Gari nyingi za automatic huwa zina gia 4 ukiacha ya reverse, O/D ikiwa off maana yake gari haitafikia ile top gear, yaani itajibadilisha hadi gia ya 3 tu basi haitazidi hapo.
Mara nyingi uatumia hii ikiwa unapandisha kamlima au unashuka hasa ukiwa unashuka ili gari isiwe na kasi kubwa na pengine ika over rev, yaani ikiwa inashuka unawesa kuta rpm zinakwemda hadi 5k na kama dereva haelewi anaweza sababisha matatizo kwa engine.
Vivyo hivyo L itaishia gia 1, 2 itaishia gia ya 2 na 3 itaishia ya 3 kama gari yako ina option hiyo, na hizo gear ni kubwa maana yake zina nguvu zaidi na zinakula mafuta pia, uyaona hata ukiziweka mshale wa rpm unaenda juu zaidi ya 3k kama unakanyaga mafuta sana, hivyo zitumie kama kwenye matope au mchanga na pengine kuvuta gari, ila kwa ujumla tumia kwa tahadhari na kwa kuelewa.
Matumizi ya gear hizi L na 2 hasa 2 pia ni kwenye overtaking, unapotaka kumpita mtu ukiwa kwenye D ni risk sababu unaweza kuwa gear ya juu mfano 3 au 4 halafu ukachukua muda kumpita, kumbuka unaempita pia hajasimama na anaenda, sasa ukishusha gear lever kwenye 2 gari itaongeza nguvu na kasi halafu ukishampita unarudisha kwenye D maisha yanaendelea.
I hope nitakua nimesaidia kufafanua.