Utapeli wa ndoa na hatima ya mwanaume kwenye jamii

Utapeli wa ndoa na hatima ya mwanaume kwenye jamii

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Salaam jamiiforum

Si ajabu kuona vijana Kwa wazee wanapishana katika madanguro au sehemu wanapojiuza wanawake.

Yaani vijana umri wa miaka 21 hadi 35 lakini pia kuna umri huu 35 mpaka 55 wote hao wanapishana na kupeana koneksheni ya madanguro (machimbo) mapya.

Hii yote inasababishwa na nini?

1.Maisha magumu kwa wanawake na wanaume?

2.Mazoea mabaya kupenda mteremko haswa Kwa wanaume?

3.Wanawake kujidharau na kujichukulia simple?

4.Ni visasi na kukata tamaa kulingana na mtu alivyotendwa?

5.Au ni watu kukosa uvumilivu na kutoiheshimu ndoa?

Yapo maswali mengi sana lakini yapo majibu Machache tu kwenye haya maswali matano,

Kwanza lazima tutambue kwamba hakuna Jambo zuri lenye kuleta heshima kama kumuoa mwanamke Bikra,naam msichana ambaye hajaguswa kabisa.hii hufanya kuheshimiana katika NDOA na kuilinda

NDOA inalindwa, NDOA inahitaji watu wawili mume na mke walio kwenye utayari hata wakigombanq vipi lakini neno Talaka liwe gumu kwao kulitamka na siyo ,kosa kidogo mwanamke anadai kuachwa.

Moja ya makosa ambayo yanafanywa na wazazi ni kuwalea watoto wa kike Kwa minajili ya kujitegemea zaidi yaani niwe mkweli mzazi anamwambia mwanaye asome Kwa bidii aje kuwa na KAZI yake kwani maisha ya kumtegemea mwanaume yamepitwa na wakati. Anaenda mbali zaidi na kumtisha kuwa kama atakuwa hana kazi na maisha yake ni kumtegemea mume basi atatanyanyasika,hapo inajengeka ile spirit Kwa msichana kwamba ni lazima ajijenge kivyake.

Wanaoharibu mishe za NDOA ni wanawake, mwanaume hajawahi kutotamani ndoa, kila mtu anapenda aoe,kwani ndoa ni heshima na inampa thamani na heshima mwanaume hata aokote makopo kama sehemu ya utafutaji wake ,lakini kitendo cha kujulikana ana mke na watoto. Humuongezea Imani na uaminifu Kwa jamii.

Kinachowafanya wanaume kuogopa kuoa, Kwanza ni kuogopa yafuatayo,

1.kuchapiwa,

Hakuna kitu mwanaume huhuzunika na kusononeka kama kuchapiwa yaani ,mbaya zaidi umjue mgoni wako halafu huna cha kumfanya, mwanamke wa Leo ana tamaa haogopi tena mume,yeye anachofanya ni kutengeneza mazingira asionekane tu basi.

Hapa tunazalisha ,vijana wa kiume wengi wagonjwa wa afya ya Akili , wanaojiua hata kukata tamaa ya maisha, mwisho wa siku kuingia kwenye matumizi ya drugs kama sehemu ya kutafuta furahq.

2.Kutokuheshimiwa,

Ikiwa utaoa mwanamke wa kufanana na wewe Lakini akawa na kazi au kipato kukuzidi,sahau neno heshima,labda kama atakuigizia tu ila kiasili huna cha kumfanya
Mwanamke ana uwezo WA kujenga ana uwezo WA kununua usafiri ana uwezo WA kusimamia miradi yake midogo midogo wewe ni na ushupaze mishipa ya shingo kumkaripia , mwanamke wa leo Hana heshima hata kama hana kitu na wazazi na wake ni masikini,bado mwanamke wa Leo Hana heshima ni ile spirit wanayolishwa na jamii,utandawazi na mwenendo wa Dunia umewaharibu mno

3.Mwanamke kuzaa nje ya ndoa.

Yaani sasahivi mwanamke hana uoga kabisa ,tumezoea kuona wanazaa bila ndoa imekuwa kawaida,lakini kuna hili mwanamke kubeba mimba ya mwanaume mwingine tenq bila hofu wala uoga wowote akiwa ndani ya ndoa,na kumbuka kiumbe kitachozaliwa hakina kosa , wanaume tuna mitihani sana.

Haya ni Machache katika mengi yanayomnyima mwanaume fursa ya kuoa mbaya zaidi Dunia imeegamia upande mmoja, mwanaume ameachwa apambane kivyake ,
Na hapaswi kulia au kuonesha udhaifu fulani.

Anaambiwa awe na Kaba,awe na kifua cha kuvumilia mambo,yaani uchapiwe,uwe katika hatari ya kulea mtoto asiye wako halafu uvumilie tu.

NB: wanawake wazuri bado wapo wengi tu cha muhimu omba Mungu akupe chaguo sahihi.

Lakini pia wanaume ambao hawawezi kuishi na mtu nao wapo ,hawana uwezo wa kusimama imara kuiongoza familia,hawa nao ni chanzo cha kuongeza single mothers wengi mtaani.

Pichani ni baadhi ya wanawake wa kileo ambao pengine ni wake za watu au wachumba wa watu
 

Attachments

  • 20250126_094251.jpg
    20250126_094251.jpg
    89 KB · Views: 7
Mnamkataa Mungu anayewapa road map ya maisha mnafikiri mtafanikiwa kwenye vitu sensitive kama ndoa? Fools!

Wanawake hawana kosa lolote, wako kwenye angle ngumu tu ya ku expose ubaya wao, ila wanaume ubaya wao hauonekani!

Shida ya mwanadamu ni "Dhambi, uasi na kutoka kwenye Mpango wa Mungu" Haya mengine upuuzi tu usio na maana.

Mwanaume:

1. Unaishije bila kuoa? Fool.
2. Mwanamke unatokaje nje ya ndoa?
3. Mwanamke unakimbiaje watoto?

#fools
 
Back
Top Bottom