DOKEZO Utapeli wa Mtandaoni kwa Wanunuzi wa Pikipiki, Bajaji, na Maguta

DOKEZO Utapeli wa Mtandaoni kwa Wanunuzi wa Pikipiki, Bajaji, na Maguta

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naomba kutoa taarifa juu ya utapeli wa Mtandaoni unaondelea kupitia account ya facebook inayojiita "HONDA AFRICA LTD" na Chanel ya Whatsapp inayojiita "HONDA AFRICA MOTORS"

Binafsi ninayeandika ujumbe huu ni mfanyakazi wa kampuni halisi ya Honda Motor Southern Africa Pty yenye makao yake makuu Mbagala Zakhem na Service Center Kariakoo mtaa wa Congo na Kariakoo.

Hawa wanaojiita HONDA AFRICA LTD wamekuwa wakidanganya wananchi mtandaoni kwamba ni wakopeshaji wa pikipiki, bajaji na maguta ambapo wanabainisha ofisi zao zipo Mkwepu DSM.

Watu hawa wamekuwa wakitumia Jina na logo ya Honda ijapokuwa hawakopeshi pikipiki za Honda, wameenda mbali zaidi na kuchukua picha na video zinazopostiwa katika kurasa zetu halisi na kuweka kwenye kurasa zao kuwaaminisha wananchi.

Tumepokea malalamiko mengi ya wananchi wanaotapeliwa kila siku kupitia kampuni hii na imekua vigumu kuwakamata sababu hawakubali mteja afike ofisini kwao bali hupendelea kumalizana kwa njia ya simu.
whatsapp chanel.jpeg

Random 3.jpeg

With contacts.jpeg
Honda Motor Southern Africa Pty ina kurasa mbili mtandaoni ambazo ni Facebook Bei Facebook anmelden na Instagram Login • Instagram
Hatuna uhusiano wowote na kampuni ya ukopeshaji ya HONDA MOTOR AFRICA LTD na tunapenda kuwatahadharisha wananchi kutokuingia kwenye mtego wa matapeli hawa.
With contacts (1).jpeg

Main page.jpeg
 
Attachments

  • Whatsapp number & lipa number.jpeg
    Whatsapp number & lipa number.jpeg
    52.2 KB · Views: 2
  • With contacts.jpeg
    With contacts.jpeg
    128.1 KB · Views: 2
  • Random 3.jpeg
    Random 3.jpeg
    91.1 KB · Views: 2
  • Main page.jpeg
    Main page.jpeg
    82.2 KB · Views: 1
  • Random2.jpeg
    Random2.jpeg
    126.1 KB · Views: 1
  • Random post with prices.jpeg
    Random post with prices.jpeg
    134.1 KB · Views: 2
  • FB Group.jpeg
    FB Group.jpeg
    49.9 KB · Views: 2
Naomba kutoa taarifa juu ya utapeli wa Mtandaoni unaondelea kupitia account ya facebook inayojiita "HONDA AFRICA LTD" na Chanel ya Whatsapp inayojiita "HONDA AFRICA MOTORS"

Binafsi ninayeandika ujumbe huu ni mfanyakazi wa kampuni halisi ya Honda Motor Southern Africa Pty yenye makao yake makuu Mbagala Zakhem na Service Center Kariakoo mtaa wa Congo na Kariakoo.

Hawa wanaojiita HONDA AFRICA LTD wamekuwa wakidanganya wananchi mtandaoni kwamba ni wakopeshaji wa pikipiki, bajaji na maguta ambapo wanabainisha ofisi zao zipo Mkwepu DSM.

Watu hawa wamekuwa wakitumia Jina na logo ya Honda ijapokuwa hawakopeshi pikipiki za Honda, wameenda mbali zaidi na kuchukua picha na video zinazopostiwa katika kurasa zetu halisi na kuweka kwenye kurasa zao kuwaaminisha wananchi.

Tumepokea malalamiko mengi ya wananchi wanaotapeliwa kila siku kupitia kampuni hii na imekua vigumu kuwakamata sababu hawakubali mteja afike ofisini kwao bali hupendelea kumalizana kwa njia ya simu.

Honda Motor Southern Africa Pty ina kurasa mbili mtandaoni ambazo ni Facebook Bei Facebook anmelden na Instagram Login • Instagram
Hatuna uhusiano wowote na kampuni ya ukopeshaji ya HONDA MOTOR AFRICA LTD na tunapenda kuwatahadharisha wananchi kutokuingia kwenye mtego wa matapeli hawa
Mnatakiwa muishtaki hiyo kampuni kwa kutumia jina lenu,Na hao waliotapeliwa muwatafute ili wawe wateja wenu!
 
Ni michezo yenu hiyo..
Kampuni husika baadhi ya watumishi wasio waadilifu wanafungua account,inayofanana jina na hiyo.
mteja akipatana kwenye kampuni OG,kwenye miamala ela anaambiwa atume kwenye account fake.
Hii michezo ndo alikuwa anafanyiwa psquare muhusika akiwa kaka yao.
 
Nadhani njia nzuri ya kuwashika ni kutrace No. , Pia huenda Jina wanalotumia limesajiliwa TRA na Brela .

Inasikitisha kuona watu wanatapelika kwa Aina hii ya utapeli .
Like unamtumia mtu ela akusajilie pikipiki na hamjawahi kukutana face to face .
 
Na nyie weken logo yenu tuione ikoje isije ikawa ndio wale wale kukwepa kodi TRA maana wabongo hatuchelewi kupindisha michongo ya hela
 
Back
Top Bottom