Hivi vitu vinataka uelewa na kujaribu ili uthibitishe, wala haina sababu ya kubishana, binafsi nimefanya sana na ndio inashauriwa pale unapotaka ku overtake especially kwenye high way unapo overtake malori, mabasi marefu yakiwa kwenye speed ya 80+kph.
Kuna suala hapo jamaa pia kasema kuwa overdrive ni gia ya tano, siwezi kubisha pengine gari yake iko hivyo, lakini wengine tumeona kwemye gari ambazo zinahesabu gia kwenye dashboard pale inaonyesha kadri unavyoenda na ukizima O/D haivuki gia 3 na ukiwasha inaongeza mpaka ya 4 na haizidi hapo, jambo hilo lilitosha kunisukuma nidadisi na kujifunza kuhusu kitu hicho zaidi.
Kwa ufupi O/D ni economy feature, inaruhusu output shaft izunguke tofauti na input shaft, hivyo unakua na kasi lakini katika rmp ndogo, hence hutumii mafuta mengi, kwa lugha ingine ukifika kuanzia say 70kph na kuendelea OD itawezesha shafts zizunguke zaidi ya engine inavyozunguka, na gari ita accelerate kwa momentum zaidi.
Sasa katika mazingira hayo ukitaka ku overtake, utakanyaga kibati, baadhi ya gari zita detect na computer itapangua gia itashusha kwenda za chini ili rpm iweze endana na output shaft plus gari ipate nguvu na kasi hivyo rpm zitapanda. Lakini kwa anaefahamu anaweza kufanya kitu hicho hicho manually kwa kushusha gia kutoka D kwenda 2.
Kwa wanaoendesha manual ndio wanaelewa sana hii mambo, kwanza gari nyingi manual ni 5 speed gears, uakiacha reverse gear, sasa akiwa kwenye kuanzia gear ya 4 au 5 halafu anataka kumpita ambaye nae yuko kasi lazima apangue gia ili apate nguvu ya kumpita.
Tuendelee kujifunza.