DOKEZO Utapeli mpya umeibuka kwenye Vyombo vya Habari Tanzania, Serikali chukueni hatua

DOKEZO Utapeli mpya umeibuka kwenye Vyombo vya Habari Tanzania, Serikali chukueni hatua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Naomba kuuliza huo ni aina gani ya mchezo???

Kutuma pesa alafu unakaa unasubiri wao waamue nani mshindi huo ni mchezo kweli??
 
Mimi sioni tatizo kwa Wachezeshaji kupiga pesa kwani Wabongo hawa ni wetu sote.

Ingawa ningetamani sana Mamlaka kuwalazimisha hawa Wachezeshaji kuwa wakweli ili "Mliwa" aliwe kwa ridhaa yake.

Kwa hali ilivyo sasa wengi wanapotoshwa na ushawishi wa Wachezeshaji.....haswa hii lugha ya kusema "kwa shilingi elfu moja tu unapata shilingi laki tatu" na hapohapo Wachezaji wengi wakiulizwa wanasema ametumia zaidi ya laki moja kuipata hiyo laki tatu.
 
Mm ni mpenzi wa kusikiliza clouds kila asubuhi na jioni niwapo njiani. Ikifika ile sehemu ya kuchezesha sijui pesa huwa nazima.

SIPENDI KUSIKIA UJINGA HUO WA WATU ZAIDI YA ELFU KUMI WANATOA ELFU MOJA MOJA ILI MMOJA WENU APEWE MILIONI HALAFU AITWE MSHINDI. BORA HATA WANAOBETI MPIRA ANGALAU UTASEMA ANAYEBETI ALIFANYA ANALYSIS, NA HADI MWENYE KAMPUNI YUPO KWENYE RISK YA KUPOTEZA, HII YA WATU ELFU KUMI KUCHANGA ELFU ELFU HALAFU MMOJA ANAPEWA MILIONI NYINGINE ZIBAKI REDIONI NI UJINGA WA WACHEZAJI, ILA WAJINGA NDO WALIWAO.
 
Nikwelii mkuu hii michezoo imekuwa mingi mnoo mimi kiukweli tangu michezo hii ianze sijawahii muona mtu ninaye mfahamu akashinda sa sijuii wanapeana. Ushindi wa mchongo ili tuzidi kutuma helaa
Halafu hata anayetangazwa kuwa mshindi haoneshi bashasha.
 
Hasira zako za Kucheza mara Elfu Mbili na mpaka sasa hujaambulia chochote usizilete katika hizi Media ambazo zinachezesha huu Mchezo Kihalali kabisa ( kwa ruhusa ya Gaming Board na Serikali ) huku Washindi nao wakipatikana kwa Haki pia.

Sasa kama una Nuksi zilizokujaa kutoka katika Visigino vyako hadi katika Kope zako za Macho yako hayo Makubwa uliyonayo kama Kalmati za Vingunguti ulitegemea nawe Ushinde kweli?

Kwani Umelazimishwa Kuucheza?
Dah mkuu vp tena mbona hivyo
 
Kwa upande wa commercial fm radio especially zinazosikika eneo kubwa la Tanzania nadhani ni RFA na East Africa Radio pekee ambazo hazifanyi hizi michezo
Ni kweli kabisa
 
Madhara ya punyeto iliyopitiliza hayaachani sana na betting iliyokubuhu. Unakumbuka shuka saa tatu ahsubuhi.

Punguza kubet hakuna mgodi wa utajiri huko
Uzuri sijawahi kufanya hivyo asante kwa ushauri
 
hio michezo imehalalishwa kisheria kwahiyo ww piga domo kodi inaingia kama kawaida na usitarajie serikali itakataza wakati inalamba kodi toka kwenye hiyo michezo ya kubahatisha
 
Kwaiyo ww unaona redio maria sio wezi?? ww ukiwa na akili timamu unamchangiaje bikra maria wakat hata dunian hayupo!
Hawa sio wezi si wameomba kihalali ni kama tu kujitolea msaada ila wazee tuma buku ni sawa na wale matapeli wa tumia namba hy
 
Kitu kikishakuwa hiyari sijui unaanzaje kulalamika.
Kama ni utapeli si watu waache kucheza, sio lazima
Sawa mkuu mm sijawahi cheza ila inaleta kero maana wengine tumeokoka kusikia watu wakitapeliwa inatuuma
 
Naomba kuuliza huo ni aina gani ya mchezo???

Kutuma pesa alafu unakaa unasubiri wao waamue nani mshindi huo ni mchezo kweli??
Ndio nashangaaga sana alafu wadau wanabariki sasa kuna utofauti gani na wale tuma kwenye namba hy alafu serikali inawavalia njuga kwann wasiruhusiwe na wao kihalali
 
Mimi sioni tatizo kwa Wachezeshaji kupiga pesa kwani Wabongo hawa ni wetu sote.

Ingawa ningetamani sana Mamlaka kuwalazimisha hawa Wachezeshaji kuwa wakweli ili "Mliwa" aliwe kwa ridhaa yake.

Kwa hali ilivyo sasa wengi wanapotoshwa na ushawishi wa Wachezeshaji.....haswa hii lugha ya kusema "kwa shilingi elfu moja tu unapata shilingi laki tatu" na hapohapo Wachezaji wengi wakiulizwa wanasema ametumia zaidi ya laki moja kuipata hiyo laki tatu.
Ndio utapeli wenyewe
 
Wakuu hivi tuseme hizi media zimeishiwa mbinu za kutafuta pesa au wanA wawezesha wasikilizaji?

Kumekuwa na mchezo mmoja saizi naona unasambaa kwenye kila redio.

Unakuta watangazaji wanasema tuma kiasi fulani ujishindie kiasi fulani.

Na ni kwa kila kipindi husika je huu sio utapeli kama serikali inapinga watu kutapeliwa kwenye simu. Sasa kwanini inaruhusu hizi media ziwatapeli watu.

Nb wamiliki wa media kama mnaona mnashindwa kuendesha matangazo yenu bora muombe msaada kama ifanyavyo redio maria kumchangia bikira maria (kapu la mama maria)

Kulikoni hiki mnachofanya?

AU wanakuu mnasemaje,? Kwenye hili
Hizo ndio njia rahisi za kutafuta pesa katikati ya wajinga, unakusanyanya milioni 10 kutoka kwao kisha unampa mmoja million 1 na wote wanaongeza juhudi ya kutuma pesa wakipigania kupewa milini 1
 
hio michezo imehalalishwa kisheria kwahiyo ww piga domo kodi inaingia kama kawaida na usitarajie serikali itakataza wakati inalamba kodi toka kwenye hiyo michezo ya kubahatisha
Ndio maana nasema na wale wa tuma kwa namba hy waruhusiwe
 
Back
Top Bottom