Utaratibu ukoje kwa Mwanamke ambaye hataki kumwachia mtoto aishi na Baba yake na anadai matumizi "Child Support" kwa nguvu?

Sijui kama umetafiti labda ni kwasababu una uelewa mdogo wa hicho unachomaanisha.

Mimi ni kitu nimeobserve siongei hapa kwasababu nasikia watu wanasema au nimehadhithiwa ni jambo naona.

Unaweza sema unampenda mtoto ila matendo yako ni zero hiyo inamaanisha kuwa wewe ni muongo na haupo serious.

Mwanamke au mwanaume aliyeserious na mtoto au familia yake utaona matendo yake. Hutosikia mtoto anaumwa, hutosikia mtoto anapitia sijui hali gani.

Wanawake wa siku hizi picha linaanza unamkabidhisha mtoto kwa housegirl ndio awe mlezi wako au mama yako akulelee wewe kazi kupuyanga na maisha kufanya purukushani ambazo ukipima mwaka mzima umeingiza nini unaona hakuna la maana umepoteza muda wako tu.

Unampima mwanamke au mwanaume mapenzi yake kwa mtoto kutokana na namna anachagua mama au baba wa mtoto.

Wewe unaenda kutana na mvuta bangi huko vichochoroni halafu unakuja tuambia unapenda mtoto kwa kumpa malezi ya misukosuko.

Kuna mabinti wapo very strong and nawapa heko hawajakubali kuzaa kibwege nje ya mahusiano halali hadi leo wakijua hasara yake.


So achana na maneno ya kusema unapenda mtoto au watoto kama haujawatengenezea mazingira mazuri ya familia ya baba na mama. Hayo mengine ni maigizo tu.
 
Eeh..watajua hawajui... Shwain kabisaa!! Kama sijui kulea angeonekana hata kwenye hiyo picha?
Napiga nao picha coz their my pride! Hapo utakuta libaba lisilohudumia hata 100 linakuja kuiba picha..hahahahaa!
Sasa kama kupiga picha ndio kulea uwe unamuachia baba yao nae apige nao picha ili iwe ndio namna yake ya kulea na wewe.
 
Sasa kama kupiga picha ndio kulea uwe unamuachia baba yao nae apige nao picha ili iwe ndio namna yake ya kulea na wewe.
kupiga picha ni matokeo ya malezi mema, so Yeye atasubiri tuu za kuibia bia..maana kulea kumeshamshinda.
 
Una shilingi ngapi kwenye account yako. Kama our kids is our everything ungeanza kwa kuwaheshimu kwa kuwajengea mazingira ya familia bora ili waje kufurahia dunia.

Sio mtoto anashangaa kila mwezi anabadilishiwa baba tofauti.
Sasa umeongea nini?
 
Wewe mahusiano ya Ex wako yanakuhusu nini...Wewe focus kwenye malezi ya mwanao.Acha kutafuta visingizio.
 
Unaweza kudhani ni u-strong kumbe ni utasa teh
Point yangu ni kuwa usimjudge mtu kwa vile unavyomuona kwa nje pasipo kujua undani wake
 
Kwanza unatakiwa ufahamu kuwa,
1. Kuna umri wa baba kuishi na mtoto wake. nadhani ni kuanzia miaka 7. Chini ya hapo anatakiwa aishi na mama.
2. Mama naye kuishi na mwanae lazima awe na uwezo wa kumtunza. Siyo yeye anaishi kwa baba yake halafu anang'ang'ana kuishi na mtoto
3. Mama lazima awe anaishi mazingira mazuri ya kulelea mtoto. Siyo mtoto anafunguwa ndani mama safari kudanga. hapo lazima baba apewe mtoto
4. Ukiona unasumbuliwa sana nenda dawati. Nina mtu namfahamu baada ya kushindana sana alikwenda dawati na amepangiwa kulipa laki 1 kwa kila mwezi
 
Kwan wanawake wa siku hiz hawaombi msaada kwa mahousegirl? Tena unakuta hajui ata kama mtoto wake kaoga ula yeye kila kitu ni ku-order tu dada muogeshe mtoto dada mtoto amekula? Dada mtoto kalala ? Hakuna anachojihusisha nae ata anapokuwa nyumban
 
Wanaupima upendo kwa kuconsider materials things kama walivyo pima upondo kwa waliozaa nao. Wanasahau kuwa upendo kwa mtoto unaangalia mambo mengo zaidi ya vitu unavyo mnunulia
 
Wewe mahusiano ya Ex wako yanakuhusu nini...Wewe focus kwenye malezi ya mwanao.Acha kutafuta visingizio.
Hapa unapotoka sana. Hii kitu ni yakuzingatia sana maana mtu aliye kwenye mahusiano na mzazi mwenzio anaweza kuhathiri pakubwa sana malezi/maadili ya mtoto wenu
 
Mkuu,SIRI ni moja tu.Mtoto akitaka matunzo lazima aje kwako kila week end muonane mcheze umnunulie zawadi kisha unga kilo mbili na mchele kilo mbili na buku mbili ya mboga.Tena unampa mtoto.Full stop.Hataki ujue ni kiranga hicho
Unyama sana hapa [emoji3][emoji3]
 
Hapa unapotoka sana. Hii kitu ni yakuzingatia sana maana mtu aliye kwenye mahusiano na mzazi mwenzio anaweza kuhathiri pakubwa sana malezi/maadili ya mtoto wenu
Ni kweli, lakini na mimi kwa ustawi wa mwanangu, siwezi kuanza kutoka na mwanaume asiyeeleweka.

Na pia, itachukua muda kumtambulisha huyo mwanaume kwa mwanangu.Siwezi tu kumtambulisha kila mtu kwa mwanangu

Pia, wanaume wengi hawataki mzazi mwenzie amove on ila yeye mwenyewe ana haki ya kumove on.
 
SawA mkuu nmekuelewa

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…