Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Mimi mwenyewe Mkulungwa mzee.

Sio rahisi kuniingia kwa sababu ninatabia ya kuendesha mazungumzo, nipo huru mkuu.

Nimeshazungula DSM yote, Arusha, Mbeya, Mwanza, Moro,
Unajigamba mtandaoni ili watu wakuone mjanja wa mjini, lakini unaweza kuta wewe umetapeliwa sana tu na wenye akili nyingi.
 
Wengi sana wameuziwa sabuni, binafsi hiyo miaka ya 2005- 2010 jamaa ninaowafahamu waliuziwa miche ya sabuni
 
Wengi sana wameuziwa sabuni, binafsi hiyo miaka ya 2005- 2010 jamaa ninaowafahamu waliuziwa miche ya sabuni
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?
 
Msowero, Mvumi, Rudewa, Kilosa, Mkambarani, n.k. huko ndiko machimbo ya magenius STD 7, haataarii!
Hapo Msowero wanaitwa MALEBANONI!

Everyday is Saturday.............................. 😎
Geniuos ni yule tu anayemudu maisha yake na ya ndugu zake kwa hali zote... Sasa tukianza kuwaita vibaka mageneous tunakuwa tunakosea heshima mageneous wa heshima... Bora uwe mwizi wa mabilioni huko kwenye mabenki tukujue uko smart upstairs ila mwizi wa simu naye Biig No..
 
Mwizi ni mwizi tu, kabla ya hackers walikuwepo na watakuwepo wezi wasiotumia nguvu wala silaha, wanatumia akili, saikolojia...hawa wangesoma wangekuwa kina SNOWDEN. Sema Bongo bahati mbaya!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?
Hivyo vijiji ni notorious kwa sisi wakulima wa WhatsApp! Na watafuta shamba...

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Siwezi tapeliwa Mimi wewe. Mimi mwenyewe tapeli.

Utaniibia kwa kunikaba lakini sio ujanja wowote wa akili yako
NINARUDIA TENA:

Unajigamba mtandaoni ili watu wakuone mjanja wa mjini, lakini unaweza kuta wewe umetapeliwa sana tu na wenye akili nyingi.
 
Nakazia
 

Wewe unaenda kariakoo kuna maduka ya simu, alafu unanunulia nje ya duka barabarani alafu ukiibiwa useme aliyekuibia anaakili, wewe kama sio mjinga ni nani?

Yaani utoke home, unajua kabisa unaenda kununua simu aina Fulani, tayari ushajua bei yake kabla hujafika. Unafika unazuzuliwa kipuuzi na wapuuzi alafu kwa upuuzi wako unawaona wanaakili, wewe si mpumbavu tuu.

Wewe unaenda kukata tiketi, unajua kabisa nauli ya mwanza ni 40- 50. Unafika ubungo, ati Sarange(mpiga debe) anakudandia anakuambia unaenda wapi, nawe unajibu. Kisha anakuambia nauli 60 magari yamejaa. nakujaza upepo huku akikuvuta Vita atakavyo, nawe kwa vile hamnazo, hujiamini unatoa pesa.
Badala ufike ofisi ya gari husika, kama nauli ipo juu nenda ofisi ingine, mpaka utakapopata yenye nauli halali.

Wengi wanaoibiwa hawajiamini, wanatamaa alafu akili zao ni zero.

Utanunuaje kitu ambacho hujui bei yake?
Yaani utoke home unaenda kununua simu usiyoijua bei?

Mkuu kuibiwa ni ushamba,

Nashukuru wewe umenielewa
 
Mbona unang'ang'ania sana wizi na utapeli wakati mimi nimetumia tu kama mfano wa kuwaeleza watu wenye akili nyingi licha ya kwamba hawajasoma sana.

Mbona hauongelei wanasiasa, wachezaji, wahubiri, wachambuzi unakazania utapeli tu na wizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…