Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Mimi mwenyewe Mkulungwa mzee.

Sio rahisi kuniingia kwa sababu ninatabia ya kuendesha mazungumzo, nipo huru mkuu.

Nimeshazungula DSM yote, Arusha, Mbeya, Mwanza, Moro,
Unajigamba mtandaoni ili watu wakuone mjanja wa mjini, lakini unaweza kuta wewe umetapeliwa sana tu na wenye akili nyingi.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la (7) tu kwa sababu ya umasikini wa nyumbani kwao wakashindwa kuendelea na masomo.

Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku, na kwa namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.

Wewe jenga picha wale wezi wa pale kariakoo wanakuibia mfukoni bila hata wewe kujua kama kuna mkono umeingia ndani ya mfuko wako wa suruali na kuchukua pesa yako ya dagaa. Zile ni akili nyingi sana sema tu zimeelekezwa pahala pasipo stahili.

KISA KIDOGO CHA MIMI KUUZIWA KIPANDE CHA SABUNI KWA 20,000/= NIKIDHANIA NI SIMU

================

Nikiwa kidato cha 6 miaka hiyo ya 2000 na kitu, niliahi kuuziwa kipande kidogo cha sabuni nikidhani kuwa ni simu. Nilikuwa ninatoka Tabata Segerea nyumbani mama yangu mkubwa nilienda kumtembelea siku ya ijumaa jioni sasa nikawa ninarudi jumapili mchana ili nifanye maandalizi ya usafi wa nguo kwa ajili ya shule kesho yake ambayo ni Jumatatu.

Baada ya kushuka kutoka katika daladala pale mtaa wa Kongo akatokea jamaa mmoja rika langu akiwa ameshika simu aina ya nokia zile za jeneza za zamani akawa ananioneshea kwa ukaribu basi mimi nikaichukua ile simu nikaikagua vema kisha nikamuuliza bei gani, yeye akasema ni 20,000/=. Nikasema kimoyomoyo poa ngoja nichukue hii ngoma ili na mimi nikatambe huko mitaani.

Alafu hiyo pesa yenyewe sasa ndio nilikuwa nimepewa kama pocket money ya mwezi mzima na huyo mama yangu mkubwa. Yule jamaa rika langu kabisa akaniambia mwamba njoo huko hapo barabarani sana, basi mimi nikaenda, akanipa tena simu nikaikagua kwa mara ya pili, simu ipo sawa haina tatizo.

Sawa. Basi mwamba akaichukua simu akaiweka katika bahati fulani hivi ya kaki kisha na mimi nikampa pesa yake 20,000/= huyo nikaondoka. Kabla sijaenda mbali, baada ya kupanda daladala za kwenda home kwetu kurasini, nikaona ngoja nifungue bahasha nitoe simu yangu walau nicheze hata game la nyoka niji-keep busy, halooooo!

Nilikutana na kipande cha sabuni ya kodrai hahahahahaaaaa size ile ile kama simu ya Nokia ya jeneza (3310) kikiwa kinaniangalia tu. Kwa kweli roho iliniuma sana.

Ukizingatia 20,000/= ni pesa nyingi sana kwa miaka ile alafu mimi bado mwanafunzi sina majukumu mengi. Basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia hasira nilizokuwa nazo na nilipofika home nikafua nguo zangu kwa kutumia sabuni ya kipande ya 20,000/= hahahahaaaaa.

Kuna watu wenye akili nyingi lakini hawajasoma sana hususan huko vijijini. Unakuta mwanakijiji yeye hawajawahi kuwa na njaa bomani kwake. Miaka yote anavuna mahindi mengi, anafuga ng'ombe wake vizuri na anasomesha watoto kwa kuuza maziwa tu mpaka watoto wanamaliza form six. Siku akiamua kukuandikia barua, huo muandiko wake utadhani labda ni mwalimu wa secondary.

Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wengi sana wameuziwa sabuni, binafsi hiyo miaka ya 2005- 2010 jamaa ninaowafahamu waliuziwa miche ya sabuni
 
Wengi sana wameuziwa sabuni, binafsi hiyo miaka ya 2005- 2010 jamaa ninaowafahamu waliuziwa miche ya sabuni
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?
 
Msowero, Mvumi, Rudewa, Kilosa, Mkambarani, n.k. huko ndiko machimbo ya magenius STD 7, haataarii!
Hapo Msowero wanaitwa MALEBANONI!

Everyday is Saturday.............................. 😎
Geniuos ni yule tu anayemudu maisha yake na ya ndugu zake kwa hali zote... Sasa tukianza kuwaita vibaka mageneous tunakuwa tunakosea heshima mageneous wa heshima... Bora uwe mwizi wa mabilioni huko kwenye mabenki tukujue uko smart upstairs ila mwizi wa simu naye Biig No..
 
Mwizi ni mwizi tu, kabla ya hackers walikuwepo na watakuwepo wezi wasiotumia nguvu wala silaha, wanatumia akili, saikolojia...hawa wangesoma wangekuwa kina SNOWDEN. Sema Bongo bahati mbaya!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?
Hivyo vijiji ni notorious kwa sisi wakulima wa WhatsApp! Na watafuta shamba...

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Siwezi tapeliwa Mimi wewe. Mimi mwenyewe tapeli.

Utaniibia kwa kunikaba lakini sio ujanja wowote wa akili yako
NINARUDIA TENA:

Unajigamba mtandaoni ili watu wakuone mjanja wa mjini, lakini unaweza kuta wewe umetapeliwa sana tu na wenye akili nyingi.
 
Siwezi ibiwa na mtu aliyefeli shule hata siku moja.

Kwanza sipendi vitu vya bei nafuu.
Mbili nipo huru na pesa yangu, na sina tamaa.

Tatu, ninachokitaka ndio huwa, sina tabia ya kumsikiliza MTU. Mimi ni dikteta. Hunipeleki peleki.

Kabla sijanunua kitu nimeshafanya research.

Nikitembea huwezi nikaribia na kunigusa, utajuta.

Kuibiwa ni dalili ya ujinga. Kabla uniambie kufanyiwa ujambazi.

Lakini wizi kama wizi sidhani.

Usipende bwerere
Nakazia
 
Wewe unaenda kariakoo kuna maduka ya simu, alafu unanunulia nje ya duka barabarani alafu ukiibiwa useme aliyekuibia anaakili, wewe kama sio mjinga ni nani?

Yaani utoke home, unajua kabisa unaenda kununua simu aina Fulani, tayari ushajua bei yake kabla hujafika. Unafika unazuzuliwa kipuuzi na wapuuzi alafu kwa upuuzi wako unawaona wanaakili, wewe si mpumbavu tuu.

Wewe unaenda kukata tiketi, unajua kabisa nauli ya mwanza ni 40- 50. Unafika ubungo, ati Sarange(mpiga debe) anakudandia anakuambia unaenda wapi, nawe unajibu. Kisha anakuambia nauli 60 magari yamejaa. nakujaza upepo huku akikuvuta Vita atakavyo, nawe kwa vile hamnazo, hujiamini unatoa pesa.
Badala ufike ofisi ya gari husika, kama nauli ipo juu nenda ofisi ingine, mpaka utakapopata yenye nauli halali.

Wengi wanaoibiwa hawajiamini, wanatamaa alafu akili zao ni zero.

Utanunuaje kitu ambacho hujui bei yake?
Yaani utoke home unaenda kununua simu usiyoijua bei?

Mkuu kuibiwa ni ushamba,

Nashukuru wewe umenielewa
 
Mbona unang'ang'ania sana wizi na utapeli wakati mimi nimetumia tu kama mfano wa kuwaeleza watu wenye akili nyingi licha ya kwamba hawajasoma sana.

Mbona hauongelei wanasiasa, wachezaji, wahubiri, wachambuzi unakazania utapeli tu na wizi.
 
Back
Top Bottom