Utapeli tiGOPesa!

Utapeli tiGOPesa!

naona hiyo shida ilianza tokea jana na kitu chengine hata alert yoyote hawajatoa bado amini ila bora umetujuza..
 
Hayo yamenikuta na mie last week. Sijafanikiwa kurudishiwa 5,000 niliyonunua vocha kwa tigo pesa.Ingia kwenye http//m.tigo.co.tz/customercare usajili tatizo lako.Niliambiwa labda kuanzia kesho mambo yatakuwa sawa, tusubiri, ila ni vyema ukasajili tatizo lako customer care.
 
loh!toka jana nimejaribu kununua muda wa maongezi kwenye simu yangu ya tigo imeshindikana,leo asubuhi imekubali na kukata pesa lakini ni masaa kumi hadi sasa haiosomeki kwenye salio!!!!
 
Wataalamu wa software na kuingilia mitandao ya mifumo mbali mbali leo wameingilia mifumo ya tigo pesa so leo natoa taarifa kuwa wataotumia mtandao huu watakuwa wanahatarisha usalama wa amana zao kwa leo kwani hackers wanaweza kunasa mpaka password za account za watu

Unatumiwa nini? maelezo yako ni baada ya Tigo kutangaza bingo ya kupewa airtime kwa mtu yeyote aliyejisajili na baada ya kutumia service hiyo?
 
wakuu mbona hata voda ni hivyo hivyo.mimi nimeweka vocha ya 2000 nikaambiwa vocha imetumika kwenye namba zangu lakini nikiuliza salio naona hola!ingawa baada ya dk 15 inakubali.so yawezekana hata voda wana tatizo hilo hilo.
 
Hizi habari ni za uhakika ,mi mwenyewe ni wakala wa tigo pesa,toka juzi nimesitisha huduma ya tigo pesa,unamuingizia mteja fedha kwenye account yake ,wakala unapata majibu kuwa hela zimeenda kwa mtu flani lkn mteja hela hazifiki kwenye account yake,ukijaribu kupiga simu customer care ya tigo ipo busy muda wote,nimeshapata hasara ya tsh lak 2 hivihivi,Mwenye kusikia awe amesikia ,mwenye kuamini aamini,mwenye kupuuza aendelee kupuuza lkn majibu yatapatikana si muda mrefu,
 
Tigo wame post hii kwenye wall yao ya facebook
[h=6]Tigo Pesa upholds the highest standards of security and privacy in accordance with local and international regulatory procedure. Should you be experiencing any problems or issues with your service, please refer to our customer service department via email at customercare@tigo.co.tz
Tigo Pesa inazingatia viwango vya juu vya usalama na faragha ya kadiri ya utaratibu wa mamlaka za kitaifa na kimataifa. Ukipatwa na jambo au matatizo yoyote ya huduma yako, tafadhali lifikie idara yetu ya huduma kwa mteja kwa njia ya barua pepe customercare@tigo.co.tz
[/h]
 
Hili tatizo ni kweli lipo, mimi toka asubuh nimenunua muda wa maongezi kwa tigo pesa lakini mpaka sasa bado salio halijaongezeka na ktk tigo pesa wameshakata. Leo hii ni kama mara ya tatu hivi katika wiki mbili kitu kama hiki kinanitoke.
 
nadhani ngoja official notification kwani ni kawaida ya watanzania kutoamini mpaka tatizo lishindikane, hivi ninavyokwambia tayari tigo wanaendelea kukabiliana na tatizo hili na wameomba msaada wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa mifumo,
wewe kama huna imani tafuta wahusika wa TIGO waulize suala hili,

Kaka tunashukuru kwa taarifa hii nzuri.
 
mpesa maan..pesa yako iko salama wakati wowote

Mbona mie ijumaa nimetuma pesa kwa jamaa yangu kupitia M Pesa, kwa vile mie sijasajiliwa nikatumia wakala ambaye alituma direct kutoka kwenye simu yake, na nikapata message kuonesha kuwa pesa imeenda kwa mhusika, ila cha ajabu pesa hakufika kwa mhusika.
Hadi sasa hivi sijui nini cha kufanya na mbaya zaidi hata namba ya wakala sikuweza kuichukua na kwa sasa niko mbali na eneo husika.
 
Posibly,mida ya kabla ya sa 5 leo tigopesa ilkuwa haifany kaz na wakat mwngne ilkuwa inafanya lakn kwa bahat saaana.
 
Ni kweli hata mie nimenunua muda wa maongezi mara mbili inashindikana na hela wanasema nimeongezewa so marambilii zote hizo manake wameshakula buku mbili ila mara ya tatu imekubali ila buku mbili inamaanisha nimeliwa hawa dawa yao kuwahama tu au kuacha kutumia service zao manake naona sikuhizi wameamua kujiharibia halafu hawajui kitu kinachoitwa samahani manake hata siwaelewi.
 
jana nimemtumia mtu kwa Tigo pesa akaniambia amepata lakini kunapungufu ya shs 1OOO. Wakati mimi nilikatwa charges za kutumia. Ni kweli kuna tatizo kwenye tiGo pesa.
 
tunapoingia katika mfumo wa maisha wa kikompyuta, mambo haya hayaepukiki, kwasasa matukio bado ni machache sana, maofisa wa polisi wameona mbali imebidi iwapeleke baadhi ya maofisa wake ili kuweza kufanya uchunguzi wa matukio kama hayo.
 
ndo nimeelewa sasa_juz wife kakauta 45 elfu imeliwa, leo kakuta 100elfu imeliwa_tunawauliza tigo_hawana majibu itakuwa hackers wamevamia , kaz kwel kwel
 
Back
Top Bottom