JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kutokana na changamoto ambazo zimekuwa zinawakumba Watu wenye ulemavu pamoja na wale wenye mahitaji maalumu pindi wanapotumia usafiri wa umma, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar (DART) ilijipambanua kwa kuzingatia kipaumbele cha huduma rafiki kwa makundi hayo suala ambalo lilipigiwa chapuo.
Urafiki wa huduma ambao ulikuwa umejengewa msingi kuanzia kwa watoa huduma kwenye vituo kutoa kipaumbele cha watu hao umetoweka, kwenye magari huko ndiko kabisa.
Awali, ndani ya mwendokasi kulikuwepo na uwajibikaji uliotokana na usimamizi na ufuatilia wa karibu kama watu wenye ulemavu wamepewa huduma rafiki, ambapo kwenye gari hizo kuna maeneo maalum kwa ajili ya watu hao, siku hizi unakutana na Mtu mwenye ulemavu amesimama kwa taabu kwenye usafiri wa Mwendokasi.
Kwa sasa kutokana na uhaba wa magari hali imekuwa mbaya zaidi, ambapo usafiri huo umekuwa wa kuchuana, jambo hilo limeongeza ugumu wa makundi mbalimbali yanayohitaji uangalizi maalumu hususani wajawazito na watu wenye ulemavu kutumia usafiri huo, ambapo wengi wamekata tamaa na kuona usafiri huo sio rafiki tena kwao.
Wito wangu kwa mamlaka ni muhimu kuendelea kuweka msisitizo wa kuzingatia huduma rafiki na kipaumbele kwa makundi hayo ili nao waweze kufurahia huduma kama sehemu ya watanzania wengine.
Lakini pia ni vyema mamlaka zikaongeza jitihada za haraka kupunguza changamoto ya uhaba wa magari ili kuondoa msongamano ambao unaweka hatarini afya za watu wenye ulemavu.