UTAPELI: njia za kuingiza kipato Kwa kuangalia video tiktok,YouTube na kulipwa!

UTAPELI: njia za kuingiza kipato Kwa kuangalia video tiktok,YouTube na kulipwa!

kadiri kasimba

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
588
Reaction score
1,150
Salamu wakuu!

Picha linaanza unafatwa kwenye comment labda umechangia mada flani TikTok
Kuna Fursa ya kujiingizia kipato Kwa siku kama itakupendeza niandikie neno nifundishe wanaweka na namba ya kumcheki,

Sasa ikishamcheki direct atakutumia video nyingi za kukuonesha watu wanavyo ingiza hela Kwa kuangalia video

Ukishaingia kwenye mfumo atakwambia kuna gharama za kujisajili na huwa mara nyingi huwa ni 13500 na unalipa kbs kwenye namba ya kampuni na imesajiliwa kabisa baada ya hapo anakuunga na itakuta kweli kuna video chache za kuangalia na utaambiwa uangalie,
Ukishazimaliza, utaona Kuna Hela umeingiza kwenye acc yako kidogo ambapo ata 2000 haifiki
Baada ya hapo utaambiwa uingie mafunzo
Na hapo ndo utaambiwa inabidi utafute watu wa kujiunga kama walivyokupata wewe ndo njia ya kuingiza kipato,

Sasa maswali yangu ni Haya
1.kama Wanajua kuwa njia ya kuingiza kipato ni kutafuta watu kwanini wasieleze awali na badala yake wanatangaza kuwa utalipwa Kwa kuangalia video? Huu si utapeli?
2.Ni watu wangapi wameingizwa mkenge Kwa staili hii na kuliwa hiyo 13500?
3.Je wasajili wa hizi platform inamaana hawajui utapeli unaoendelea wazi,wazi?
Nini kifanyike kuteketeza utapeli huu?
 
Nilishajiunga nikajiuta napewa shilingi 200 per video nikaacha😀
 
Vijana hawataki kazi ngumu, wanataka wachezee tu simu huku fedha ziingie. Hiyo haiwezekani
 
Back
Top Bottom