Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Rais Magufuli anafanya kazi ya ziada kuhusu ardhi na sasa inarudi kwa Wananchi maana mikoa mingi Wananchi waliteseka sana.
 
Ma-professors wengi ndio engine ya serikali na nchi kwa ujumla...


Ndio maana nikakamwambia akili za daradani sio akili za mtaani ,,,

Wapo wenye uwezo darasani ukimleta mtaani anashindwa kuperfome, Na wapo wenye ujanja mtaani ukimleta darasani anakuwa Wa mwisho.
 
Kusoma sana hakuna mbadala kama nchi inataka kusonga mbele...


Kusoma ni lazima, lakini sio kila aliyesoma sana ndiye aliyefanikiwa sana,,, rudi kwenye mada yako!

Elimu ya darasani ina tofauti na elimu ya mtaani, ukishindwa kulijua hili basi hutapata jibu la swali lako
 
Tajiri wa kutupwa hawezi kuwa "Policy Maker" wa nchi kwa maana pesa anazo lakini hana utaalam...

Sio kweli hata kidogo,,

Donald John Trump ni tajiri Wa kutupwa lakini ni Rais Wa Marekani

Mayor Wa New York Michael Bloomsburg ni tajiri Wa kutupwa lakini ni mwanasiasa maarufu marekani

Berluscon alikuwa waziri mkuu Wa Italy na alikuwa tajiri mkubwa nchini humo.

Hata hapa kwetu wakina Freeman Mbowe ni matajiri kwao tangu babayake Aikael Mbowe mpaka mwanae Freeman lakini ni wanasiasa wote wawili.

Mkumbuke pia Paul Rupiah aliyekuwa mfanyabiashara tajiri sana Mwanza, na alikuwa mwanasiasa pia aliyemsaidia sana Mwl Nyerere kwenye kudai Uhuru.

Kwahiyo hoja yako kuwa matajiri eti hawawezi kuwa wanasiasa eti kwasababu wana Mali nyingi hawahitaji kuwa viongozi ni mufilisi, tena matajiri wengi wanahitaji kuwa wanasiasa au kwenye uhusiano na wanasiasa ili Mipango yao iende vizuri, mwangalie Abood Wa morogoro ni mbunge Wa ccm, kwani anashida gani kwenye Mali au siasa?!

Mwangalir Mohamed Dewji alikuwa mbunge Wa Singida, kwani sio tajiri mkubwa?!

Mwangalir Rostam Aziz alikuwa mbunge huko tabora kwani hakuwa tajiri?!

Mwangalie mzee Ndesamburo, alikuwa mbunge Wa Moshi Mjini na alikuwa tajiri vilevile?!

Asikudanganye mtu eti matajiri hawataki kuwa wanasiasa wakati unajua fika Mipango ya nchi ya kiuchumi ndio upangwa na wanasiasa sasa nani hataki kuwa mwanasiasa ili Mipango take ya kibiashara iende vizuri?!
 
Hiyo sio hoja ya msingi, kwani maprofessor hawataki kuwa matajiri?! Kwahiyo wao wameridhika kubaki kuwapakingia wenzao viwango vya kodi wao utajiri hawataki sio?!

Ingelikuwa hivyo, yule professor Anna Tibaijuka, angekumbwa na kashfa ya mabilioni aliyoyaita Visenti vya mboga?!

Hakuna mtu hasiyetaka utajiri kaka, tatito jinsi ya kuupata, uwe professor au uwe kapuku, wangekuwa na ujanja huo ungekuta maproffesors wote ni matajiri Wa kutupwa tatizo ujanja huo hawana. Ndio maana huwezi kuta proffesor tajiri mkubwa, elimu yao ya darasani haijawasaidia kuwa matajiri Bali kuishia kuajiriwa tu wengi wao, na wale watu Wa kawaida ndio unakuta mabilionairs referred to late Mengi, Mo Dewji, Abood , Bakhressa nk


Ma-professor sio matajiri wa kutupwa lakini wao ndio huwapangia hao matajiri wa kutupwa namna gani ya kutumia pesa zao kama vile viwango vya kodi wanavyopaswa kulipa serikalini...
 
Donald John Trump ni tajiri Wa kutupwa lakini ni Rais Wa Marekani
Trump sio "Policy Maker" yeye anatekeleza sera za nchi kama mwanasiasa na haundi sera.

Tena afadhali ungetolea mfano kwa nchi za Afrika na sio wanasiasa wa Ulaya. Hapa umekosea sana...
 
Hata hapa kwetu wakina Freeman Mbowe ni matajiri kwao tangu babayake Aikael Mbowe mpaka mwanae Freeman lakini ni wanasiasa wote wawili.
Upo sahihi. Mwanasiasa ni mtekeleza sera na sio muunda sera (Policy Maker)...
 
Mkumbuke pia Paul Rupiah aliyekuwa mfanyabiashara tajiri sana Mwanza, na alikuwa mwanasiasa pia aliyemsaidia sana Mwl Nyerere kwenye kudai Uhuru.
Sawa mkuu, mifano ni mingi sana mpaka familia ya akina Bush na Clinton...
 
Kwahiyo hoja yako kuwa matajiri eti hawawezi kuwa wanasiasa eti kwasababu wana Mali nyingi hawahitaji kuwa viongozi ni mufilisi,
Ila wewe jamaa unapenda sana kutunga mambo. Ni wapi nimesema kuwa tajiri hawezi kuwa mwanasiasa? Kwanini unanisingizia mambo ambayo sijayasema humu mkuu?...
 
matajiri wengi wanahitaji kuwa wanasiasa au kwenye uhusiano na wanasiasa ili Mipango yao iende vizuri, mwangalie Abood Wa morogoro ni mbunge Wa ccm, kwani anashida gani kwenye Mali au siasa?!
Mbona sijaongelea issues za SIASA vs UTAJIRI?...
 
Mwangalir Mohamed Dewji alikuwa mbunge Wa Singida, kwani sio tajiri mkubwa?!

Mwangalir Rostam Aziz alikuwa mbunge huko tabora kwani hakuwa tajiri?!

Mwangalie mzee Ndesamburo, alikuwa mbunge Wa Moshi Mjini na alikuwa tajiri vilevile?!
Unatoa mifano mingi sana mbayo ipo nje kabisa ya mada mkuu. Yaaani hoja ya KUSOMA SANA vs UTAJIRI wewe umeigeuza kuwa SIASA vs UTAJIRI? Umenishangaza sana mkuu...
 
Asikudanganye mtu eti matajiri hawataki kuwa wanasiasa wakati unajua fika Mipango ya nchi ya kiuchumi ndio upangwa na wanasiasa
Mipango hupangwa na "Policy Makers" ambao wapo wizarani na Ikulu, hao jamaa sio wanasiasa hata kidogo. Wao ni wazalendo to the fullest...
 
Back
Top Bottom