Utapeli wa “Chumvi na Mafuta ya Upako” Wafichuliwa

Ushauri wako ni upi maana utapeli umeenea hata kwa makanisa yasiyouza hivyo vitu sadaka zimekuwa nyingi mno mtu unakamuliwa mpaka Senti ya mwisho uliyo nayo je tukasali wapi sasa maana tunampenda Mungu
Swali zuri.
Ni kweli utapeli umeenea, lakini Mungu hajawahi kukosa Watumishi wake waaminifu. Kama umehakikisha kabisa pasina shaka kwamba hapo unaposali kuna ujanja ujanja, ni heri utafute kanisa jingine linalohubiri Injili kamili ya Kristo bila kulazimisha watu kwa hila. Soma Biblia, muombe Mungu akupe hekima, na umshirikishe Roho Mtakatifu akuelekeze mahali sahihi pa kuabudu.

Sadaka inayompendeza Mungu ni sadaka inayotolewa kwa hiari si kwa kulazimishwa.
2 Wakorintho 9:7
"Kila mtu na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
 
Mkuu Seti, Setfree , japo mimi nimefika St. Peter Basilica, na The Holly Bible, nimeisoma yote, mimi sio mtu wa vifungu kihivyo!, ndio maana nilitoa angalizo hili, Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.
P
 
Washenzii wajipatia fursa ni kuzoa mijihela kwa wauumini, wanakondoo wa Bwana.

Wanafaata nyayo za nabii Tb Joshua.
 
Asante sana na Mungu akubariki kwa somo zuri ila hii vita na hawa manabii feki na matapeli wengine wa kiroho ni ngumu maana watu wengi wanazidi kuwaamini na kuwafuata
 
Washenzii wajipatia fursa ni kuzoa mijihela kwa wauumini, wanakondoo wa Bwana.

Wanafaata nyayo za nabii Tb Joshua.
Tusaidiane kupiga kelele watu wajihadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…