Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
- Thread starter
- #61
Sio naviona kama utapeli. Ni utapeli kabisa.Wakati wewe unaviona chumvi na mafuta ya upako kama utapeli, wachawi wakubwa duniani wanavipiga vita kali kwa sababu vinawaharibia mambo yao yanakwama.
Wewe umelishwa matango pori ya kutosha. Hebu nikuulize: ni nani mchawi mkubwa kuliko shetani? Wachawi wanafanya uchawi wao kwa kutumia nguvu za giza(shetani na mapepo). Kwa maneno mengine wachawi ni wasaidizi tu wa shetani. Sasa jiulize: Ni andiko gani linalosema tumpinge shetani kwa kutumia chumvi na mafuta? Jina la Yesu pekee linatosha kumpinga shetani
Yakobo 4:7 SRUV
“Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”
Andiko hilo halisemi tumieni chumvi na mafuta kumpinga shetani.
Kama ulisikia shuhuda za watu wanaodai ni wachawi na kwamba chumvi zimeharibu mambo yao, hizo ni shuhuda feki zenye lengo la kuzidi kuwafanya watu waamini kuwa chumvi na mafuta wanayouziwa vina nguvu. Shetani ni baba wa uongo.
Yohana 8:44 SRUV
"...Ibilisi ...tangu mwanzo; hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo."
Ibilisi amewatumia wachawi hao kueneza uongo ili watu wazidi kuliwa pesa zao na kuweka matumaini yao kwenye chumvi badala ya kulitumainia Jina la Yesu.
Katika Matendo 13:6-12 tunasoma habari za Elima Mchawi – aliyepigwa upofu kwa Jina la Bwana.
"Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na mtawala Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye mtawala akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi, akashindana nao, akitaka kumtia yule mtawala moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka? Basi, angalia, mkono wa Bwana uko juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule mtawala, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.”
Umeona? Hakuna chumvi iliyotumika hapo kumkemea Elima mchawi. Sasa wewe unadanganywa eti wachawi wanaipiga vita chumvi. Wachawi wanaogopa Jina la Yesu tu maana ndilo Jina lipitalo kila jina.
Katika Luka 10:19 SRUV Yesu anasema:
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
Yesu hajasema amewapa chumvi na mafuta. Badala yake anasema katika Marko 16:17 SRUV
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo...”
Jina la Yesu peke yake, linatosha kumshinda shetani, mapepo na wachawi wote duniani.
Shtuka! Toka huko, acha kuliwa pesa zako bure, na usiendelee kueneza uongo wa manabii wa uongo.