Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Trump sio "Policy Maker" yeye anatekeleza sera za nchi kama mwanasiasa na haundi sera.

Tena afadhali ungetolea mfano kwa nchi za Afrika na sio wanasiasa wa Ulaya. Hapa umekosea sana...


Donald Trump ingekuwa hachangii kuunda Sera hasingekuwa tofauti Na wenzake wakina jeb bush Na marepublicer wenzake, kiongozi yeyote anachangia sana kwenye msimamo wa serikali iliyopo madarakani, msimamo wa trump unachangia sana uelekeo wa marekani hata kama sio kati ya watu waliotunga Sera au ilani,

Msimamo wa magufuli sio sawa na kikwete hata kama ilani au Sera (policy) hakutunga yeye, kiongozi aliyeko madarakani ana ushawishi mkubwa sana wa kuielekeza nchi. Hata kuiba Na kupora. Ndio maana wengi wa wafanyabiashara matajiri wanakimbilia kwenye siasa Siku hizi ili mambo yao yaenda, Na huo ndio ukweli,
 
Sawa upo sahihi ni mwanasiasa tajiri.

Mwanasiasa ni mtekeleza sera na sio muunda sera (Policy Maker)...


Na sio lazima watekeleze kwa asilimia mia, matajiri wengi wanakimbilia siasa kwaajiri ya mambo yao yaende, kutekeleza Sera ni wajibu wakila kiongozi, kusukuma mambo yao ni agenda nyingine,

Utajiri Na siasa

Ujanja wa mtaani vs elimu ya darasani
 
Unatoa mifano mingi sana mbayo ipo nje kabisa ya mada mkuu. Yaaani hoja ya KUSOMA SANA vs UTAJIRI wewe umeigeuza kuwa SIASA vs UTAJIRI? Umenishangaza sana mkuu...


Hapana nimejibu hoja yako kwamba, kwanini waliosoma sana hawafanyi vizuri mtaani?!

Nikakujibu kuwa elimu ya darasani ni tofauti Na ujanja wa mtaani,

Nikakupa mfano wa matajiri wengi sio wasomi wakubwa kama maproffesors, Na maproffesors wengi sio matajiri wakubwa!

Ukasema maproffesors wengi ndio wako serikali wakiwapangia Sera matajiri,

Nikakujibu wako serikalini kwasababu wao ni wazuri kwakazi hizi za kuajiriwa, ujanja wao ni darasani ni wazuri kwa Kazi za collar job, sio wazuri kwa ujanja wa mtaani ili waweze kupata utajiri kama matajiri wengine, maana hakuna mtu anayetaka kuajiriwa tu maisha yake yote hasitake kuwa tajiri binafsi, ukasema matajiri wengi sio wanasiasa wazuri , nikakupa mfano wa Trump, Blomberg, shinawatra, belosconi, nk

Hapo ndio tulipofikia kwenye MATAJIRI VS SIASA
KUSOMA SANA VS UTAJIRI

Ni mwendelezo wa mada tu usiogope mkuu,,,
 
Mipango hupangwa na "Policy Makers" ambao wapo wizarani na Ikulu, hao jamaa sio wanasiasa hata kidogo. Wao ni wazalendo to the fullest...


Tunarudi kulekule mkuu,, kwamba waliopo Wizarani wanaweza kwenda kinyume Na wanasiasa ambao wanaiongoza serikali?!

Tunaongozwa Na ilani ya chama au watu wa Wizarani?!

Contradiction! Antagonistic!
 
Lakini utajiri wao unasimamiwa na wasomi wa kihivyo (Financial advisors). Si ndio?...


Sawa lakini kusimamia ni tofauti na kumiliki,,,

Kwani wao wasomi wanaosimamia huo utajiri, hawataki kuwa matajiri?!

Mbona hawana utajiri sasa?! Pamoja na usomi wao wote?!

Tunarudi kulekule elimu ya darasani ni tofauti na elimu ya mtaani (ujanja),
 
Ni kweli kabsa, halafu enzi hizo kuiba ilionekana kama sifa, mwizi anamwambia nimeichomoa kwa muhindi nawe unakubali kununua mali ya wizi kisa ni bei chee.
 
Sawa lakini kusimamia ni tofauti na kumiliki,,,

Kwani wao wasomi wanaosimamia huo utajiri, hawataki kuwa matajiri?!

Mbona hawana utajiri sasa?! Pamoja na usomi wao wote?!
Utajiri wanao ndani ya vichwa vyao mkuu...
 
Tunarudi kulekule mkuu,, kwamba waliopo Wizarani wanaweza kwenda kinyume Na wanasiasa ambao wanaiongoza serikali?!

Tunaongozwa Na ilani ya chama au watu wa Wizarani?!

Contradiction! Antagonistic!
Wanasiasa wanaandaa Ilani ya chama baada ya kupata muongozo kutoka kwa wataalam wa nyanja husika kama afya, uchumi, foreign policy, elimu, etc
 
Na sio lazima watekeleze kwa asilimia mia, matajiri wengi wanakimbilia siasa kwaajiri ya mambo yao yaende, kutekeleza Sera ni wajibu wakila kiongozi, kusukuma mambo yao ni agenda nyingine,
Hii sina uhakika nayo kwa maana moyo wa mtu ni kichaka kinene...
 
Trump hana msimamo, bali ule ni msimamo wa nchi. Kumbuka Rais ni taasisi na sio mtu mmoja kama Trump...
 
Lissu alikuwa anawatetea Mabeberu bungeni waendelee kuchimba madini yetu huku Rais Magufuli akitutetea sisi wanyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…