Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
- Thread starter
- #101
Swali zuri.Ushauri wako ni upi maana utapeli umeenea hata kwa makanisa yasiyouza hivyo vitu sadaka zimekuwa nyingi mno mtu unakamuliwa mpaka Senti ya mwisho uliyo nayo je tukasali wapi sasa maana tunampenda Mungu
Ni kweli utapeli umeenea, lakini Mungu hajawahi kukosa Watumishi wake waaminifu. Kama umehakikisha kabisa pasina shaka kwamba hapo unaposali kuna ujanja ujanja, ni heri utafute kanisa jingine linalohubiri Injili kamili ya Kristo bila kulazimisha watu kwa hila. Soma Biblia, muombe Mungu akupe hekima, na umshirikishe Roho Mtakatifu akuelekeze mahali sahihi pa kuabudu.
Sadaka inayompendeza Mungu ni sadaka inayotolewa kwa hiari si kwa kulazimishwa.
2 Wakorintho 9:7
"Kila mtu na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.