Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Zaidi ya mara moja, ni vile tu nimekuwa mvivu kuandika thread/comment ndefu.Je, ulishawahi kuwaona/kukutana na watu wana namna hii?
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zaidi ya mara moja, ni vile tu nimekuwa mvivu kuandika thread/comment ndefu.Je, ulishawahi kuwaona/kukutana na watu wana namna hii?
Sawa mkuu, nimekuelewa.Zaidi ya mara moja, ni vile tu nimekuwa mvivu kuandika thread/comment ndefu.
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Wale nao ni kiboko...Na ule wa dirishani unaupa asilimia ngapi?
Dah hii yako ni kibokoNa ule wa dirishani unaupa asilimia ngapi?
Kuna siku nilikua nimepanga ku-download windows sasa nikakumbuka offer ya ya usiki kutoka halotel yenye unlimited data
Majira ya usiku kama saa tisa hivi hapo speed imechanganya inaenda mpaka 5mbps ikanibidi nilale.
nikamuachia usukani brother yangu aendelee ku monitor si unajua sometimes network na servers zinazingua unakuta dowload files zina stop kwaiyo hapo itakubidi uwe karibu u-resume
Nilikua nime connect internet kwenye pc kupitia simu kwa njia ya wireless halafu ile simu nilikua nimeichomeka chaji kupitia usb port ya pc nikawa nimeiweka juu ya keybord, na pia kulikua na kisimu cha keypad cha tecno kilikua nacho nimekiweka hapo hapo kwenye keyboard
Nikajikuta nimestuka majira ya saa 11, kucheki internet signal naona alama ya ❌ Kuangalia pale kwenye keybord ya laptop sioni simu, naona usb cable inabembea chini bila simu
Nikaanza kuitafuta huku nikiwaza pengine itakua ilianguka chini lakini sikuweza kuipata. Hapo nikapata wazo la kuchukua simu ile ndogo ili niipige niskie itapoitia niichukue kiulaini, nashangaa nayo simu ndogo haipo.
Ikabidi nimuamshe bro tusaidiane maana ishu ishakua heavy, katika harakati za kutafuta tukafunua pazia tukaona kuna tobo kwenye wavu
Distance ya kutoka dirishani mpaka mezani ambapo tuliweka pc ilikua ni umbali wa futi 9 au kumi, na hapo ndipo nilipoamini kua hii kumkwepa mwizi ni ngumu.
Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku, na kwa namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.Siwezi ibiwa na mtu aliyefeli shule hata siku moja.
Kwanza sipendi vitu vya bei nafuu.
Mbili nipo huru na pesa yangu, na sina tamaa.
Tatu, ninachokitaka ndio huwa, sina tabia ya kumsikiliza MTU. Mimi ni dikteta. Hunipeleki peleki.
Kabla sijanunua kitu nimeshafanya research.
Nikitembea huwezi nikaribia na kunigusa, utajuta.
Kuibiwa ni dalili ya ujinga. Kabla uniambie kufanyiwa ujambazi.
Lakini wizi kama wizi sidhani.
Usipende bwerere
Sawa...Siwezi ibiwa na mtu aliyefeli shule hata siku moja.
Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sanaDah hii yako ni kiboko
Mbunge wenu ni MsukumaUsicheze na Sisi darasa la Saba nyie someni vyuo mkimaliza mje huku mtaani tuwaajiri
Bora huyo kuliko mrusha mate wa jalalaniMbunge wenu ni Msukuma
Hahahhahhhahahahh!bila kusahau tandale a.k.a mbingu A idete muhola minepa mavimba[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa jinsi ulivyo hivi wewe huwajui kabisa hawa wajuba, jichanganye nao ndo uje utuambie hawakuwezi wewe unawakimbiaSiwezi ibiwa na mtu aliyefeli shule hata siku moja.
Kwanza sipendi vitu vya bei nafuu.
Mbili nipo huru na pesa yangu, na sina tamaa.
Tatu, ninachokitaka ndio huwa, sina tabia ya kumsikiliza MTU. Mimi ni dikteta. Hunipeleki peleki.
Kabla sijanunua kitu nimeshafanya research.
Nikitembea huwezi nikaribia na kunigusa, utajuta.
Kuibiwa ni dalili ya ujinga. Kabla uniambie kufanyiwa ujambazi.
Lakini wizi kama wizi sidhani.
Usipende bwerere
Taja sehemu ya utotoni usiyoisahauShikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la (7) tu kwa sababu ya umasikini.
Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku, na kwa namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.
Wewe jenga picha wale wezi wa pale kariakoo wanakuibia mfukoni bila hata wewe kujua kama kuna mkono umeingia ndani ya mfuko wako wa suruali na kuchukua pesa yako ya dagaa. Zile ni akili nyingi sana sema tu zimeelekezwa pahala pasipo stahili.
KISA KIDOGO CHA MIMI KUUZIWA KIPANDE CHA SABUNI KWA 20,000/= NIKIDHANIA NI SIMU
================
Nikiwa kidato cha 6 miaka hiyo ya 2000 na kitu, niliahi kuuziwa kipande kidogo cha sabuni nikidhani kuwa ni simu. Nilikuwa ninatoka Tabata Segerea nyumbani mama yangu mkubwa nilienda kumtembelea siku ya ijumaa jioni sasa nikawa ninarudi jumapili mchana ili nifanye maandalizi ya usafi wa nguo kwa ajili ya shule kesho yake ambayo ni Jumatatu.
Baada ya kushuka kutoka katika daladala pale mtaa wa Kongo akatokea jamaa mmoja rika langu akiwa ameshika simu aina ya nokia zile za jeneza za zamani akawa ananioneshea kwa ukaribu basi mimi nikaichukua ile simu nikaikagua vema kisha nikamuuliza bei gani, yeye akasema ni 20,000/=. Nikasema kimoyomoyo poa ngoja nichukue hii ngoma ili na mimi nikatambe huko mitaani.
Alafu hiyo pesa yenyewe sasa ndio nilikuwa nimepewa kama pocket money ya mwezi mzima na huyo mama yangu mkubwa. Yule jamaa rika langu kabisa akaniambia mwamba njoo huko hapo barabarani sana, basi mimi nikaenda, akanipa tena simu nikaikagua kwa mara ya pili, simu ipo sawa haina tatizo.
Sawa. Basi mwamba akaichukua simu akaiweka katika bahati fulani hivi ya kaki kisha na mimi nikampa pesa yake 20,000/= huyo nikaondoka. Kabla sijaenda mbali, baada ya kupanda daladala za kwenda home kwetu kurasini, nikaona ngoja nifungue bahasha nitoe simu yangu walau nicheze hata game la nyoka niji-keep busy, halooooo!
Nilikutana na kipande cha sabuni ya kodrai hahahahahaaaaa size ile ile kama simu ya Nokia ya jeneza (3310) kikiwa kinaniangalia tu. Kwa kweli roho iliniuma sana.
Ukizingatia 20,000/= ni pesa nyingi sana kwa miaka ile alafu mimi bado mwanafunzi sina majukumu mengi. Basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia hasira nilizokuwa nazo na nilipofika home nikafua nguo zangu kwa kutumia sabuni ya kipande ya 20,000/= hahahahaaaaa.
Kuna watu wenye akili nyingi lakini hawajasoma sana hususan huko vijijini. Unakuta mwanakijiji yeye hawajawahi kuwa na njaa bomani kwake. Miaka yote anavuna mahindi mengi, anafuga ng'ombe wake vizuri na anasomesha watoto kwa kuuza maziwa tu mpaka watoto wanamaliza form six. Siku akiamua kukuandikia barua, huo muandiko wake utadhani labda ni mwalimu wa secondary.
Wakuu, Hii ndana ni mimi pekee au hata wewe pia unaijua? Je, ulishawahi kuwaona/kukutana na watu wana namna hii?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kuwaona/kukutana na watu wa namna hiyo?
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?Msowero, Mvumi, Rudewa, Kilosa, Mkambarani, n.k. huko ndiko machimbo ya magenius STD 7, haataarii!
Hapo Msowero wanaitwa MALEBANONI!
Everyday is Saturday.............................. 😎
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?Unapajua Kizunguzi?
Pole sana mkuu...Mimi niliuziwa kipande cha sabuni pia.,
kisa kinaendana na chako.
Huyo aliyekuuzimia kipande Cha sabuni unajuaje ni darasa la Saba?? Ila hoja yako bado Ina mantiki...wako wengi darasa la Saba lakini ni brilliant and intelligent...chukulia kwa mfano mbunge kibajaji...Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la (7) tu kwa sababu ya umasikini.
Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku, na kwa namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.
Wewe jenga picha wale wezi wa pale kariakoo wanakuibia mfukoni bila hata wewe kujua kama kuna mkono umeingia ndani ya mfuko wako wa suruali na kuchukua pesa yako ya dagaa. Zile ni akili nyingi sana sema tu zimeelekezwa pahala pasipo stahili.
KISA KIDOGO CHA MIMI KUUZIWA KIPANDE CHA SABUNI KWA 20,000/= NIKIDHANIA NI SIMU
================
Nikiwa kidato cha 6 miaka hiyo ya 2000 na kitu, niliahi kuuziwa kipande kidogo cha sabuni nikidhani kuwa ni simu. Nilikuwa ninatoka Tabata Segerea nyumbani mama yangu mkubwa nilienda kumtembelea siku ya ijumaa jioni sasa nikawa ninarudi jumapili mchana ili nifanye maandalizi ya usafi wa nguo kwa ajili ya shule kesho yake ambayo ni Jumatatu.
Baada ya kushuka kutoka katika daladala pale mtaa wa Kongo akatokea jamaa mmoja rika langu akiwa ameshika simu aina ya nokia zile za jeneza za zamani akawa ananioneshea kwa ukaribu basi mimi nikaichukua ile simu nikaikagua vema kisha nikamuuliza bei gani, yeye akasema ni 20,000/=. Nikasema kimoyomoyo poa ngoja nichukue hii ngoma ili na mimi nikatambe huko mitaani.
Alafu hiyo pesa yenyewe sasa ndio nilikuwa nimepewa kama pocket money ya mwezi mzima na huyo mama yangu mkubwa. Yule jamaa rika langu kabisa akaniambia mwamba njoo huko hapo barabarani sana, basi mimi nikaenda, akanipa tena simu nikaikagua kwa mara ya pili, simu ipo sawa haina tatizo.
Sawa. Basi mwamba akaichukua simu akaiweka katika bahati fulani hivi ya kaki kisha na mimi nikampa pesa yake 20,000/= huyo nikaondoka. Kabla sijaenda mbali, baada ya kupanda daladala za kwenda home kwetu kurasini, nikaona ngoja nifungue bahasha nitoe simu yangu walau nicheze hata game la nyoka niji-keep busy, halooooo!
Nilikutana na kipande cha sabuni ya kodrai hahahahahaaaaa size ile ile kama simu ya Nokia ya jeneza (3310) kikiwa kinaniangalia tu. Kwa kweli roho iliniuma sana.
Ukizingatia 20,000/= ni pesa nyingi sana kwa miaka ile alafu mimi bado mwanafunzi sina majukumu mengi. Basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia hasira nilizokuwa nazo na nilipofika home nikafua nguo zangu kwa kutumia sabuni ya kipande ya 20,000/= hahahahaaaaa.
Kuna watu wenye akili nyingi lakini hawajasoma sana hususan huko vijijini. Unakuta mwanakijiji yeye hawajawahi kuwa na njaa bomani kwake. Miaka yote anavuna mahindi mengi, anafuga ng'ombe wake vizuri na anasomesha watoto kwa kuuza maziwa tu mpaka watoto wanamaliza form six. Siku akiamua kukuandikia barua, huo muandiko wake utadhani labda ni mwalimu wa secondary.
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi. Je, ulishawahi kukutana nao katika maisha yako?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kwa jinsi ulivyo hivi wewe huwajui kabisa hawa wajuba, jichanganye nao ndo uje utuambie hawakuwezi wewe unawakimbia
Nimetumia kiwango hicho cha darasa la saba kumaanisha mtu ambaye hajasoma sana. Anaweza asiwe la saba lakini akawa form 2...Huyo aliyekuuzimia kipande Cha sabuni unajuaje ni darasa la Saba??