Utapeli uliofumbiwa macho na Serikali

Utapeli uliofumbiwa macho na Serikali

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UTAPELI ULIOFUMBIWA MACHO NA SERIKALI.

Anaandika Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu jeusi.

Angalizo; Andiko hili laweza kuwa na Lugha Kali hasa Kwa waumini wa madhehebu ya utandawazi. Hivyo Kama ni mwepesi WA hasira, mwoga wa ukweli, na unayeongozwa na mihemko, tafadhali achia hapahapa kusoma. Kuendelea kusoma huku ukijua huwezi himili lugha Kali itahesabika Kama ukaidi na madhara ya kujitakia, nami sitahusika.

Utapeli ni kitendo cha kumlaghai mtu Kwa kumuibia Mali au haki zake Kwa kutumia maneno au ujanja usiohusisha Nguvu.
Utapeli ni Aina ya wizi usiohusisha nguvu ya Mwili. Utapeli ni kwenda kinyume na makubaliano.

Ikiwa makubaliano yatatimizwa basi hakutakuwa na utapeli, na Kama katika makubaliano kuna mmoja ameonewa Kwa ujinga au shida zake haitahesabika Kama utapeli. Mfano, mekubaliana na Mtu katika biashara ya mazao. Akakuambia Niuzie hayo mahindi Gunia moja Kwa Tsh 100,000/= mkauziana kisha yeye akaenda kuyauza hayo mahindi Gunia moja Tsh 200,000/= huo sio utapeli.

Mfano wa #2
Mmekubaliana Utalipwa laki tatu, nawe Kwa hiyari yako ukakubali licha ya Mshahara kuona haukutoshi. Huo sio utapeli. Labda akikupa chini ya hapo au asikupe kabisa, huo huitwa utapeli.
Utapeli ni Aina Fulani ya dhulma ya akili au ujanja ujanja. Wizi wa kuaminika.

Utapeli upo wa Aina nyingi lakini msingi Mkuu wa utapeli ni kuiba uaminifu wa mtu.

Aina za UTAPELI
1. Utapeli wa Mali
2. Utapeli wa fikra au wazo
3. Utapeli wa Muda.

Utapeli wa Muda unaingia sehemu karibu zote.
Mfano: Umemuachia mtu kazi Kwa kumpa Oda Fulani, akufanyie au akuandalie Jambo Fulani. Mkakubaliana siku kumi zijazo utakuja kuchukua. Inafika siku ya 9 unapiga simu kuwa umeghairi na unamuambia huwezi kulipia Kwa sababu hujachukua. Hujali mwenzako amehangaika kushughulikia Oda yako. Hapo umemtapeli mwenzako Muda wake na pia baadhi ya gharama alizotumia.

Utapeli katika masuala ya Uchumba, upo Kwenye mahusiano na binti au kijana wa watu, kumbe hauna Future naye, huo ni utapeli wa Muda.

Serikali inaweza kushughulikia utapeli karibia wote lakini utapeli wa kwenye makanisa ya siku hizi umeufumbia macho.

Sijajua Kwa nini serikali imefumbia macho utapeli unaoendelea kwenye makanisa haya ya siku hizi.

Matapeli wamejiimarisha mpaka imefikia hatua wanalipia vipindi Redioni na kwenye Luninga ili kutapeli watu. Wapo ambao wamebarikiwa mpaka kufungua Media ili wazidi kutapeli watu.

Baadhi ya matapeli ni rafiki zangu Wakubwa, wanawaita Manabii na mitume, huwaga nikiongea nao wanabakia kuniambia niokoke huku wakitabasamu.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anatibu UKIMWI Kwa maombi wakati ni uongo wa wazi Kabisa, inafumbia macho wakati msemaji Hana hata cheti cha Udaktari, Hana Uelewa wa kina wa ugonjwa huo.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anafufua wafu inakaa kimya badala ya kumpa mtu huyo karipio la kuacha kuirubuni jamii.

SERIKALI inasikia kabisa mtu akiwadanganya watu kuwa anatoa Utajiri na inajua ni uongo kabisa lakini inafumbia macho. Kama hawa manabii wangekuwa wanatoa Utajiri Kwa nini wasiisaidie Nchi kuwa Tajiri mpaka tunakopa mikopo nchi za zingine.

Hao manabii hivi wanajua nchi yetu inakopa? Hao manabii hivi wanajua kuwa nchi hii kila siku watu wanakufa? Kama sio utapeli Kwa nini washindwe kutoa Suluhu la matatizo ya nchi yetu. Hawa manabii wanajua nchi yetu kuna watu ni Watumwa wanalipwa mishahara ya laki na ishirini Kwa mwezi na wanafamilia?

Yupo mtume mmoja alinipigia siku mwaka Juzi kunitishia, nikamwambia asifikiri kila mtu ni Mpumbavu.

Pendekezo;

1. Serikali iunde sheria zinazozibana taasisi za Kidini kuhusu kutapeli wananchi hasa katika kutoa mafundisho ya uongo yanayoingilia fani na taaluma za watu wengine Kama Madaktari, waalimu n.k.
Unakuta mchungaji anaongea uongo kabisa alafu anapigiwa Makofi ukimuuliza atakuambia ni mambo ya kiroho. Hakuna mambo ya hivyo.

2. Kwa vile dini ni biashara, serikali itoze Kodi kutoka Kwa taasisi za Kidini.
Wafanyakazi wa dini husika wasajiliwe kuanzia Wachungaji, wapiga kinanda na waimba kwaya. Nilishawahi kusema, wapo watu wanatumika bure Kanisani pasipo kulipwa, kuanzia Wana kwaya mpaka mashemasi walipwe mishahara sio wadanganywe wanamtumikia Mungu Bure. Hakuna Mungu WA bure.

3. Iundwe sheria kuwa wachungaji sharti wawe wamesomea uchungaji na wanacheti. Na wahubiri kulingana na vyeti vyao. Sio mtu Hana Uelewa wowote wa Dunia na mambo ya Zama hizi anapewa kipaza sauti anahutubia taifa zima mambo ya kizamani ambayo baadhi ni irrelevant Kwa Zama hizi.

Mtu WA Darasa la Saba au Kidato cha nne azungumzie mambo ya kawaida Kwa kiwango cha elimu yake, sio aongee mambo yaliyomzidi uwezo, mambo complicated mwishowe apotoshe jamii.

4. Sheria za Miradi ya Kanisa iundwe kuwa waumini wa Kanisa husika watalipiwa Nusu ya Ada na Kanisa alafu nusu nyingine watatoa wenyewe. Sio waumini wajenge mashule na Hospitali ya Kanisa alafu bado muwaumize kwenye Ada kubwa Kwa watoto wao wajapo kusoma. Huo ni uhuni na utapeli. Kama shule au Hospital niya Kanisa Acha watoto wa waumini wafaidi Miradi Yao. Ninaongea Kwa uzoefu.

5. Mafundisho yajikite zaidi kutatua matatizo ya Zama hizi za wanajamii na sio kujikita katika ulimwengu ujao ambao hakuna mwenye ushahidi nao. Mafundisho ya ulimwengu ujao yanatengeneza kizazi cha uvivu wa fikra na kuona hapa Duniani tunapita. Hivyo kukifanya kukosa Ari ya kufanya maendeleo.

6. Mapato ya wachungaji yaendane na Hali halisi ya waumini.

7. Serikali ijihusishe na dini Kama haijihusishi ni Bora izifute zote, tuongozwe na utanzania na sheria za nchi.
Dini na madhehebu ya Dini ni Kama Club za Simba na yanga tuu, ni Kama taasisi zingine lazima ziingiliwe na kuwekewa sheria Kali.

8. Iundwe sheria ambazo zitasimamiwa na Baraza la dini litakaloundwa kuhusu vyeo vya majina ya viongozi WA dini. Rank ya juu Kama itakuwa ni Kuitwa Nabii. Ambaye atathibitishwa Kwa maajabu ayafanyayo mubashara, kutabiri na ikatokea, na kufanya mambo makubwa Kama kufufua.

Nabii atajaribiwa unabii wake mbele ya halaiki Kwa kupewa atoe miujiza kadhaa ya kumthibitisha, na sio mdomo wake umthibitishe.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM
 
Mkuu umenena ukweli mtupu ila wafia dini wasio na uelewa wa mambo watakushambulia pasipo hoja.
 
Yaani dunia ipo busy kutafuta dawa ya kuponya UKIMWI miaka na miaka halafu eti kuna mchungaji wa bonyokwa anaponya hahahaaa..

Hao jamaa ni matapeli wakutosha tu maana kama kweli wanaponya kwanini wasiende mahospitali kama Muhimbili palipo na wagonjwa wa kila aina wawaponye ili kuwapunguzia gharama za matibabu na kuisaidia serikali.

Badala yake wanafanya maigizo ya kutafuta walemavu feki na wagonjwa feki kujifanya wamewaponya na kushuhudia uongo.
 
UTAPELI ULIOFUMBIWA MACHO NA SERIKALI.

Anaandika Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu jeusi.

Angalizo; Andiko hili laweza kuwa na Lugha Kali hasa Kwa waumini wa madhehebu ya utandawazi. Hivyo Kama ni mwepesi WA hasira, mwoga wa ukweli, na unayeongozwa na mihemko, tafadhali achia hapahapa kusoma. Kuendelea kusoma huku ukijua huwezi himili lugha Kali itahesabika Kama ukaidi na madhara ya kujitakia, nami sitahusika.

Utapeli ni kitendo cha kumlaghai mtu Kwa kumuibia Mali au haki zake Kwa kutumia maneno au ujanja usiohusisha Nguvu.
Utapeli ni Aina ya wizi usiohusisha nguvu ya Mwili.
Utapeli ni kwenda kinyume na makubaliano.

Ikiwa makubaliano yatatimizwa basi hakutakuwa na utapeli, na Kama katika makubaliano kuna mmoja ameonewa Kwa ujinga au shida zake haitahesabika Kama utapeli,
Mfano,
Umekubaliana na Mtu katika biashara ya mazao. Akakuambia Niuzie hayo mahindi Gunia moja Kwa Tsh 100,000/= mkauziana kisha yeye akaenda kuyauza hayo mahindi Gunia moja Tsh 200,000/= huo sio utapeli.

Mfano wa #2
Mmekubaliana Utalipwa laki tatu, nawe Kwa hiyari yako ukakubali licha ya Mshahara kuona haukutoshi. Huo sio utapeli. Labda akikupa chini ya hapo au asikupe kabisa, huo huitwa utapeli.
Utapeli ni Aina Fulani ya dhulma ya akili au ujanja ujanja. Wizi wa kuaminika.

Utapeli upo wa Aina nyingi lakini msingi Mkuu wa utapeli ni kuiba uaminifu wa mtu.

Aina za UTAPELI
1. Utapeli wa Mali
2. Utapeli wa fikra au wazo
3. Utapeli wa Muda.

Utapeli wa Muda unaingia sehemu karibu zote.
Mfano,
Umemuachia mtu kazi Kwa kumpa Oda Fulani, akufanyie au akuandalie Jambo Fulani. Mkakubaliana siku kumi zijazo utakuja kuchukua.
Inafika siku ya 9 unapiga simu kuwa umeghairi na unamuambia huwezi kulipia Kwa sababu hujachukua. Hujali mwenzako amehangaika kushughulikia Oda yako. Hapo umemtapeli mwenzako Muda wake na pia baadhi ya gharama alizotumia.

Utapeli katika masuala ya Uchumba, upo Kwenye mahusiano na binti au kijana wa watu, kumbe hauna Future naye, huo ni utapeli wa Muda.

Serikali inaweza kushughulikia utapeli karibia wote lakini utapeli wa kwenye makanisa ya siku hizi umeufumbia macho.

Sijajua Kwa nini serikali imefumbia macho utapeli unaoendelea kwenye makanisa haya ya siku hizi.

Matapeli wamejiimarisha mpaka imefikia hatua wanalipia vipindi Redioni na kwenye Luninga ili kutapeli watu.
Wapo ambao wamebarikiwa mpaka kufungua Media ili wazidi kutapeli watu.

Baadhi ya matapeli ni rafiki zangu Wakubwa, wanawaita Manabii na mitume, huwaga nikiongea nao wanabakia kuniambia niokoke huku wakitabasamu.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anatibu UKIMWI Kwa maombi wakati ni uongo wa wazi Kabisa, inafumbia macho wakati msemaji Hana hata cheti cha Udaktari, Hana Uelewa wa kina wa ugonjwa huo.

Serikali inasikia kabisa mtu anatangaza anafufua wafu inakaa kimya badala ya kumpa mtu huyo karipio la kuacha kuirubuni jamii.

SERIKALI inasikia kabisa mtu akiwadanganya watu kuwa anatoa Utajiri na inajua ni uongo kabisa lakini inafumbia macho.
Kama hawa manabii wangekuwa wanatoa Utajiri Kwa nini wasiisaidie Nchi kuwa Tajiri mpaka tunakopa mikopo nchi za zingine.

Hao manabii hivi wanajua nchi yetu inakopa?
Hao manabii hivi wanajua kuwa nchi hii kila siku watu wanakufa?
Kama sio utapeli Kwa nini washindwe kutoa Suluhu la matatizo ya nchi yetu.
Hawa manabii wanajua nchi yetu kuna watu ni Watumwa wanalipwa mishahara ya laki na ishirini Kwa mwezi na wanafamilia?

Yupo mtume mmoja alinipigia siku mwaka Juzi kunitishia, nikamwambia asifikiri kila mtu ni Mpumbavu.

Pendekezo;

1. Serikali iunde sheria zinazozibana taasisi za Kidini kuhusu kutapeli wananchi hasa katika kutoa mafundisho ya uongo yanayoingilia fani na taaluma za watu wengine Kama Madaktari, waalimu n.k.
Unakuta mchungaji anaongea uongo kabisa alafu anapigiwa Makofi ukimuuliza atakuambia ni mambo ya kiroho. Hakuna mambo ya hivyo.

2. Kwa vile dini ni biashara, serikali itoze Kodi kutoka Kwa taasisi za Kidini.
Wafanyakazi wa dini husika wasajiliwe kuanzia Wachungaji, wapiga kinanda na waimba kwaya.
Nilishawahi kusema, wapo watu wanatumika bure Kanisani pasipo kulipwa, kuanzia Wana kwaya mpaka mashemasi walipwe mishahara sio wadanganywe wanamtumikia Mungu Bure.
Hakuna Mungu WA bure.

3. Iundwe sheria kuwa wachungaji sharti wawe wamesomea uchungaji na wanacheti.
Na wahubiri kulingana na vyeti vyao. Sio mtu Hana Uelewa wowote wa Dunia na mambo ya Zama hizi anapewa kipaza sauti anahutubia taifa zima mambo ya kizamani ambayo baadhi ni irrelevant Kwa Zama hizi.
Mtu WA Darasa la Saba au Kidato cha nne azungumzie mambo ya kawaida Kwa kiwango cha elimu yake, sio aongee mambo yaliyomzidi uwezo, mambo complicated mwishowe apotoshe jamii.

4. Sheria za Miradi ya Kanisa iundwe kuwa waumini wa Kanisa husika watalipiwa Nusu ya Ada na Kanisa alafu nusu nyingine watatoa wenyewe.
Sio waumini wajenge mashule na Hospitali ya Kanisa alafu bado muwaumize kwenye Ada kubwa Kwa watoto wao wajapo kusoma. Huo ni uhuni na utapeli.
Kama shule au Hospital niya Kanisa Acha watoto wa waumini wafaidi Miradi Yao.
Ninaongea Kwa uzoefu.

5. Mafundisho yajikite zaidi kutatua matatizo ya Zama hizi za wanajamii na sio kujikita katika ulimwengu ujao ambao hakuna mwenye ushahidi nao.
Mafundisho ya ulimwengu ujao yanatengeneza kizazi cha uvivu wa fikra na kuona hapa Duniani tunapita. Hivyo kukifanya kukosa Ari ya kufanya maendeleo.

6. Mapato ya wachungaji yaendane na Hali halisi ya waumini.

7. Serikali ijihusishe na dini Kama haijihusishi ni Bora izifute zote, tuongozwe na utanzania na sheria za nchi.
Dini na madhehebu ya Dini ni Kama Club za Simba na yanga tuu, ni Kama taasisi zingine lazima ziingiliwe na kuwekewa sheria Kali.

8. Iundwe sheria ambazo zitasimamiwa na Baraza la dini litakaloundwa kuhusu vyeo vya majina ya viongozi WA dini.
Rank ya juu Kama itakuwa ni Kuitwa Nabii. Ambaye atathibitishwa Kwa maajabu ayafanyayo mubashara, kutabiri na ikatokea, na kufanya mambo makubwa Kama kufufua.

Nabii atajaribiwa unabii wake mbele ya halaiki Kwa kupewa atoe miujiza kadhaa ya kumthibitisha, na sio mdomo wake umthibitishe.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM
Taikuni wa fasihi hujawahi kuniangusha.

Ccm wote ni matapeli ukiwemo na wewe🤣
 
Serikali ikianza na huyu itapendeza sana.
images.jpeg
 
Mtoa mada kaanza na mikwara mizito.ila tuende mbele na kurudi nyuma kuna ndugu zetu wakiristo huko makanisani sijui akili zao huwa wanapeleka wapi saa zingine.nishawai ona mtu anapeleka fungu la kumi kwa kanisa wakati baba yake na mama anauza mama ntilie anaishi nyumba ya kawaida .jamaaa kapeleka milion moja church.iliniuma sana nikamuuliza akasema haya ni mambo ya kiimani huwezi ukajua ww ni muislamu.basi sikuwa na jinsi ya kufanya.
 
Yaani dunia ipo busy kutafuta dawa ya kuponya UKIMWI miaka na miaka halafu eti kuna mchungaji wa bonyokwa anaponya hahahaaa..

Hao jamaa ni matapeli wakutosha tu maana kama kweli wanaponya kwanini wasiende mahospitali kama Muhimbili palipo na wagonjwa wa kila aina wawaponye ili kuwapunguzia gharama za matibabu na kuisaidia serikali.

Badala yake wanafanya maigizo ya kutafuta walemavu feki na wagonjwa feki kujifanya wamewaponya na kushuhudia uongo.

Hawa ndio wanafanya watu wazipuuze Dini na kuona ni geresha.

Kina Kiranga hupitia humo humo
 
Mtoa mada kaanza na mikwara mizito.ila tuende mbele na kurudi nyuma kuna ndugu zetu wakiristo huko makanisani sijui akili zao huwa wanapeleka wapi saa zingine.nishawai ona mtu anapeleka fungu la kumi kwa kanisa wakati baba yake na mama anauza mama ntilie anaishi nyumba ya kawaida .jamaaa kapeleka milion moja church.iliniuma sana nikamuuliza akasema haya ni mambo ya kiimani huwezi ukajua ww ni muislamu.basi sikuwa na jinsi ya kufanya.

😀😀😀😀

Inasikitisha Sana, Ila inafurahisha Kwa upande mwingine ukikutana na mtu huyo akikuelezea
 
Hakika umeandika kweli tupu, wengi wanajificha nyuma ya roho ntakatifu pale wanapoulizwa maswali wasiyoweza kujibu.
 
Mtoa mada kaanza na mikwara mizito.ila tuende mbele na kurudi nyuma kuna ndugu zetu wakiristo huko makanisani sijui akili zao huwa wanapeleka wapi saa zingine.nishawai ona mtu anapeleka fungu la kumi kwa kanisa wakati baba yake na mama anauza mama ntilie anaishi nyumba ya kawaida .jamaaa kapeleka milion moja church.iliniuma sana nikamuuliza akasema haya ni mambo ya kiimani huwezi ukajua ww ni muislamu.basi sikuwa na jinsi ya kufanya.
Zaka au Fungu la kumi ni amri na ni lazima hilo huwa halinaga mjadala mbona
 
Cha ajabu, hawa Manabi na viongozi wa makanisa mengine, ndo watu Serikali inawaogopa kuliko hata vijana wasio na ajira waliopo mtaani.

Usisahau pia hata hao unaowaambia wachukue hizo hatua wanananufaika pakubwa na kazi za hawa Miamba.(Manambii, mitume na makanisa).
Na baada ya kunogewa wako wanasogea taratibu na kwa wajuba wengine wanaitwa machifu😊😊😊😊😊😊😊
 
Ni utapeli kwa Manara kuwaambia wapenzi wa Yanga eti Feisal Salum ndio kiungo bora kuliko wote duniani.
 
Back
Top Bottom