Utapeli Uagizaji wa Bidhaa Kutoka Nje ya Nchi

Utapeli Uagizaji wa Bidhaa Kutoka Nje ya Nchi

Elimu tosha kabisa nitashangaa sana km mwanaJF atafanya kosa km hili tena.

Thank you brother unatumia kinywaji gani tafadhari!!
 
Ukweli mchungu ni huu hapa.
Kununua simu aliexpress za topbrands kama LG, iphones, Sony, Samsung, Googlepxl, na nyinginezo ukiambiwa ni brand new ni umedanganywa hizo ni refurbs (zile simu ambazo zilikua na shida zikatengenezwa wanaziweka macover mapya zionekane mpya ila in reality sio mpya, na wanafanya repackaging kabisa na box lake ukiifungua unasema 0 mileage.

Simu ambazo unaweza kuzipata. Mpya yaani brand new kutoka mitandao ya kichina kama aliexpress, alibaba, na mingineto ni hizi hapa

1. XIAOMI
2. HUAWEI
3. LENOVO
4. ZTE
5. NOKIA
Na nyenginezo brand kubwa kubwa za kichina.

Kwa hiyo ndugu zangu mnaonunua hizo s9 sijui s10 na iphones kariakoo na makumbusho na maduka mengi nchini kwa kuambiwa ni mpya ni mnadanganyika na kurubuniwa, ila si mnapenda bei rahisi huko ndio penyewe.

Mfano Ukitaka Samsung mpya hizi flagship kwa hapa TZ utapata kwenye maduka ya mitandao ya simu, dealership stores na baadhi ya maduka makubwa ila bei zake lazima ushtuke kidogo ukija kulinganisha na zile za wachinku.
Thanks broo, nimejifunza kitu [emoji120][emoji120]
 
Wengi wanapingwa ila wapo kimya mm kikuu niliagiza mzigo ila ulinifikia sikuupeenda ulikua ni kopi iliyokuwa kubuu nilirudisha
 
Wachina sometimes wangese sana, kuna bidada alichagua nguo aliexpress gauni mbili zinavutia kwa picha, bidhaa ilipofika ilikuwa ya ajabu sana.

Kuna molds za silcone nilizinunua, kuzipokea ni vibaya kuliko picha zenyewe. Aliexpress inahitaji umakini sana kununua, na pia kusoma reviews za waliokwisha fanya biashara na muuzaji.
Daaah umenifungua ubongoo[emoji848][emoji848]
 
Pole Kwa yaliyokukuta Ila AliExpress ule mtandao unaongoza Kwa kuuza vitu vya hovyo sana na kama unapenda cheap ndiyo utabinunua Hadi basi Ila huyo mfanya biashara kwanini akutajie mtandao unaouza vitu vibaya bora Amazon ingawaje kule napo unatakiwa uwe Makini mana wapigaji wengi
Amazon umakini kama upi mkuu?
 
Mi nawaza baada ya wewe kumpatia link ya simu yako unayoitaka aliipuuza na kwenda kuchukua clone za kikuu. Usithubutu kununua kitu kikuu hasa bidhaa za elektroniki.
 
Wana Jamii Forums Salaam. Natumai kila mtu ameshakifuta vumbi kichinjio chake tayari kwa ajili ya kesho.

Nimekuwa nikiona matangazo mbalimbali ya watu kuagiza Bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi. Kiukweli yale matangazo yamekuwa yakivuta attention ya watu na wengine wamekuwa wakijitosa na kuagiza bidhaa nje ya nchi mimi nikiwa mmoja wapo.

Kuna waagizaji ambao ni maarufu na wengine ambao sio maarufu. Mimi niliwahi kufanya biashara na bwana mmoja maarufu saana humu ndani ambaye anaagiza bidhaa toka nje ya nchi na mara nyingi ukitaka kuagiza bidhaa kutoka Ebay au Amazon huwa ana recommend akuagizie kupitia Ali Express.

Mwaka jana nilikuwa na shida. Kutokana na reputation ya yule bwana nikaamua kufanya nae mawasiliano na kumuomba aniagizie samsung S9+ kwa kuamini kwamba yeye ni mzoefu na hawezi fanya utapeli wa aina yoyote.

Nilimpatia link ya simu niliyokuwa naitaka toka ebay ila akanishauri aniagizie toka Aliexpress. Nilimkubalia kwa sababu nilitokea kumwamin saana kupitia post zake humu ndani. Baada ya kumpa jina la simu na rangi niliyotaka

Sikujihangaisha tena na kila kitu nilimwachia amalize yeye. Gharama ya simu mpaka kunifikia mkononi ilikuwa milioni moja na laki mbili na elfu arobaini. Nililipa pesa zote bila baki kupitia Tigo pesa.

Baada ya miezi miwili ya kusubiri nilipokea mzigo wangu wa simu ukiwa umefungwa vizuri. Ilikuwa ni samsung s9 plus kwa nje. Kwa kuwa ilikuwa ni mpya nilitegemea high performance lakini cha ajabu ile simu ilianza kupata joto kubwa kwa nyuma na ilikuwa inaishiwa chaji baada ya masaa manne au matano regardless matumizi. Nilijaribu kuwasiliana na jamaa yangu mmoja ambae pia alikuwa anatumia simu kama ile kutaka kujua huenda ni tatizo la simu kwa ujumla lakini jamaa aliniambia simu yake ilikuwa haipati joto na akichaji asubuhi inadumu na chaji mpaka jioni.

Nilijaribu kugoogle maneno yaliyoko nyuma ya simu ambayo huwa yanaonyesha model pamoja na manufacturer wa simu. Nilikuja kugundua ile simu ilikuwa ni clone/fake na ilitakiwa kuuzwa angalau laki 4 au 3. Niliumia saana lakini sikuwa na cha kufanya.

Jamaa aliyenifanyia hivi ni maarufu saaaana humu ndani kwenye haya mambo ya uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi ila Kesho tukapige kura tu.
we muongo mtaje.
 
Back
Top Bottom