Utapoteza marafiki wengi wa faida kwasababu ya kutaka kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (65)✍️
Si kila mwanamke au mwanaume ambaye mtakuwa marafiki ni lazima utembee nae au awe mpenzi wako, utapoteza marafiki wengi wa faida kwasababu ya kutaka kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mara zote tendo la ngono hufifisha ukaribu. Unaweza kumwona fulani (ambaye ni rafiki yako) ni handsome au ni mrembo sana na anakuvutia, lakini ukishatembea nae utagundua ni tamaa ndio ilikudanganya. Hivyo ule ukaribu wenu utafifia taratibu mwishowe mawasiliano yenu yatapotea.

Marafiki wengine wabakishe kama akiba yako ya baadae. Unawaona watu wanajivunia mjini kuwa na "connections za kimaisha" ni kwasababu waliwatunza vizuri marafiki wa faida.

ZINGATIA: Baada ya ngono au kukataliwa huwa unakuja upepo wa kumwona mtu uliyetembea nae au aliyekukataa ni kero kwenye masikio, macho, na hisia zako.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Huu ushauri ungewaendea wanawake moja kwa moja

Ni mara chache sana wanawake wanaweza wakawa connection ya mwanaume kutoboa ila ni mara nyingi wanaume wanaweza wakawa connection kwa mwanamke kutoboa
 
Itajulikana mbele kwa mbele ila vocal muhimu maana Kuna kuchukuliana poa
 
📖Mhadhara (65)✍️
Si kila mwanamke au mwanaume ambaye mtakuwa marafiki ni lazima utembee nae au awe mpenzi wako, utapoteza marafiki wengi wa faida kwasababu ya kutaka kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mara zote tendo la ngono hufifisha ukaribu. Unaweza kumwona fulani (ambaye ni rafiki yako) ni handsome au ni mrembo sana na anakuvutia, lakini ukishatembea nae utagundua ni tamaa ndio ilikudanganya. Hivyo ule ukaribu wenu utafifia taratibu mwishowe mawasiliano yenu yatapotea.

Marafiki wengine wabakishe kama akiba yako ya baadae. Unawaona watu wanajivunia mjini kuwa na "connections za kimaisha" ni kwasababu waliwatunza vizuri marafiki wa faida.

ZINGATIA: Baada ya ngono au kukataliwa huwa unakuja upepo wa kumwona mtu uliyetembea nae au aliyekukataa ni kero kwenye masikio, macho, na hisia zako.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
Hili swala naona ni zito kwangu na kwa baadhi ya vijana na wanaume wa aina au wenye akili kama yangu, sijasema na akili punguwani NO hapana.

Swala la urafiki wa jinsia mbili tofauti katika eneo moja (Kijiji, mtaa au kitongoji) ni kitu kigumu sana kwa Karne hii ya 21 lazima pawe na NEGATIVE RELATIONSHIP.

Vinginevyo tutadanganyana sana. Goja niweke kituo kwanza hapa.
 
Nimesoma hii mada halafu nikaanza kuhesabu mademu ambao niko nao karibu na hatuna issue za kukulana nimegunduwa ni ujinga mtupu.
 
Huu ushauri ungewaendea wanawake moja kwa moja
NAUNGA MKONO HOJA.

Wanawake wanapenda kuwa na urafiki na Wanaume kuliko Wanaume. Kwasababu wanawake hawana vingi vya kumpa mwanaume ila Mwanaume anakuwa na vingi vya kutoa - so mara nyingi huwa sio Urafiki wenye manufaa kabisa kwa Mwanaume.

Kila kitu ambacho mwanaume atahitaji kukipata kutoka kwa Rafiki, basi anaweza kukipata kwa rafiki yake wa kiume katika uwingi wa kutosha na kwa haraka zaidi. Vilevile Rafiki wa kiume hatakuwa mzigo kwake na pia thamani atayoipata kwa rafiki wa kiume huwa ni kubwa.

Mara nyingi urafiki na mwanamke huwa ni wa upande mmoja, kwasababu wao ni wana hisia sana na Ujinga mwingi, so utajikuta mara nyingi urafiki wenu ni kama Mwalimu na Mwanafunzi (kumsaidia sana) kuliko kuwa mutual.

Unless unampenda mwanamke kama DADA, MAMA, MKE, MPENZI - ila kuwa na Urafiki na mwanamke katika mazingira halisia ya kimaisha ni kujipa mzigo usiokuwa na faida kama ni Mwanaume uliyekamilika.

Wanawake ni wazuri pale unazungumza na kuchat nao vitu fulani vya kihisia(Flirt), hiyo ni kitu pekee ambayo huwezi pata kwa rafiki wa kiume. Vilevile kama ni Mwanaume wa kulialia, kusikitika sana na unahitaji mtu wa kukusikiliza basi rafiki wa kike atakufaa kwenye hilo.

Mazingira kama kazini, kwenye Biashara na connection za kazi hazihitaji uwe na urafiki na mwanamke ili akupe connection, hizo zinahitaji kufahamiana tu na sio URAFIKI.

Be a Man, Rafiki wa kike hana kikubwa atakachokupa ambacho utakikosa kwa rafiki wa kiume.
 
ZINGATIA: Baada ya ngono au kukataliwa huwa unakuja upepo wa kumwona mtu uliyetembea nae au aliyekukataa ni kero kwenye masikio, macho, na hisia zako.
Dah hii ni ukweli mtupu.
Mwezi wa 10 tuu ....

1. Kuna binti katoka chuo nikawa mshauri wake mzuriii.
Dah kuna siku akanikuta bar, nikamnunulia flyiing fish 4 tu mara yupo hoi.
Nikaenda nikamla, tokea siku hiyo sijawahi tena ongea nae na namba nishafuta..!!!

2. Kuna mdada bonge la shape, alikuwa rafiki yanguu. Tatizo lolote la ofisini kwangu ananifahamisha.
Juzi kati tumegongana kimasihala, Dah hata simu zake kupokea naona shida siku hizi.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Ukweli ukitanguliza sex, huwezi kufanikisha chochote
 
Hii inawahusu wanachuo na vijana wadogo
Nimeona watu wazima wanapigana mistari wanachomoana kwa busara na bila kelele na urafiki unaendelea kama kawaida.
Hawa wake zetu wanakutana na mengi na wengi - mitongozo mingi sana wangekua kila anayewapiga sound anakuwa adui au wanafuta ukaribu..kuanzia mitaani, makanisani, misikitini, kwenye jumuiya, maofisi..wangekuwa hawazungumzi na watu.
 
Ukweli ukitanguliza sex, huwezi kufanikisha chochote
Inategemea mnadeal na wanawake gani, kuna mheshimiwa hakimu moja tulikulana, nilishalichomoa jitu mahakamani kwa kesi ambayo dhamana alishakataliwa lakini kuniona tu kwa heshima yangu akampa bond ya maandishi.

Hivi mnataka wanawake wawasaidie nini sasa? Jamaa yangu anatoka na corporate director wa bank fulani pesa ikishakuwa wired tu ulaya mshkaji kama anashida ya pesa anampa kabla haijasoma kwenye account.

Kuna wadada wanauza msosi mzuri sana yani catering fulani hivi hawa ni washkaji zangu sana muda wowote nakula au napiga simu mtu anahudumiwa hizi zote ni benefit ni vile tu hamjui jinsi ya kuishi nao.
 
Nimesoma hii mada halafu nikaanza kuhesabu mademu ambao niko nao karibu na hatuna issue za kukulana nimegunduwa ni ujinga mtupu.
Mbona kama hizi kauli zinapingana!!!🤔🤔🤔
Inategemea mnadeal na wanawake gani, kuna mheshimiwa hakimu moja tulikulana, nilishalichomoa jitu mahakamani kwa kesi ambayo dhamana alishakataliwa lakini kuniona tu kwa heshima yangu akampa bond ya maandishi.

Hivi mnataka wanawake wawasaidie nini sasa? Jamaa yangu anatoka na corporate director wa bank fulani pesa ikishakuwa wired tu ulaya mshkaji kama anashida ya pesa anampa kabla haijasoma kwenye account.

Kuna wadada wanauza msosi mzuri sana yani catering fulani hivi hawa ni washkaji zangu sana muda wowote nakula au napiga simu mtu anahudumiwa hizi zote ni benefit ni vile tu hamjui jinsi ya kuishi nao.
 
📖Mhadhara (65)✍️
Si kila mwanamke au mwanaume ambaye mtakuwa marafiki ni lazima utembee nae au awe mpenzi wako, utapoteza marafiki wengi wa faida kwasababu ya kutaka kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mara zote tendo la ngono hufifisha ukaribu. Unaweza kumwona fulani (ambaye ni rafiki yako) ni handsome au ni mrembo sana na anakuvutia, lakini ukishatembea nae utagundua ni tamaa ndio ilikudanganya. Hivyo ule ukaribu wenu utafifia taratibu mwishowe mawasiliano yenu yatapotea.

Marafiki wengine wabakishe kama akiba yako ya baadae. Unawaona watu wanajivunia mjini kuwa na "connections za kimaisha" ni kwasababu waliwatunza vizuri marafiki wa faida.

ZINGATIA: Baada ya ngono au kukataliwa huwa unakuja upepo wa kumwona mtu uliyetembea nae au aliyekukataa ni kero kwenye masikio, macho, na hisia zako.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
kupiga sound muhimu, eti urafiki wa kawaida na mwanamke! huo kama sio ujuha ni nini? hakuna urafiki wa jinsia mbili tofauti, napinga vikali. vinginevyo huyo jamaa atakua shoga tu.
 
Back
Top Bottom