Utapeli ulivyonirudisha Jamii Forums baada ya miaka 14

Utapeli ulivyonirudisha Jamii Forums baada ya miaka 14

Af juzi wakakucheka na itel yako kumbe jamaa unapiga pesa zako kimya kimya ndivyo inavyo takiwa boss
Wanataka nimiliki sim ya milion niifanyie nn, itel yangu naipenda nikipiga picha mizigo yangu inatoa freshi wao wanunueni tu hizo sim zao za heshima wanasema tusipangiane
 
Snuff inahela sana watu hawajui tu Mimi nauza ugoro wa kimasai naagiza hapo Dodoma nikichanganya na maji ya mwarobaini natoa kitu konk wiki tu mzigo umeisha
makampuni ya snuff ya copenhagen na skoal wanawakilisha zaidi ya $1bn kwenye retail sale
 
Kuna muda naweza kuwa nafikilia je wakina active au wakina paw na moderate wote hivi hawawezi kuwa I'd kama zetu wakaanzisha nyuzi, Huwa nawaza sana kwakweli mambo haya ni magumu sana 🤔
Ikitokea ikawa hivyo, unafikiri mimi naweza kuwa moderator yupi?
 
Tuache na my wetu LBL, nyie komaeni na mshahara wa mwisho wa mwezi sisi tunapiga pesa huku tumekaa. Siku hizi naingiza 20,000 kwa siku.
Alisikika bakubaku kichaa mmoja.

Kipo wapi sasa!
Sasa hivi wanaona aibu wanaongea kwa makundi makundi kama nyumbu wanaona aibu kama malaya. Kwenye magroup ya wasap wanajitetea kuwa viongozi wao wamesema kuna changamoto ndogo na BOT.
 
Nimeulizwa sana kwenye nyuzi, ngoja leo niwasimulie.

Jan 16, 2025 alinipigia simu ndugu yangu mmoja akasema anataka tuonanae. Nikamkaribisha nyumbani, akaja na akaanza kunielezea shida yake. Kiufupi, alikuja kuniomba nimuazime pesa na atanirudishia baada ya wiki mbili. Nikamuuliza kulikoni? akanijibu, kuna fursa ambayo amekutana nayo ya LBL Tanzania. Yeye ameshatengeneza faida ya zaidi ya TZS 300,000 na sasa kuna special offer, akiweka milioni 4 atapata milioni moja ya faida ndani ya wiki mbili kwa hiyo atatoa milioni 5 na ushee.

Taa nyekundu ikawaka kichwani, nilikua sijawahi kusikia kuhusu hiyo kampuni ila kwa maelezo ya awali, nilijua tu ni Pyramid scheme. Akanionyesha group lao la WhatsApp ambalo wako watu 1,000 pamoja na kiongozi wao muwakilishi kutoka hiyo kampuni na app yao ya movie. Alivyoona natilia mashaka, akasema bora hata nisingekuambia hiyo hela nataka kufanyia nini, maana ushaanza kuleta komplikesheni Nikaignore hiyo kauli, nikamwambia nitamjibu jumatatu ngoja nimshirikishe Mr. (Wote mlio kwenye mahusiano mnajua hichi kisingizio kinavyotusevu kwenye upumbavu).

Alivyoondoka nikaendelea na utafiti wangu, nikagundua hao watu wa LBL ni matapeli. Kwa sababu sina mitandao ya kijamii, nikawa natafuta namna gani nitawaambia na watu wengine kuhusu hili janga. Ndiyo nikakumbuka kuna Jamii forums ya Maxence Melo , wakati najiunga 2011 nilikua binti mdogo na jamvi lilikua la moto sana kwa mambo ya kiasiasa. Sikuwahi kuthubutu kuchangia na baadaye maisha yalichanganya (watoto, kazi, familia etc.) sikukumbuka tena mambo ya JF wala mtandao wowote wa kijamii.

Nyuzi yangu ya kwanza kuandika ilikua Ijumaa Jan 17, 2025 na ilihusu utapeli wa hii kampuni na kuwaonya watu kutojiunga LBL: Pyramid Scheme Inayowatapeli Watu kwa Kisingizio cha Uwekezaji. Pia nilimuonya huyo ndugu yangu na nikamwambia pesa ya kumuazima sina.

Japo lengo langu lilikua ni kuandika hii nyuzi ili kufikisha taarifa na kusign out after. Nilipoperuzi kidogo nilinogewa baada ya kukutana na nyuzi za mapishi za Mwachiluwi , nyuzi za siasa za Cute Wife , Waufukweni etc. nyuzi za picha za kushangaza za Mshana Jr , story za realMamy , Mallerina , Poor Brain , Eli Cohen , PSL god n.k bila kusahau replies za wanajamvi kama mzee Ushimen , Aaliyyah , Numbisa , ephen_ , Qashy Lilith , nakwede97 , Intelligent businessman na wengine wengi.

Asante kwa wote mnaoandika nyuzi za kufundisha, kutoa taarifa na kuburudisha.
Asanteni pia wote mnaochangia kwenye nyuzi zangu na mnaonichekesha kwenye replies kama Nomadix na wenzako.

Hakuna kipindi nimejifunza, nimefurahi na nimecheka kwa sauti mpaka nikaja kuulizwa kama niko sawa, kama baada ya kurudi JF last month. Haya tuliendeleze Jamvi 🫶!
Naona umetaja baadhi ya IDs zako kule juu. Umeamua kujitaja taja tu na kuandika upupu
 
Mkuu; ulivosema taa nyekundu ikakuwakia kichwani, nikastaajabu. Kumbe wanadamu mna taa na hamsemi? Kwenye traffic, taa nyekundu huashiria kusimama. Huenda hii ikawa sababu ya waliotapeliwa kuwa na akili zilizosimama..😁😁(Natania)

Kimsingi... Huwezi kutenganisha Watanzania na kutapeliwa.. sijui tumerogwa? Ukiangalia hii aina ya utapeli imekuwa ikifanana na zingine kasoro majina. Ila mimtu bado ipo tu. Inasikitisha kwakweli.
 
Back
Top Bottom