A
Anonymous
Guest
Naomba kutoa taarifa juu ya utapeli wa Mtandaoni unaondelea kupitia account ya facebook inayojiita "HONDA AFRICA LTD" na Chanel ya Whatsapp inayojiita "HONDA AFRICA MOTORS"
Binafsi ninayeandika ujumbe huu ni mfanyakazi wa kampuni halisi ya Honda Motor Southern Africa Pty yenye makao yake makuu Mbagala Zakhem na Service Center Kariakoo mtaa wa Congo na Kariakoo.
Hawa wanaojiita HONDA AFRICA LTD wamekuwa wakidanganya wananchi mtandaoni kwamba ni wakopeshaji wa pikipiki, bajaji na maguta ambapo wanabainisha ofisi zao zipo Mkwepu DSM.
Watu hawa wamekuwa wakitumia Jina na logo ya Honda ijapokuwa hawakopeshi pikipiki za Honda, wameenda mbali zaidi na kuchukua picha na video zinazopostiwa katika kurasa zetu halisi na kuweka kwenye kurasa zao kuwaaminisha wananchi.
Tumepokea malalamiko mengi ya wananchi wanaotapeliwa kila siku kupitia kampuni hii na imekua vigumu kuwakamata sababu hawakubali mteja afike ofisini kwao bali hupendelea kumalizana kwa njia ya simu.
Honda Motor Southern Africa Pty ina kurasa mbili mtandaoni ambazo ni Facebook Bei Facebook anmelden na Instagram Login • Instagram
Hatuna uhusiano wowote na kampuni ya ukopeshaji ya HONDA MOTOR AFRICA LTD na tunapenda kuwatahadharisha wananchi kutokuingia kwenye mtego wa matapeli hawa.