Ukweli mchungu ni huu hapa.
Kununua simu aliexpress za topbrands kama LG, iphones, Sony, Samsung, Googlepxl, na nyinginezo ukiambiwa ni brand new ni umedanganywa hizo ni refurbs (zile simu ambazo zilikua na shida zikatengenezwa wanaziweka macover mapya zionekane mpya ila in reality sio mpya, na wanafanya repackaging kabisa na box lake ukiifungua unasema 0 mileage.
Simu ambazo unaweza kuzipata. Mpya yaani brand new kutoka mitandao ya kichina kama aliexpress, alibaba, na mingineto ni hizi hapa
1. XIAOMI
2. HUAWEI
3. LENOVO
4. ZTE
5. NOKIA
Na nyenginezo brand kubwa kubwa za kichina.
Kwa hiyo ndugu zangu mnaonunua hizo s9 sijui s10 na iphones kariakoo na makumbusho na maduka mengi nchini kwa kuambiwa ni mpya ni mnadanganyika na kurubuniwa, ila si mnapenda bei rahisi huko ndio penyewe.
Mfano Ukitaka Samsung mpya hizi flagship kwa hapa TZ utapata kwenye maduka ya mitandao ya simu, dealership stores na baadhi ya maduka makubwa ila bei zake lazima ushtuke kidogo ukija kulinganisha na zile za wachinku.