Utapeli kupitia laini za TTCL umeporomosha imani ya wateja kwa TTCL

Utapeli kupitia laini za TTCL umeporomosha imani ya wateja kwa TTCL

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,435
Reaction score
4,788
TTCL wanapaswa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaotumia laini za mtandao wao kufanya utapeli. Tatizo si hasara za kifedha pekee, bali pia kupungua kwa imani ya wateja.

Leo watu wengi wakiona simu kutoka kwenye laini za TTCL husita kupokea au hupuuza maelekezo muhimu wakidhani ni matapeli. Hali hii inaweza kuathiri hata mawasiliano halali kutoka kwa taasisi, kampuni na watu binafsi wanaotumia mtandao huo.

Kulinda uaminifu wa mtandao ni wajibu wa kila mtoa huduma za mawasiliano. Kuwabaini, kuwafungia na kushirikiana na vyombo vya dola kuwachukulia hatua wanaotumia laini za TTCL kufanya utapeli kutarejesha imani ya wananchi na kuimarisha usalama wa mawasiliano.
 
Mara nyingi hata mm hutumiwa sms kwa mt toka namba ya ttcl akifanya utapel
 
Back
Top Bottom