Said Fella na Babu Tale walikuwa mameneja kipindi ambacho hata wao wenyewe walikuwa hawajui nini majukumu yao. Unaposikia mafanikio ya wasanii uliowataja, ni kwamba wale wasanii ndiyo walikuwa wana mchongo. Kama unamzungumzia Nature, nyuma yake kuna mtu anaitwa P Funk. Fella alikuwa amepewa shafu la kuiongoza TMK Family kama braza tu wa Temeke aliyependa muziki, ndiyo maana Nature alipomshtukia ananenepa tumbo wao wanakonda akasepa zake. Unauliza alipo Nature, unajua alipodondokea Fella?
Nature alipoondoka TMK, kundi likayumba na kufa akabakia Mh Temba na Chege wao kama wao na kumbuka TMK haikuwa lebo. Tip Top pia haikuwa lebo ni kundi ambalo Babu Tale aliletwa tu awajue wasanii na ndugu yake ambaye ndiye muasisi wa kuitwa Bonge (rip). Kipindi kile wasanii walikuwa wanaona fashion tu kuona kuna mtu anawasimamia ndiyo maana wasanii wajanja kama Sugu hawakutakaga huo ujinga.
Diamond alipokuwa Sharobaro, jamaa alipata recognition kubwa sana kiasi kwamba akajiona yupo juu, lakini dogo alipoondoka na kuanzisha wasafi unaweza niambia Sharobaro Records imepiga hatua kwenda mbele au nyuma?
Mpeni sifa zake Diamond, acheni kujifanya mnatafuta watu eti ndiyo wamempandisha juu. Hivi mnajua dogo aliwakazia kwa kiwango gani Clouds chini ya yule Mungu wa wasanii hadi wakashindwa?
The boy deserve credit. Fikiria watu wanazungumzia kuhusu yeye kupata tuzo za Grammy