Utapeli wa wasanii wa bongo movie: Diamond ni mhanga na aliwasema waziwazi

Utapeli wa wasanii wa bongo movie: Diamond ni mhanga na aliwasema waziwazi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nina uzoefu binafsi na hawa watu.. Sio wakuwaendekeza hata kidogo. Ni wabinafsi, ni wachoyo, ni ombaomba hawaridhiki na hawana shukrani.. Ni waongo sana pia na huwa wanajiona ni wajanja kukuzidi

Unaweza kujitoa kuwasaidia sana. Watakupamba sana na kukuganda lakini nyuma ya pazia wanakuona popoyo tu na bonge la mbutika🤬
Watakuonesha rangi zao halisi ukiwanyima kitu, ama ukiishiwa ..! Ni mabingwa wa kukopa lakini kulipa shida.. Ni mabingwa wa kuazima vitu kama nguo lakini kurudisha ugomvi
Kwenye no ndio kabisa. Unaweza ukapangwa wewe mpaka ukaota tege kama si kibyongo. Muulizeni Mond walichomfanya au Harmo!

Wanaowaamini na kuwapetipeti kwasasa majuto hayako mbali.. Dalili zimeshaanza kujionesha kwenye sekeseke la Ngorongoro... Hapo pengine waliomba fungu wakanyimwa!

Natambua wazi baada ya kupandishwa pipa na kwenda kula bata huko kwa wavimba macho... Na hata kupelekwa kule kwenye wiki la tamasha kule visiwani.. Walitegemewa sana watoke na ka script japo kamoja! Lakini wako kimya kama hawapo wala hawaoni yanayoendelea...

Ila wanakinike hasira za mkizimkazi hazipozwi na wimbi la maji kupwa...!

Good night my beautiful Tanganyika❤❤❤
 

Attachments

  • 20240823_203336.jpg
    20240823_203336.jpg
    116.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom