Utaratibu wa kuhama kwa Watumishi wa umma kwenye mashirika ya umma ukoje?

Utaratibu wa kuhama kwa Watumishi wa umma kwenye mashirika ya umma ukoje?

Hivi wanakubali kweli kuhamisha. Maana taasisi X unakuta mshahara ni mdogo kuliko taasisi Y. Au mm sijaelewa hapa.? Naweza nikatoka ofisi ya maliasili nikahamia tpdc bila kufanya interview huko tpdc. Maana kila taasisi inamfumo wake, vinginevyo itangazwe ajira uombe, ukipata kazi uteme bungo la kwanza then uhamie hiyo taasisi mpya. Waajiri wengi ukishamtonya nataka nihamie taasisi fulani atakuitikia ndio ndio (safi sana hayo ndio mawazo ya kimaendeleo kijana wangu) gues what, haipiti wiki linakuja bonge la waraka wa Yohana mbatizaji kwa bosi wa mkoa Huku likipambwa na muhuri was SIRI KICHWA CHA HABARI CHAKE SASA ( KWA WATUMISHI WOTE) nimarufuku kuomba Kazi taasisi nyingine. Hapo lazma ujiulize kwa nn niliropoka.
 
Hili la siku siku 21 linakuwaga kama halina ukweli mtu unaandika barua inakaa siku 60 hakuna jibu lolote ukipiga simu unaambiwa inafanyiwa kazi ukienda dodoma unaambiwa tunaifanyia kazi yaani document zote zipo umeweka daa jamani.
 
Akimaliza hapo, ile Barua yake aliyoiandika kwenda Taasisi X atajibiwa (coz alishaomba nafasi wakamruhusu!

Majibu yatatolewa kwa Maandishi (barua) kwenda kwa Mwombaji na Copy kwenda kwa Mwajiri.

Mwombaji ukishapata barua yako kutoka Taasisi X kuwa Umekubaliwa kuhamia... Utaandika Barua kwenda kwa KTB MKUU UTUMISHI ukimuomba kuhamia Taasisi X. Barua hii itapitia tena kwa Mkuu wako.

Safari hii barua hii itaambatana na ile ilotoka Taasisi X.

Pia barua hii itakuwa na ATTACHMENTS zingine zote zinazohusu UTUMISHI wako ukiweza weka na report ya UHAKIKI.

Barua hii unaweza kutuma kwa POSTA japo ni vzr uipeleke mwenyewe physically MTUMBA, MTAA WA SERIKALI au UTUMISHI UDOM. Kwenye barua yako usisahau kuweka sentensi hii: GHARAMA ZA UHAMISHO HUU NI JUU YANGU.

Utumishi wataingiza Maombi yako ktk mfumo wao wa kielektroniki na wewe utapata SMS kuwa maombi yako yamefika.

Muda wa kushughulikiwa maombi yako ni siku 21 na baada ya hapo ruksa kuanza kuulizia status ya Maombi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi km utaandika moja kwa katibu mkuu kupitia kwa mwajiri na unakotaka kuhamia ambapo atacoment nafasi ipo...si inakubalika hii
 
Asante kwa swali zuri, mtumishi anayetaka kuhama tok taasisi moja Kwenda nyingine anatakiwe kwanza ahakikishe kule anakotaka Kwenda Kuna nafasi, na pia aandike barua kupiti mwajiri wake Kwenda anakotaka kuhamia ili kuomba kuhamia huko. Ndio utaratibu huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nawezaje kujua kama ninakoenda kuna nafasi?
 
Nawezaje kujua kama ninakoenda kuna nafasi?
Nachojua Pia naweza kusahihishwa, unaomba kazi ukishapata kama ni Kwa interview au vipi ndio unaanza process ya kuomba Kwa mwajiri wako WA awali. Cha kufanya unajisajili ajira/recruitment portal ajira ikitangazwa unaomba muhimu iwe kwenye fani yako baada ya interview kama utapata ndio ushughulikie kuhama. Pia naamini ziko njia nyingine kama wadau walivyoeleza hapo juu. Angalizo epuka kujisajili na taarifa za kibashite utaumbuka.
 
Hapa inakuaje kama utaomba kazi na kufanya interview then unafaulu tatizo linakuja kama hujathibitishwa kazini utaweza kuhama kweli?..bila kumaliza mwaka hapo ulipoajiriwa?
 
Namimi nimeanza kazi halmashauri x Nina miezi 5 kazini Bado sijathibitishwa kazini. Ila Kuna taasisi y nikaenda kuomba part time job coz muda huo tulikua idle hakuna kazi yoyote ninayoifanya pale halmashauri x. Sasa Yule mkuu wa taasisi y akasema Kama mungu umekuja akaenda kuomba kwa mkurugenzi akakubaliwa Kama nimeazimwa na taasisi y kutoka halmashauri x. Ila sijapelekwa kule kimaandishi ni kwa mdomo tu bosi wangu kaniambia nenda ila ukaeukijua tukikuhitaji utarudi hiyo imekaaje Kuna uwezekano wa kusepa kweli hapo. Na halmashauri x na taasisi y zote zipo chini ya mkurugenzi mmoja.
 
Akimaliza hapo, ile Barua yake aliyoiandika kwenda Taasisi X atajibiwa (coz alishaomba nafasi wakamruhusu!

Majibu yatatolewa kwa Maandishi (barua) kwenda kwa Mwombaji na Copy kwenda kwa Mwajiri.

Mwombaji ukishapata barua yako kutoka Taasisi X kuwa Umekubaliwa kuhamia... Utaandika Barua kwenda kwa KTB MKUU UTUMISHI ukimuomba kuhamia Taasisi X. Barua hii itapitia tena kwa Mkuu wako.

Safari hii barua hii itaambatana na ile ilotoka Taasisi X.

Pia barua hii itakuwa na ATTACHMENTS zingine zote zinazohusu UTUMISHI wako ukiweza weka na report ya UHAKIKI.

Barua hii unaweza kutuma kwa POSTA japo ni vzr uipeleke mwenyewe physically MTUMBA, MTAA WA SERIKALI au UTUMISHI UDOM. Kwenye barua yako usisahau kuweka sentensi hii: GHARAMA ZA UHAMISHO HUU NI JUU YANGU.

Utumishi wataingiza Maombi yako ktk mfumo wao wa kielektroniki na wewe utapata SMS kuwa maombi yako yamefika.

Muda wa kushughulikiwa maombi yako ni siku 21 na baada ya hapo ruksa kuanza kuulizia status ya Maombi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nimeupenda ufafanuzi wako!!!

Naomba nami unielekeze hapa

Mimi ni mtumishi mtendaji wa kijiji lakini sasa nina degree ya upande wa ardhi nahitaji kufanya kazi idara ya ardhi kama unavyojua kwa sasa ardhi haipo tena chini ya halmashauri.... Nifanye nini Au nifate taratibu zipi ili niweze kuhamia idara ya ardhi
 
Nakereka sana na Waajiri wanao zuia watumishi kuhama. Na bado wanapowazuia hawawapi nafasi ya kuonesha utendaji wao zaidi ya kuwapiga majungu.

Unakuta mtu anasifa za kutosha anataman kutafatu sehemu ambayo ataonesha impact ya kile alichonacho kama professional, lakini mwajiri anamkwamisha na bado anamzuis kuhama.

Humu kuna waajiri wengi sana, mnatushaurije tunaokutana na hali kama hizi!
 
Gambino
Hapa naona mnalishana matango pori! Hakuna horizontal transfer katika mashirika ya umma. Horizontal transfers zinawezekana katika idara za serikali, yaani mtu unaweza kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa. Au kuhama kutoka serikali kuu kwenda shirika linalifanya kazi moja kwa moja na wizara inayohusika kwa mfano kutoka DAWASA kwenda wizara ya maji au Chuo cha maji.

Mashirika mengi ya umma ni autonomous yanajitegemea kwa kwa kila kitu. Mtu hawezi kuhama kutoka UDSM kwenda TANESCO isipokuwa kama nafasi ya kazi itatangazwa na wewe kuiomba na kuchaguliwa. Mashirika ya umma yana salary scheme zinazotofautiana, kwa hiyo ukiajiriwa katika shirika lingine unaanza ajira upya na hakuna muendelezo wa ajira ya shirika lako la mwanzo.
 
Umemaliza Mkuu
 
Umemaliza Mkuu
Sio kweli!
Hata mashirika ya umma kwa sasa kila kitu kinawezekana, na karibia Mashirika yote yako chini ya ya wizara UTUMISHI.

na Wizara imekuwa iki regulate viwango vya mishahara kwa mashirika ya Umma
 
Nakala la vyeti vya taaluma (kuanzia Sekondari, chuo n.k)
Barua ya ajira yako ya mwanzo na barua ya kuthibitishwa kazini kama ipo

Sent using Jamii Forums mobn
Nimekua nasikia mabos na watu weng wakiwa wanasema ukiwa ujathibitishwa kazin huwez kuhama,JE hili lina ukweli gan na JE NI sheria au ni maneno tu....maana kuna jamaa nawajua nilipata nao ajira na wamehama bila ata kuthibitishwa..Apo ndo nachanganyikiwa, Uku mimi napata vikwazo et mpaka nikae miaka 2 ad 3 ndo naweza kuhama
 
Mkuu nimeupenda ufafanuzi wako!!!

Naomba nami unielekeze hapa

Mimi ni mtumishi mtendaji wa kijiji lakini sasa nina degree ya upande wa ardhi nahitaji kufanya kazi idara ya ardhi kama unavyojua kwa sasa ardhi haipo tena chini ya halmashauri.... Nifanye nini Au nifate taratibu zipi ili niweze kuhamia idara ya ardhi
Daah swali lako halijajibiwa hadi leo. Akina Slim5 na Ileje mje kusaidia huku haya mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimeupenda ufafanuzi wako!!!

Naomba nami unielekeze hapa

Mimi ni mtumishi mtendaji wa kijiji lakini sasa nina degree ya upande wa ardhi nahitaji kufanya kazi idara ya ardhi kama unavyojua kwa sasa ardhi haipo tena chini ya halmashauri.... Nifanye nini Au nifate taratibu zipi ili niweze kuhamia idara ya ardhi
Mi nakushauri kwanza ukaongee na Afisa Utumishi wako, akupe jinsi ya kufanya. Kama kuna uwezekano wa wewe kufanyiwa "recategorization" hapo hapo Halmshauri ama nini kifanyike....Mfate Afisa Utumishi umuombe Muongozo.
 
Back
Top Bottom