una ushabiki wa kizandiki

Sheria ziko wazi, chama kimekula hela kuna taratibu za kuchukuliwa, ni wapi hela zimeliwa kwenye chama cha upinzani tukaja kuwasifia hapa jukwaani?
 
Back
Top Bottom