Utapenda namna Babutale, Fella na Sallam walivyo professional kwenye kazi yao

OK TIMU NANILIU NIMEKUPATA BYE
Hahahaha

Rayvanny mbakaji na nasibu nyange, wameanza kuwika kimataifa kitambo sana yani sana, wana mituzo ya bet na MTV, sasa kwa mtu aliyewika kimataifa kitambo tunatarajia sasa awe ana Grammy kama tano. Ziko wapi Grammy awards za nasibu na rayvanny? Na hapa tuko Tanzania , tunaongelea ya watanzania, mana mnasema nasibu kama mtanzania ni tishio kwa burna. sasa basi hadi hivi sasa tunatarajia kwenye kabati kuna tuzo za Grammy za kuelezea "utisho" huo.. Ziko wapi ?
 
Said Fella na Babu Tale walikuwa mameneja kipindi ambacho hata wao wenyewe walikuwa hawajui nini majukumu yao. Unaposikia mafanikio ya wasanii uliowataja, ni kwamba wale wasanii ndiyo walikuwa wana mchongo. Kama unamzungumzia Nature, nyuma yake kuna mtu anaitwa P Funk. Fella alikuwa amepewa shafu la kuiongoza TMK Family kama braza tu wa Temeke aliyependa muziki, ndiyo maana Nature alipomshtukia ananenepa tumbo wao wanakonda akasepa zake. Unauliza alipo Nature, unajua alipodondokea Fella?
Nature alipoondoka TMK, kundi likayumba na kufa akabakia Mh Temba na Chege wao kama wao na kumbuka TMK haikuwa lebo. Tip Top pia haikuwa lebo ni kundi ambalo Babu Tale aliletwa tu awajue wasanii na ndugu yake ambaye ndiye muasisi wa kuitwa Bonge (rip). Kipindi kile wasanii walikuwa wanaona fashion tu kuona kuna mtu anawasimamia ndiyo maana wasanii wajanja kama Sugu hawakutakaga huo ujinga.
Diamond alipokuwa Sharobaro, jamaa alipata recognition kubwa sana kiasi kwamba akajiona yupo juu, lakini dogo alipoondoka na kuanzisha wasafi unaweza niambia Sharobaro Records imepiga hatua kwenda mbele au nyuma?
Mpeni sifa zake Diamond, acheni kujifanya mnatafuta watu eti ndiyo wamempandisha juu. Hivi mnajua dogo aliwakazia kwa kiwango gani Clouds chini ya yule Mungu wa wasanii hadi wakashindwa?
The boy deserve credit. Fikiria watu wanazungumzia kuhusu yeye kupata tuzo za Grammy
 
Jamaa wako very smart kinoma hatar nanunusu
 
Ndio tatizo letu waswahili uwa tunafikiri mambo yanatokea pasipo sababu..Wanasema usione vinaelea vimeundwa...

Kwanza naomba nikuelekeze PFunk hakuwai kuwa meneja wa Juma Nature, P alikuwa ni producer wa Nature na ndie alimgundua ila kazi za management alizifanya Fella mpaka walipokuja kugombana...sasa wewe unasema alikuwa just a brother, ule ugomvi wao ulitokana na nini?

Pia sharobaro haikuwai kuwa label it was just a studio, Bob Junior alikuwa ni producer wa Mondi ila meneja aliyemtoa Diamond aliitwa Papaa na walipotofautiana Diamond alilipa hela ya kuvunja mkataba.

Rayvanny alipopatwa na msala nadhani hukuona Diamond pale akiangaika, waliokwenda polisi kumaliza ishu ni kina Tale. Hiyo ndio kazi ya managers kuakikisha msanii wako yupo salama. Investor amekaa zake Mbezi anapewa ripoti..Kigumu kipi hapa unashindwa kuelewa?


Hapa nachotaka nikueleweshe kusema awa managers wanafanya kazi yao vizuri sio kupuuza uwezo wa Mondi, we all know Diamond sio superman kwamba ataiendesha na atafanya kila kitu wasafi bila kuwa na watu wanaoijua kazi.

Fella, Salam na Tale ni mfano wa kuigwa, kazi wanazofanya kuna watu wameendea shule mpaka nje ya nchi ila ukiwapa wafanye hawawezi. Historia inawabeba ndio maana Mondi alisimama na Salaam yule chinga alipotaka kumletea za kuleta Salaam.
 
Wewe jamaa unachuki zako binafsi
 
Chuki zitakuua mkuu..
Kubali kataa huyo ndo msanii mkubwa Tz au na hili unabisha pia ??
 
Hivi hao ni mameneja au wataalamu wa fitna na ulozi?
 
nmekubali heshima yako kwa wasanii wa WCB mpaka kufikia hatua ya kuwahusisha na tuzo kubwa duniani sio kitoto,kikubwa tuwape subra, japo tuzo zenyewe nazo n kamaznamazingzong mengi mpaka watu wanajitoa kutojihusisha nazo
 

We unayo hiyo tuzo ya grammy...?
 
nmekubali heshima yako kwa wasanii wa WCB mpaka kufikia hatua ya kuwahusisha na tuzo kubwa duniani sio kitoto,kikubwa tuwape subra, japo tuzo zenyewe nazo n kamaznamazingzong mengi mpaka watu wanajitoa kutojihusisha nazo
Kwahusisha sio kuchukua tuzo, tunataka kuona tuzo zao mana wao wameanza mziki siku nyingi kabla ya underground burna boy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi chuki watanzania katu hazitupeleki popote. Hapa walipoufikisha wasafi muziki wa Tanzania siyo pabaya. Ipo siku watashinda. Kuwa na roho za chuki kwa binadamu mwenzako sio uungwana ni umasikini na uchawi. Mimi naamini ili kufanikiwa ni lazima niwe na sprit ya ku-appriciate mazuri wanayofanya wengine. Leo Tanzania na Afrika huwezi kuzungumzia Diamond platinumz. Wewe hata ukimchukia haitatibu njaa zako. Chuki, roho za paka na kuombea wengine mabaya kuashiria Uduni wa maisha uliyonayo
 
Kuna binadamu wengine sijui walizaliwa chooni? Kubishana na watu Aina ya huyo jamaa ni kupoteza wakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…